Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, March 13, 2024

SIMBA MORO YAPASUKA VIPANDE 2 YADAIWA NDIO SABABU YA TIMU KUKIMBIA UWANJA WA JAMHURI.

Tawi Jipya ya Shujaa lenye namba ya usajiri
          Kadi ya uwanchama ya Mzee Kiwamba


Mwenyekiti Said Mkweinda kulia akimpokea aliyekuwa mgombea  nafasi ya uwenyekiti wa klabu ya Simba Wakali Moses Kaluwa

Tawi la Shujaa la Sokoni ambapo Mzee Dalali[mwenye kanzu na koti na aliyekuwa mgombea nafasi ya uwenyekiti Wakili Moses Kaluwa[mwenye jezi ya Simba ya Bluu January 18-2023 walitinga kwenye tawi hilo kuomba kura kwa wanachama.

Tawi kuu wa Shujaa ngome kuu lililopo Mji Mpya Sokoni
lfahmike hilo tawi la Shujaa Sokoni sio tawi la kitoto kitoto kila jezi mya za Simba zinaotoka lazima ziletwe kwenye tawi hilo na wanachma wananunua jezi hizo OG kuitia uongozi wa tawi hilo
....Mgombea na wafuasi wake wakiomba dua kabla ya kuomba kura kwa wanachama wa Simba tawi la Shujaa sokonii

                                                ....Msafara huo ukirejea Dar


               Na Dustan Shekidele,Morogoro.

WANACHAMA wa timu ya Simba Mkoa wa Morogoro kupitia tawi kuu la Shujaa wameingia  kwenye mgogoro mzito uliopelekea  kugawanyika makundi mawili kundi la Wazee na kundi la Vijana.

Kama kawaida baada ya kupokea taarifa hizo nzito Mwandishi wa habari hizi aliingia mzigoni kwa lengo kuchimba na kujua mbichi na mbivu  [Black and White] za mgogogo huo.

 Chaajabu Mwanahabari huyo alipofika mitaa ya Mji Mpya lilipo tawi hilo,  alishuhudia matawi yote mawili yakiwa na namba moja ya usajiri ya klabu resens no 0142, yakichora matawi yao jina moja la Shujaa kila upande ukidai ndio wenye haki ya kumiliki tawi hilo na kuponda uongozi wa tawi lingine.

llikupata  ubuyu mzuri uliokole rangi Paparazi wa Mtandao huu alianza kutinga tawi jipya la Shujaa,lililopo kwenye mjego wa Familia ya Mzee Mlanzi, jirani na Stend ya daladala Kaloleni Mji Mya ikitazamana na Kituo cha Polisi Kata ya Mji Mpya na Zahanati ya Kata ya Mji Mya na kushuhudia mafundi wakiendelea kupaka rangi tawi hilo jipya.   

  HAWA HAPA VIONGOZI WA TAWI HILO.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Muda wa tawi hilo linaloundwa na wazee wengi wanaodai  ndio waasisi wa timu ya Shujaa ambayo ni marafiki wa Simba, Sudi Mrisho Kiwamba alipohojiwa alifunguka haya.

”Ni kweli sisi tumejiondoa kwenye tawi lile la Shujaa pale sokoni mimi kama mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya tawi  wameniandikia barua ya kunifukuza,ifahamike muda wao wa uongozi umekwisha na hawataki kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi, pia pale kwenye jengo la CCM wanadai kodi kubwa kama milioni na laki Nane muda wowote wanafukuzwa”alisema Mzee Kiwamba ambaye kitaaluma ni Mwanasheria.

Mzee Kiwamba aliendelea kumpa madini Mwandishi wa habari hizi akisema “ Shujaa sio tawi la Simba ni timu kamili ya mpira tuliyoianzisha Mwaka 1967 pale nyumbani kwangu namba yetu ya usajiri wa timu hio hao kwenye bago, sisi sio tawi la Simba ni marafiki wa Simba katika Tanzania simba inamarafiki 4 ambao ni Shujaa,ya Morogoro, Kikwajuni Zanzibar, Nguvu Moja, Lindi na Nyamaome ya Mwanza.

