Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, April 12, 2024

MORO KIDS YATINGA 4 BORA KIBABE, WAKIWAADHIBU WACHIMBA MADINI WA GEITA.

Msimamo wa ligi hiyo juzi kabla ya michezo ya Mwisho iliyopigwa jana kweny uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 Kikosi kabambe cha ‘Wana wa Pakaya’ Moro Kids. 


        Na Dunstan Shekidele, Morogoro.

TIMU Kabambe ya Moro Kids’ Wana wa Pakaya’ kutoka Mkoani Morogoro,jana wamefanikiwakutinga hatua ya 4 bora  baada ya kuwashushia kichapo cha Mbwa Mwizi timu ya Bukombe Combine ya Geita kwa kuichapa bao 5-2.

Kwa ushindi huo Mnono Vijana hao  wa Moro Kids’’Full Vipaji’ wamefanikiwa kushika nafasi ya pili ikinyakua alama 4 huku Mwenyeji Gunnes ya Dodoma ikiongoza kundi baada ya kukusanya alama 5.   .

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Moro Kids Josse Mkoko  timu hizo Gunnes na Moro Kids wanaungana na timu nyingine mbili za kundi B ambazo zitacheza nufu fainali zenyewe kwa zenyewe.

Timu mbili zitakazo shinda na kutinga fainali moja kwa moja zitapanda daraja la pili huku timu mbili zilizobaki kwa maana ya timu  zilizofungwa kwenye nusu fainali zenyewe zitaangukia kwenye Play off zikicheza na timu mbili za daraja la Pili zilizofanya vibaya kwenye ligi hiyo.

Mtandao huu unawapongeza  Moro Kids kwa kufika hatua hiyo huku Wana Morogoro tukizidi kumuomba Mungu aifanyia wepesi  kwenye mchezo huo wa Nusu fainali.   

Kama kawaida Mtandao huu utakupa taarifa zote za michuano hiyo ya Nusu fainali, cha msingi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

                              


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...