Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, March 31, 2024

DIWANI MWINGINE ATWAA UWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA WILAYA YA MOROGORO.

Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro Mhe Pascal Kihanga akizungumza na wajumbe wa mkutano Mkuu wa chama cha Soka Morogoro

Wagombea wa nafasi ya Uwemyekiti Selestn Mbilinyi Kulia na Jofrey Mwatesa wakiingia ukumbini jana
Mwatesa akinadi sera zake na kuomba kura kwa wajumbe
Selestini Mbilinyi akiomba kura kwa wajumbe baada ya kunadio sera zake
Mhe \Godfrey Ng'itu naye akiomba kura kwa wajumbe huku akisisitiza jambo
Mgombe nafasi ya Ujumbe wa mkutano Mkuu wa MRFA Alfrey Mdende akiomba kura kwa wajumbe
....Wagombe wote wakishuhudia saduku la kura likihesabiwa
Hapo sasa, Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi   Wakili Michael Mwambenga akitangaza matokeo
....Mhe Mbilinyi akisimama kwa furaha baada ya kutangza mshindi
......Kundi la wajumbe wakiwaongeza washindi wawili Mbilinyi na Mdende
Kikao mkakati, 

Mwenyekiti wa chama cha Soka  Mkoa wa MorogoroMRFA  Mhe Pascal Kihanga ambaye ia ni diwani wa kata Mazimbu[kulia] akimpa maelekezo  Mwenyekiti Mpya wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro Mh Selestin Mbiilinyi ambaye ia ni diwani wa kata ya Lukobe

Mwenyekiti Mbilinyi akizungumza baada ya kutangazwa mshindi.


 Mh Kihanga akizungumza baada ya mchakato huo wa uchaguzi kukamilika


Na Dustan Shekiodele,Morogoro.

BAADA ya danadana nyingi hatimaye  chama cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’ kimefanya uchaguzi nakufanikiwa kupata Viongozi wapya huku Diwani wa kata ya Lukobe Mhe Selestin Savin  Mbilinyi akifanikiwa kuwa Big Boss wa Chama hicho.

Uchaguzi huo wa kiporo,umefanyika jana March 30 kwenye ukumbi wa Mbaraka Mwinshehe  unaomilikiwa na halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Wajumbe 54 kutoka wilaya mbili za Morogoro Vijijini na Morogoro ,Manispaa zilizounganishwa kuunda wilaya moja ya kisoka,walishiriki kwenye Uchaguzi huo  uliogubikwa na Mizengwe kibao,hasa kwenye Group la Whatspp la Chama hicho.

 Takribani mwezi nzima Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia baadhi ya wagombea na wapiga kura wakipigana vijembe kuelekea uchaguzi huo.

Katika hali ya kushangaza licha ya heka heka zote hizo za uchaguzi huo zilizodumu takribani mwaka mmoja wajumbe hao 54 baadhi yao waliosafiri kutoka maeneo mbali mbali ya Morogoro Vijijini kama vile Kisaki, Matombo,Mvuha, Kinole Mkuyuni, Ngerengere, Kizuka, Kinonko, Ubena, Bwawani na Mikese walipiga kura kuchagua viongozi wawili pekee, Mwenyekiti na Mjumbe wa Mkutano Mkuu.

Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti Wagombea walikuwa watatu, Mhe Mbilinyi, Godfrey Ng’itu na Jofrey Mwatesa ambaye hadi uchaguzi huo unafanyika jana alikuwa akishikiria nafasi ya  katibu Mkuu wa chama hicho.

Nafasi ya Pili ilikuwa ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’wagombea walikuwa watatu.

Hamis Hassan Kiwenja.Amiri Mussa Amiri na Alfred Mdende.

Kwa mamlaka aliyopewa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo  Bw Michael Mwambenga ambaye kitaalumu ni Mwanasheria[Wakili] alitangaza matokeo hayo akianza nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu.

Amiri Mussa Amiri ambaye huyu ni Mjeda alipata kura 6. Hamis Hassan Kiwenja alipata kura 9 na Alfred Mdende alipata kura 38.

Hivyo kwa mamlaka aliyopewa wakili Mwambenga alimtangaza Mdende kuwa mshindi  nafasi hiyo.

Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti Wakili huyo alimtangaza Mh Selestin Mbilinyi kuwa Mshindi baada ya kuvuna Kura 37, huku mpinzani wake mkubwa Jofrey Mwatesa  aliambulia kura 17  na Godfrey Ng’itu akitoka Patupu baada ya kupata kura 0.

lkukumbukwe madadiliko  yaliyofanywa na Shirikisho la Mpiga wa Miguu Tanzania’TFF’kwenye mkutano mkuu uliofanyika mwaka jana jijini Mwanza,kwa kauli moja waliifanyia maboresho katiba ya uchaguzi.

Maboresho hayo ni kuanzia TFF Taifa, vyama vya Mikoa na Wilaya kwamba wajumbe watapiga kura kuchagua wagombea wa  nafasi tatu za Mwenyekiti, Mjumbe wa Mkutano Mkuu’Taifa’ na wajumbe wa kamati ya Utendaji.

Huku nafasi za Makamo Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Mweka hazina zikiteuliwa na mwenyekiti atakayeingia Madarakani.

Kwa upande wa  Wilaya nafasi zinazopigiwa kura ni mbili pekee, ya Mwenyekiti na ile ya Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Mkoa.

 Mara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa MDFA Mhe Mbilinyi ambaye pia ni diwani wa Kata ya Lukobe Manispsaa ya Morogoro kwa leseni ya CCM hapo hapo ukumbini alimteua Mgombea mwenzia Ng’itu aliyepata kura 0 kuwa Makamo mwenyekiti wa Chama hicho huku akiahidi kuteua watu wengine kuja nafasi ya katibu Mkuu na Mtunza fedha hivi karibuni.

Mara baada ya kuteuliwa kuwa Makamo Mwenyekiti  Ng’itu ambaye ni Mhe Hakimu wa Moja ya Mahakama za Mkoa wa Morogoro alimshukuru Mbilinyi kwa kumteua kwenye nafasi hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Pascal Kihanga alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema.

”Hongeni viongozi wote mliochaguliwa sasa mchape kazi kuhakikisha mpira wa  unakua kwenye wilaya yenu”alisema Kihanga ambaye pia ni diwani wa kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Mara baada ya kuzungumza Mhe Kihanga aliyechaguliwa Februari 8 kwenye uchaguzi mkuu wa MRFA uliomwingiza madarakani kukiongoza chama hicho kwa mara ya tatu mfurulizo  alitoa zawadi kwa viongozi wa Vilabu vyote 27 zilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo zawadi hizo zitaruka hewani hivi punde.

lkumbukwe katika uchaguzi huo mkuu wa chama cha soka mkoa wa Morogoro uliofanyika Februar 8 kwenye ukumbi huo huo wa Mbaraka Mwinshehe, Wilaya ya Morogoro na Wilaya ya Kilosa hazikushiriki kufuatia vyama vyao kutofanya uchaguzi kwa wakati hivyo kukosa sifa ya kushiriki uchaguzi huo mkuu wa MRFA.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wajumbe wa wilaya za Gairo, Mvomero,Malinyi, Ulanga na Kilombero wakishiriki uchaguzi huo, huku wajumbe wa Wilaya ya Kilosa na Morogoro wakiangalia uchanguzi huo kupitia  Mtandao Pendwa wa Shekidele.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...