Mwandishi wa Mtandao akizungunza kwa nyakati tofauti na Maaskofu wa Makanisa ya KKKT Jacob Ole Mameo’Mwenye kofia Kubwa na Theresphori Mkude aliyeketi kwenye kiti. Askofu Maneno alihojiwa kuhusiana na Vibaka kuingia kwenye zizi lake na Ng’ombe na kumwibia Ng’ombe zaidi ya 100.
Kwa Upande wa Askofu Mkude alihojiwa kuhusiana na kanisa lake kupiga marufufu wahitimu wa Kipa Lmara na Ekaristi kutinga kanisani na mashindano ya mavazi ya Suti na mashera. Kanisa hilo la Roma lilifikia maamuzi hayo kufuatia madai ya mmoja wa wahitimu ya Kipa Lmara ambaye ni yatima kudai wakujinyonga baada ya kutinga kanisa na nguo za vilaka huku wenzie wakimeremeta na mashuti na mashera ya bei mbaya waliyonunuwa na wazazi wao. Askofu Mkude alisema katika kuondoa mashindano hayo ya mavazi kanisa wameamua wahitimu wote wavae sare za shule mashindano hayo ya mavazi wakayafanyie huko maukumbini na si kanisani.
Habari zote hizo zilisharuka kwenye Mtandao huu na Magazeti Pendwa ya Udaku ya Kampuni ya Global Publishers.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
SIKU za nyuma Mtandao huu uliwahiri kuripoti habari hii ya baadhi ya viongozi wa dini kulalamikiwa na wafiwa kwa kitendo chao cha kuondoka na sadaka zilizotolewa kwenye lbada ya kumuombea marehemu huku wakiwaacha wafiwa wakiwemo wajane, wagane, watoto na ndugu wa marehemu wakiambulia patupu.
Siku hizo za nyuma baada ya wananchi walitinga kwenye dawati la Mwandishi wa habari hizi na kuwalalamikia baadhi ya Viongozi hao wa dini kuondoka na sadala za Msibani.
Baada ya kupokea Malalamiko hayo Mwandishi wa habari hizi aliingia kazini na kufanya uchunguzi wa kina na kubaini makanisa mengi yanayojiita ya asili,Viongozi wao wa dini ndio wanaongozi kuondoka na sadaka hizo za Msiabani.
Makaninsa hayo ya asili ni Roman Katolini, KKKT, Anglikana, Morovian na Sabato.
Uchunguzi huo umebaini Makanisa mengi ya Kilokole likiwemo kanisa la Tanzania Assemblies Of God’TAG’ yenyewe hayana tabia ya kuchukua sadaka za Msibani.
lbada inapotamatika Mchungaji huwakabidhi sadaka hiyo wafiwa na yeye kuondoka mikono mitupu kwa sababau yeye ni mchungaji anayechunga Kondoo wake bure.
Mjadara huo uliibuka tena hivi karibuni ambapo kuna muumini mmoja wa kanisa la TAG linalojulikana kwa jina la Bethel Revival Temple’B.R.T’ lililopo Mwembesongo Mkoani hapa,alifariki dunia jijini Dar es salaam na mwili wake kuletwa nyumbani kwao Kota za Paju zilizopo Mji Mpya Mkoani hapa.
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye marehemu ni jirani yake alishiriki msibani huo mwanzo mwisho.
Ifahamike Mwandishi wa Mtandao huu toka anaanza darasa la kwanza shule ya Msingi Kaloleni Manispaa ya Morogoro alikuwa akiishi hapo ambapo mpaka leo wazazi wake bado wanaishi kwenye kota hizo zinazomilikiwa na Mtanzania mwenye asili ya Asia’Muhindi’.
Mara baada ya Mchungaji wa kanisa hilo la Bethel kumaliza mahubiri yake yaliyogusa watu wengi aliamuru mwili wa marehemu ufunguliwe kwa ajiri ya kutoa heshima ya mwisho’Kuaga’sambamba na kutoa Sadaka.
Umati Mkubwa wawatu uliofurika msibani hapo walipita mbele ya jeneza lililobeba Mwili wa marehemu sambamba na kutoa sadaka kwenye kikapu kiliochowekwa mbele ya jeneza. Kabla ya kufunga lbada hiyo na kuruhusu mwili wa marehemu kuingizwa kwenye gari yatari kwa safari ya kwenda makaburi ya Kolla kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.
Mchungaji huyo alichukua kapu hilo lililojaa sadaka nyingi nyekundu nyekundu na kumkabidhi Mjane wa Marehemu huku akisema.
”Msiba haupigi hodi ni tofauti na harusi, watuwanaketi vikao zaidi ya miezi mitatu kuandaa sherehe hiyo.Kunamtu anapatwa na msiba ndani hana hata sentitano na aliyekufa ndio ‘nguzo ya familia’ anayemtegemewa kwa kila kitu.
Halafu lbada inafanyika hapa msibani Kiongozi wa dini unaondoka na sadaka zote Ukiwaacha wafiwa bila kitu, kwenye kanisa letu jambo hilo halipo mfiwa aje nikakabidhi hii sadaka iliyopatika hapa ”alisema Mchungaji huyo na kupokea zawadi ya makofi mengi kutoka kwa waombolezaji wakisifu kitendo hicho cha kiungwana.kilicho jaa faraja kwa wafiwa.
Tukiwa makaburini tunazika mjadala mkubwa ilikuw ani huo wa TGA Kumkabidhi Sadaka Mfiwa wengi wakilipongeza kanisa hilo la TAG.
Kwenye stori hiyo ya awari Mwandishi wa Mtandao huu alifunga safari hadi kanisa kuu la Mt Patrick Jimbo la Morogoro na Kuzungumza na Paroko wa kanisa hilo Fr Kwembe ambapo alipotakiwa kulitolea ufafanuzi jambo hilo alijibu.
”Shekidele habari zako za udaku unazileta hadi huku kanisani,[kicheko].
Ni kweli kanisa letu tunaondoka na sadaka za Msibani hii ni kwa mujibu wa lmani yetu.
lmani ya mkatoliki yoyote ni kwamba Sadaka zote za kwenye lbada ya kumuomba Mungu ni Mali ya Mungu na sio vinginevyo.
Watu wanachanganya Sadaka na Rambi rambi, Rambi rambini ni Mali ya Mfiwa na Sadaka ni Mali ya Mungu, ndio maana kwenye misiba yote kuna daftari la Pesa la Rambi rambi.
Mwenyezi Mungu kupitia kitabu chake kitakatifu cha Biblini imesema, wanadamu wananiibia Sadaka na Zaka ndio hii sasa Mfiwa kapewa rambi rambi mfiwa huyo huyo anataka tena na sadaka ya Mungu huko ni kumkosea Mungu”alimalizai kusema Paroko huyo.
No comments:
Post a Comment