Nyamaome na Nguvu Moja zimeshakufa. wale wa pale sokoni sio Shujaa ni kikundi cha wanachama wa Simba, hatuwatambui kwenye timu yetu kwa sababu hatimiliki zote za shujaa tunazo sisi na mimi  ndio Mdhamin wa Mali za Klabu yetu ya Shujaa’alimalizia kusema Mzee Kiwamba huku akionyesha uthibitisho  wa kadi yake ya shujaa na Simba.

 

 

 Baada ya kutoka hapo Mwandishi wa Mtandao huu alitinga  mtaa wa Pili lilipo  tawi  la awari la Shujaa ambalo liko ndani ya Ofisi za CCM Kata ya Mji Mpya Jirani kabisa na Soko Kuu la Kata ya Mji Mpya na kufanikiwa kuzungumza na Mwenyekiti wa tawi hilo Bw Said Mkwinda na mahojiano  yalikuwa hivi.

Mwandishi.  Pole na swaumu ya kwanza Mwenyekiti.

Mkwinda. Asante leo ndio chungu cha kwanza na wakati unanipigia simu muda ule wa saa 7 nilikuwa Msikiti Mpya wa Mji Mpya, niambiye shekidele ingawa nimeshajua kilichokuleta. Mwandishi. [Kicheko]Kipi hicho kilichonileta Mwenyekiti?

Mkwinda. Hao wapinzani wetu wazee waliohasi Shujaa na kwenda pale kwa Mlanzi kuanzisha tawi lao.

 Mwandishi, Ok ni kweli hicho ndicho  kilichonileta nini shida sasa wa mpasuko huu ili hali awari mlikuwa wamoja?.

Mkwinda. Shida ni mambo mawili mosi Oroho wa madaraka wa wale wazee pili makundi ya uchaguzi mkuu wa Simba bado yanaendelea ingawa viongozi wetu waliagiza tuvunje makundi  tungane kuijenga  Simba yetu wao hawajavunja kundi lao la Uchaguzi.

Mwandishi. Naomba ufafanuzi kwenye mambo hayo mawili, Uroho wa madaraka vipi wakati  Mzee Kiwamba Mzee Mselemu, Mzee Kimvuli Mzee Mwambeta walikuwa Viongozi  wa hili tawi siku za nyuma nyie mlivyoingia madarakani baadhi yao mkawateua kwenye kamati mbali mbali za tawi, Pili kitu gani ulichokiona sasa ninachoashiria bado makundi ya uchaguzi mkuu wa simba yanaendelea kwenye tawi lile? Mkwinda. Kuhusu Uroho wa madaraka kila siku wazee wale wanapiga gelele za kutaka kufanyika  uchaguzi  kinyume na utaratibu tulishawatangazia wanachama  wote kwamba Mwezi wa 5 mwaka huu tutafanya uchahuzi  wanachama wametuelewa baadhi ya hao wazee wanapiga.

 Kuhusu makundi ya uchaguzi mkuu wa Simba  wazee wengi wa tawi letu walikuwa timu Moses Kaluwa na sikia hivi karibuni wamewasiliana na Mzee Dalali aliyekuwa akimsapoti Kaluwa nasikia kila siku wanawasiliana na Mzee Dalali huenda ndiye anayewapa nguvu ya kujiondoa na kuanzisha tawi lao.

Mwandishi. Kuna taarifa zinadai baadhi ya wazee mmewafukuza akiwemo Mzee Kiwamba aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi je ni kweli?

 Mkwinda. Hakuna mtu aliyefukuzwa iko hivi miaka yote tunapokaribia kwenye uchaguzi  tunavunja kamati zote ikiwemo kamati ya uchaguzi ni kweli Sud Kiwamba ni mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi  tumempa barua ya kumjulisha kwamba tumevunja kamati, hatukumpa barua ya kumfukuza tawini.

 Mwandishi. Wale wazee wanadai wanacheti chenye namba ya usajiri ya timu na tawi la Shujaa je kwa upande wenu vitu hivyo nnavyo?

Mkwinda. Chetu na namba walioandika pale kwenye tawi lao na sisi tunayo hiyo hiyo tulivyoshinda uchaguzi walitukabidhi wao wenyewe kama  walitupa cheti na namba feki ya usajiri basi hilo ni kosa la jinai kwa sababu tulisha uchaguzi ule kihalali walipaswa kutupa Docoment halali na si feki.

