Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 4, 2024

VIMEUMANA. MILION 2 ZA NDONDO CUP ZAPELETA VITA TAIFA LA WATU WEUSI ’BLACK PEOPLE’

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akimkabidhi Kombe na Pesa Cash Milion 2 Nahodha wa Black People lbra Mkaa.

 Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Shehe Thiney Jaffar akiongoza lbada ya kuwarehemu wachezaji na wadao wa soka waliotangulia mbele za haki


             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

YAMETIMIA. Baada ya timu ya Black People Taifa la Watu Weusi’’ kutoka Pande za Mji Mpya Mkoani hapa, kutwaa ubingwa wa Michuano ya Ndondo Cup, na kukabidhiwa zawadi ya kombe na Pesa ‘Cash’ Milioni 2.

 lnadai zawadi hiyo ya Pesa imepelekea wanachama na wapenzi wa timu hiyo kutwangana makonde wakigombea pesa hizo. Taarifa za awari kutyoka kwenye vyanzo vya kuaminika zinadai baadhi ya wanachama wa timu hiyo walipinga kitendo cha Viongozi wao kutumia sehemu ya pesa kusoma dua ya kuwarehemu wachezaji na wadau wa soka waliotangulia mbele za haki.

lmeelezwa baada ya kutwangana makonde ya maana ugomvi ulipotamatika timu hiyo iligawanyika vipande viwili.

Wale wanaopingana na viongozi wa Black People kutumia pesa kuwarehemu marehemu wamejiondoa kwenye timu hiyo na kuanzisha timu yao inayojulikana kwa jina na Black Tiger. Baada ya kupokea taarifa hizo nzito Mwandishi wa Mtandao huu muda huu anatinga kwenye Maskan  ya timu hiyo kuzungumza na wahusika wa pande zote mbili kujua ukweli halisi wa taarifa hii.

  kwa habari kamili na picha endelea kuwa jirani na Mtandao Pendwa wa Shekidele muda wote.           

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...