Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, March 6, 2024

GEMU YA SIMBA NA PRINSONS BEKI KISIKI WA SIMBA AUMIA.




              Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 ‘Pira Gwaride’beki wa kutumainiwa na timu ya Taifa ya DR Congo anayecheza soka la kulipwa  klabu ya  Simba  Ennock lnonga,jioni ya leo ameumia na kulazimika kutoka uwanjani kwa kubebwa na wenzake.

lnoga aliyeng’ara kwenye michuano ya Afcon iliyotamatika hivi karibuni nchini lvory Coast akiitumikia timu yake ya taifa aliumia kwenye mchezo wa Ligi kuu kati ya timu yake dhidi ya Maafande wa Tanzania Prinson’Wazee wa Pira Gwaride’.

Mwandishi wa Mtandao huu aliyeketi nyuma ya gori la Simba akikusanya matukio mbali mbali alishuhudia lnonga akigaragara chini wakati Prisons wakifunga bao la Pili lililofungwa na Samson Mbangula na kushangilia kwa Style yao ya Kuku Kishingo’ kama wanavyoonekana Pichani.

Inonga alishindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Bakari Hussein. Gemu hiyo iliyotamatika kwa Mnyama Simba kupokea kichapo cha bao 2-1 dhidi wa Wajela jeha hao kutoka jijini Mbeya.

 Mwandishi wa habari hizi alitinga kwenye bechi la Simba kujua hali ya lnonga  alipofika alishuhudia lnonga akishindwa kutembea lkamradhimu kubebwa na wenzake kuingizwa kwenye vyumba vya Uwanjawa Jamhuri.

 Hali hiyo ilizua taharuki kwa baadhi ya mashabiki wa Simba ambao waliamua kushuka jukwaani na kumpa Pole  kama wanavyoonekana pichani.

Kwa sasa mashabiki wa Simba wanasubiri  ripoti ya madaktari wa Simba juu ya maendeleo ya mchezaji wao huyo kipenzi.  

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye mchezo huo ambayo yataruka hewani muda si mrefu

 


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...