Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, April 3, 2024

MTIBWA SUGAR YAMALIZA HASIRA ZAO KWA TAWI LAO MORO KIDS.

Vikosi cha Mtibwa Sugar kilichoanza jana
                                    Kikosi cha Moro Kids

Manahodha wa Mtibwa Oscar Massai kushoto] na Saddy  Mapuya wakipiga kura na waamuzi  kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.


                       Beki Oscar Massai akimiliki bori

Dakika ya 32 Mtibwa walifunga bao hili lakini Mshika kibendera namba moja Happiness Tamba alinyoosha kibendera akiashiria mfungaji alikuwa eneo la kutoea kabla ya kufunga.

Papatu papatu za gemu ya kirafiki kati ya Moro Kids na Mtibwa Sugar ulioigwa jana kwenye uwanja wa Jamhuri na Mtibwa kuibuka na ushindi wa bao 4 – 0.




Mshambuliaji hatari wa Mtibwa Sugar Charles llamfya, akiwajibika jana kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Moro Kids.







George Chota akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao hayo matatu kwa nyakati tofauti.






 


          Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Mtibwa Sugar yenye Maskani yake katikati ya Mashamba ya Miwa eneo la Manungu Kata ya Mtibwa Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, wamemaliza hasira zao za kufanya vibaya kwenye ligi kuu baada ya kuichapa timu ya Moro Kids bao 4-0.

Gemu hiyo ya kirafiki iliyokuwa na lengo la kuzianda timu hizo mbili za mkoa wa Morogoro zinazojiandaa na ligi mbali mbali umepigwa jana kwenye dimba la Uwanja wa Jamhuri.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika Vinaja wa Moro Kids waliwakaba koo kaka zao hao wa Mtibwa na kwenda mapunziko matokeo yakiwa sare ya 0-0. Kipindi cha Pili kocha wa Mtibwa Zubari Katwila’Kidimbwi’ aliona isiwe tabu aliwatoa wachezaji wengi wasio tumika kikosi cha kwanza na kuingiza majembe yake anayoyatumika kwenye kikosi cha kwanza.

 Mabadiliko hayo yalizaa matunda ambapo Mwamba Geoge Chota Mkazi wa Mawenzi Manispaa ya Morogoro aliyeingia kipindi cha Pili aliifungia timu yake mabao matuta peke yake.

Mwandishi wa habari hizi hakuweza kupata jina la mfungaji wa bao la 4 kwa sababu mchezo huo wa kirafiki haukuwa na line Up ‘Risti ya maji ya wachezaji’hivyo Mwandishi huyo alitumia uzowefu wake kwani baadhi ya wachezaji wa timu zote mbili anawafahamu.

 Ifahamike Moro Kids ambayo ni taasisi ya kukuza na kuibua Vipaji nchini iliyotoa wachezaji wengi kwenda Mtibwa na baadae timu kubwa kama vile Simba Yanga na Azam ndio mabigwa wa Ligi daraja la tatu Mkoa wa Morogoro msimu huu.

 Juzikati wamefanikiwa kuwa vinara kwenye ligi ya mabigwa wa Mikoa kituo cha Pwani hivyo kwa sasa kwapo kwenye maandalizi kabambe ya kujianza na hatua inayofuata.

Ligi hiyo ya Mabigwa wa Mikoa ilichezwa kwenye vituo 4  ndani ya Mikoa 4 ya Tanzania Bara na kila kituo kimetoa timu 2 za juu.

Akizungumza  jana mara baada ya gemu hiyo kutamatika, Meneja wa  Moro Kids Mussa Miraji alisema.

” Fainali za ligi ya mabigwa wa Mikoa zimepangwa kuchezwa  April 7 jijini Dodoma, timu Nane zitashiriki ligi hiyo na 4 za juu zitapanda ligi daraja la Pili”alisema Meneja huyo na kuongeza.

“Shekidele kwa timu yetu hii ulivyoiona kweli tutashindwa kushika nafasi moja wapo kati ya hizo 4?

Kupitia Mtandao wako Pendwa tunaomba wananchi wa Morogoro watupesapoti hata ya maombi ili tukaipandishe timu daraja”. alimalizia kusema Meneja huyo.

Timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo na Nane bora ni

Aagle Fc ya Dar es salaa.

Moro Kids ya Morogoro.

Arusha City ya Arusha.

Tukuyu Stars’Wanyambara’ ya Mbeya.na

Ganness  Fc, Dodoma.

Nyingine ni Leo Tena ya Kagera.Bukombe ya Geita na Hausangi ya Njombe.

Kila la Kheri Wana Mji Kasoro Bahari Moro Kids, ama kwa hakika kwa timu niliyoiona jana ninaasilimia 100 kwenye nafsi hizo 4 Moro Kids ananyakua moja.

                 


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...