Mwandishi.  Uchunguzi wa awari nilioufanya kama Mwandishi wa habari nimebani kwamba kila mwaka namba ile ya usajiri inalipiwa Baraza la Michezo Tanzania’BMT’ na kwa Afisa Utamaduni pale Manispaa chini ya uongozi wako namba ile hamkuilipia kwa miaka kadhaa wenzenu wameenda kulipia wamepewa namba na  cheti nyinyi mmebaki na kile kisicholipiwa, pia  kodi ya pango hapa CCM nasiki mnadai miezi mingi nini kauli yako kwenye uchunguzi wangu huo.

Mkwinda. Sisi kudaiwa kodi sio dhambi, taasisi yoyote kudaiwa ni jambo la kawaida kweli hapa CCM tunadeni lakini sio million moja na laki Nane kama wanavyotangaza wahao wapinzani wetu.

hapa kodi kwa mwezi tunalipa laki moja na 70 tunadaiwa kama miezi 2 hivi laki tatu na arobaini[340000]na deni hilo tutalipa wakati wowote kuanza sasa. hao wanatangaza hivyo lengo lao CCM watufukuze waje kukaa wao hapa taarifa hizo tunazo.

Mwandishi.swali la mwisho kuna madai kwamba hali hiyo ya mgogoro wa tawi lenu ndio uliopelekea Uongozi wa Juu wa Simba kuwanyang’anya timu na kuirejesha Dar es salaam taarifa hizo zinaukweli wowote?

Mkwida. Sio kweli majuzi mwenyekiti Mangungu kanipigia simu akinipa maelekezo ya maandalizi ya mchezo wetu wa Singida hapa Morogoro katika kuthibitisha hilo hata timu yenye ya Singida Fountain Get ilishafika hapa Morogoro, ghafra Azam Tv wamedaI muonekana wa picha zao pale Jamhuri sio mzuri hivyo wameomba bodi ya ligi kufungia uwanja  hiyo ndio sababu ya timu kuondoka Morogoro.Mwandishi Mwenyekiti kwa ushirikiano wako. Mwenyekiti . Asanye na wewe kwa kuja kutuhoji uma wawatanzania ujue ukweli wa mgogoro huu

 

Awari  Simba kupitia Afisa habari wake Ahmed Ally ulitanga kuhamia mkoani hapa kucheza michezo yake ya Ligi kuu kufuatia Viwanja vya Mkapa na Uhuru  Vilivyopo Temeke Jijiji Dar es salaam Kufungwa kupisha ukarabati.

Uongozi wa tawi hilo la Shujaa uliipokea timu yao hiyo ambapo lichezo mchezo mmoja tu mkoani hapa dhidi ya Tanzania Prinson na Simba kupokea kichapo cha bao 2-1.

Baada ya kichapo hicho ziku kadhaa mbele taarifa kutoka bodi ya Ligi ilitoka na kudai kakao cha pamoja kati ya Simba,  Azam Media na Bodi ya Ligi waliketi na kukubari ombi la mwenye haki ya kurusha matangazo kwa maana Azam  aliyeomba bodi la ligi kufungia uwanja wa Jamhuri kufuatia uwanja huo kuwa na changamoto nyingi za urushaji matangazo hayo ya moja kwa moja.

BAADHI YA WADAU WAMEPINGA HOJA HIYO.

Baadhi ya wadau wa soka mkoani Morogoro waliohojiwa na Mtandao huu walihoji  bodi ya ligi kufungia uwanja wa Jamhuri.

“’Kwangu mimi hoja ya  bodi ya ligi kufungia uwanja wa Jamhuri naiona kama  ni dhaifu  nahisi kuna jambo ligine sio hilo, la kufungia uwanja  eti unachangamoto za kurusha matangazo ya Azam, Tumeangalia vizuri gemu ya Simba na Prisons hakuna changamoto yoyote tulioiona sasa kama Uwanja wa Jamhuri uliozungukwa na mabati na wapiga picha wa Azam wanakaa juu ya Paa za Mabati hayo wanapiga picha zao vizuri, je  uwanja wa Manungu ambao hauna mabati au viwanja kama hivyo mbona tunashuhudia picha nzuri za Azam Tv naona kama watu wa Morogoro tunaonewa kwenye hili “.alisema Joseph Banz   

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...