Mwenyekiti Kiuno akihojiwa na Mtandao huu.
.
Katibu wa CCM Kata ya Mji Mpta Bi, Merry Kunambi akihojiwa na Mwandishi wa Mtandao huu Ofisni kwake
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, Kassim Ramadhan Lukinga’Maarufu ‘Kiuno’ anaongoza Mtaa huo kwa miaka 30 mfurulizo toka uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi ulipoingia nchini Mwaka 1994, haja wahi kushindwa kwenye kura za Maoni za chama chake cha CCM wala sandula la Kura la Uchaguzi wa Vyama Vingi hadi mwaka huu wa 2024.
Hata hivyo habari zilizopatikana ndani ya Mtaa huo zinadai katika chaguzi nyingi za kura za maoni ndani ya chama chake na zile za vyama vingi Mwenyekiti huyo anagombea peke yake akiogombwa na wapinzania wake kwa lmani za kishirikina.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa habari hizi alitinga kwenye Kata hiyo kwa lengo la kupata ukweli wa jambo hilo kwa kuzungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinzu’CCM’ Kata ya Mji Mpya,Wananchi na Mwenyekiti huyo.
WANANCHI HAWA HAPA.
“Ni kweli mwenyekiti wetu Kiuno anatuongoza kwa miaka 30 mfururizo toka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 94 hajawahi kushindwa Mpala leo”alisema Mussa Ng’anga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mji Mpya.
Alipoulizwa nini siri ya mafanikio ya kiongozi wao huo Ng’amba alisema.
“Siri ya mafanikio ni mchapa kazi mzuri anayejari shida za wananchi ambapo kwenye Misiba hakosi, kwenye sherehe tunaye hivi ninavyoongea na wewe toka hospital ya Kata ifunguliwe kajitolea kila kupanga mafairi ili wananchi wasikae foreni muda mrefu kuyatafuta”alisema Ng’amba na kuongeza.
Ni kweli kwenye mtaa huu chaguzi nyingi anakosa mpinza watu wanaogopa kuja kupambana naye kwa imani za kishirikina hilo kweli lnasema sana nyakati za uchaguzi.
Mitaa mingine hapa Mji Mpya toka mchakato wa kura za maoni ndani ya chama mpaka kwenye uchaguzi wagombea wanajitokeza wengi lakini kwenye mtaa huu kila mtu anaogopa kuchukua fomu kupambana na Kiuno Mwisho wa siku kwewnye chumba cha kupigia kura anakuwa peke wake anapita bila jasho”alimalizia kusema Ng’amba.
Kwa upande wake Mzee Omar Mabaranga ambaye kitaaluma ni Mganga wa Jadi na Tiba asili anayefanya shughuri zake kwenye mtaa huo alipohojiwa alisema
”Sisi tunampenda mwenyekiti wetu ataongoza mtaa huu mpaka achoke mwenyewe si jambo rahisi kuongoza mtaa kwa miaka 30 mfururizo hii inaweza kuwa histori kwenye Mtaa wetu na mkoa mzima wa Morogoro.
Wapinzani wake kisiasa wanadai anakimbiwa kwa ushirikina sio kweli wanamkimbia kwa sababu wanajua ni mchapa kazi, mitaa mingapi hapa Morogoro inawaganga mbona wanashindwa kwenye chaguzi mbali mbali”alisema Mzee huyo.
HUYU HAPA MWENYEKITI MWENYEWE.
Mwandishi wa habari hizi alitinga nyumbani kwa mwenyekiti huyo na kuzungumza naye ambapo alithibitisha kuongoza mtaa huu kwa miaka 30 mfurulizo.
” Ni kweli Shekidele naongoza Mtaa huu wa Makaburi A toka nicheguliwe kwa mara ya kwanza 1994 sijawahi kushindwa mpaka leo 2024.”alisema Mwenyekiti huyo.
Alipoulizwa nini sifi ya mafanikio hayo ajiribu
”Ni sera nzuri za Chama changu cha CCM zinazokubarika na wananchi wa mtaa huu pili, mimi kujitoa kwenye Raha na Shida za wananchi wangu wa mtaa huu”alisema mwenyekiti huyo.
