Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, April 2, 2024

MWENYEKITI MRFA AGAWA MIPIRA NDANI YA UCHAGUZI MKUU WA MDFA.



Kiongozi wa timu ya Mkundi United Velonica Michael akikabiudhiwa bori na Mhe Kihanga

Huyu ni kocha Hussein Mau aliyeibu na kuendeleza vipaji vya wachezaji wengi nyota wanaong’a kwa sasa ligi kuu ya Tanzania. Baadhi ya wachezaji hao ni Shomari Kapombe,Mzamiru Yassin Selemba wanaokiiga Simba. Dickson Job, Shomari Kibwana, Abuutwarib Msheri. na Nikson Kibabage [Yanga]. Wengine ni Pascal Msindo [Azam] Hamad Waziri[Kuku] Singada Fountain Gate. Na Shiza Kichuya[JKT Tanzania].

Kwa sasa Kocha Mau ametoka kwenye  taasisi hiyo ya Moro Kids na kujiunga na taasisi ya Tanzanite Soccar Academy .

Kocha Mkuu wa timu ya Mafisa United Yahya Ally Jangalu akikabidhi Mpira na  Mhe Kihanga. Yahya ni mtoto wa kwanza wa Kocha Ally Jangalu ambaye hivi karibuni alikuwa kocha msaidizi wa Kagera Sugar ya Bukoba.

Baadae Kocha Jangalu alimua kutoka Kagera na kuja nyumbani kwao Morogoro na kuanzisha Academy yake ya kukuza na kuibua Vipaji vya soka kwa watoto wa kiume.

Mhe Kihanga akizungumza baada ya kugawa miira hiyo miya kabisa iliyochanwa kwenye boksi

 


          Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Mhe Pascal Kihanga juzi amegawa zawadi ya Mipira  27 kwa Vilabu 27 vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA.’

Kama hiyo haitoishi Mhe Kihanga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, alimkabidhi zawadi ya Mipira 2 Mwenyekiti Mpya MDFA  Mhe Selestin Mbilinyi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Lukobe.

Akizungumza mara baada ya kugawa mipira hiyo Mhe Kihanga alisema.

“ Nimeamua kuwapa zawadi ya mpira mmoja viongozi wa timu zote 27 zilizoshiriki uchaguzi huu kwa lengo la kukuza mchezo huu  kwenye wilaya yenu ya Morogoro.’’ Alisema Mhe Kihanga.

Angalia picha zaidi za viongozi wa timu hizo hapo chini akiwemo Mtoto wa kocha Maarufu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...