Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, March 9, 2024

MATUKIO GEMU YA SIMBA NA WAJELA JELA

MKONGO Man Fabrice Ngoma  akifumua shuli  kali katikati ya mabeki na kuifungia timu yake bao,  

........waamuzi hao walilikataa bao hilo kama unavyoonekana Ngoma akimlalamikia refa

VAR ya Mtandao wa Shekidele, imemulika na kubaini hili ni bao.


  

Mshambuliaji wa Simba Freddy Michael Koubalan aliyesajiriwa  juzikati kwenye usajiri wa dirisha dogo.aliwafanyia unyama mwingi

mabeki ya maafande wa Magereza  na kuchonga krosi iliyoungwanishwa wavumi na Kibu D.

Hata hivyo waamuzi walilikataa bao hilo





PISHA NJIA.

Mnyama Kibu Denis 'Kibu D' akiichambua beki ya Priinson kama Karanga. angalia picha zaidi hapo chini


HE  HE HE We Kimenya viti tena unammenya mwenzio kama ndizi?




Beki wa Prinsons Salumu Kimenya akimvisha kanzu beki wa Simba lsrael Mwenda.

MKONGOMAN INONGA.

Beki Kisiki wa Simba  Henock lnoga akiwajibika kwenye gemu dhidi wa Prisons.

 

Hata hivyo mwisho wa Simba Maafande hao wa Prisons walimumiza mchezaji huyo ambapo taarifa za Simba kupitia Afisa habari wao Ahmed Ally amedai


Inonga ameumia Mguu kwa sasa anatembea kwa msaada wa Magongo. Kwa mujibu wa Kiongozi  huyo  baada ya mchezo na Prisons , lnonga alirejeshwa Dar es salaam kwa matibabu zaidi

Hiki sio chama  Cha  Siasa. ni Mwamba wa Lusaka


Clatous Chama Fundi wa bori akikusanya kijiji cha Maafande wa Magereza

Kipa wa Prinsons Amos Yona aklinyaka Mpira huku akichungwa na mabeki  wake

Aisha Manula aliyelalamikiw ana mashabiki wa Simba kwenye gemu hiyo kwa madai ya kucheza chini ya Kiwango akiondoa moja nya hatar kwenye gori lake Na Dustan Shekidele,Morogoro.
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...