Alipotakiwa kuelezea kwa nini mara nyingi anagombea peke yake bila mpinzani kuanza kura za maoni ndani ya chama chake cha CCM na uchaguzi wa Vyama Vingi alijibu”
Kama nilivyokueleza awari silaha kubwa ni mimi kukubarika na wananchi wangu, wapinzania wanaukimbia mtaa huu wakijua hawawezi kunishinda”.
Kuhusu Madai yakumbiwa na wapinzani wake kwa madai ya kumuogopa kwa imani za kishirikina alijibu.
”Habari hizo zipo sana hapa mtaani lakini hazininyimi usingizini wala kunikatisha tamaa ya kuwatumikia wananchi wangu, hizo ni hoja dhaifu za wapinzani wangu”alisema Mwenyekiti huyo kwa kujiamini.
Alipoulizwa anampango wa kugombea tena kwenye uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika November mwaka huu?alijibu
“Ndio nasubri kipenga kianze kikachukue fom ”.
Alipoulizwa swali la mwisho kwamba kwa mafanikio hayo kwa nini asigombee udiwani ndani ya kata hiyo alijibu.
“ Wazo la kugombea udiwani nilikuwa nao uchaguzi uliopita nilikwenda kugombea kijiji kwetu Konga Kata ya Kauzeni Kule Mzinga Jeshini Manispaa ya Morogoro lakini kwa bahati mbaya kura hazikutosha.
Kwa hapa kata ya Mji Mpya huyu Diwani wetu Mh Emmy Kiula Maarufu Mama Kiula anafanya kazi nzuri acha endelee kutuongoza na mimi nikiendelea na nafasi yangu ya uwenyekiti tukimsaidi Majukumu ya kutatua kero za wananchi wa kata yetu ”alimalizia kusema Mwenyekiti huyo.
Baada ya kuzungumza na Mwenyekiti huyo Mwandishi wa Mtandao huu alitinga Ofisi ya CCM Kata y Mji Mpya na kufanikiwa kuzungumza na Katibu wa CCM Kata Bi. Merry Kunambi ambapo alipohojiwa alithibitisha Kada wake huyo Kuking’arisha chama hicho kwa kuongoza mtaa huo kwa miaka 30 mfurulizo.
“ Ni kweli Mwanachama wangu Kiuno anakiheshimisha chama chetu kwa kuongoza mtaa wa Makaburi A kwa miaka 30 mfurulizo, hapa tulipo CCM Kata tuko Mtaa wa Makaburi B yeye anaongoza mtaa huo wa Makaburi A.
Kwa mafanikio hayo sisi kama chama Kata ya Mji Mpya atakapokuja kuchukua fomu ya kugombea tena kwenye uchaguzi wa Mwaka huu tutamkabidhi Tuzo ya heshima.
kwenye sherehe hiyo ya kumtunza tutakualika shekidele ujekuchukua habari ukairushe kwenye mtandao wako na shughuri hiyo tumeipanga kuifanya siku Mwenyekiti huyo atakapokuja kuchukua fomu ya kugombe tena nafasi hiyo ”alisema Katibu huyo. Alipoulizwa kuhusu taarifa za kada wake huyo kudaiw akukimbiwa na wapinzani wake toka ndani ya kura za maoni za CCM hadi kwenye uchaguzi wa wa vyama vingi kati huyo huyo alijibu.
” Sisi chama na serikali hatuamini mambo hayo ya kishirikina tunaamini kwenye uwajibikaji hivyo sisi kama chama tunaamini Kassimu Ramadhani Lukinga Maaruifu ‘Kiuno’ uajibikaji wake unapelekea kukubarika na wananchi wa Mtaa wanaoendelea kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 30 sasa
” Kwa mara ya kwanza mfumo wa Vyama Vingi uliingia nchini mwaka 1992 na uchaguzi wa kwanza vya serikali ya Mtaa ulioshirikisha vyama vingi ulifanyika mwaka 1994 na uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1995
Wahusika wote walihojiwa na Mtandao huu huku wakirekodiwa ambapo Clip video hizo zitaruka hewani hivi punde.
No comments:
Post a Comment