Mithari 17.9-15.
“Afunikaye kosa hutafuta kupendwa,bali yeye akashifuye neno hutenga rafiki.
Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu,kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.
Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.
Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake kuliko na Mtumbavu katika upumbavu wake.
Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,mabaya hayataondoka nyumbani kwake.
Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji,basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki .hao wote wawili ni chukizo kwa Bwana.”
Hili ndilo neno letu leo jumapili ya March 17. UCHAMBUZI WA NENO.
Neno hili la Mungu limejitoshereza hivyo halihitaji uchambuzi mwingi.
Lakini sitawaacha hivi hivi nitalichambua kidogo neno hilo kwale lengo lile lile na kuwakumbusha na kuikumbusha pia nafsi yangu.
Sehemu kubwa ya ujumbe huo mzito wa Mwenyezi Mungu umelenga na kukemea kwenye maeneo matatu ya Ugomvi, Masimango na Chuki baina na mtu na mtu.
Hivyo mtu mwenye akili timamu,siku zote anaikimbia shari lakini mpumbavu siku zote anaitafuta na kuifuata shari. Mwenye masikio naalisikie neno hilo la Mungu asiye na masikio[…..]
No comments:
Post a Comment