Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, March 8, 2024

ATO Z BLACK PEOPLE KUTWANGANA MAKONDE KISHA DUA YA KUWAREHEMU WALIOIAGA DUNIA.

Polisi wenye mbwa wakiaamulia ugomvi ullioibuka kati ya mashabiki wa Black People na wenzao wa Damu Chafu kwenye mchezo wa fainali ya Ndondo Cup.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Aziz Aboodkulia] akimkabidhi Kombe na Pesa taslmu million 2 Nahadha wa Black People lbra Mkaa..
Mashabiki wa Black wakishangilia na kombe lao.

  

 

  Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Thiney Jaffar akiwaongoza waumini na wadau wasoka kwenye lbada ya kuwarehemu wachezaji na wadau wa soka waliofariki dunia.


Seif Kijiji  akipokea dua wakati ya lbada ya kuwarehemu marehemu,

 Mwamini Mnyepe Makiliki wa Nyuki akihojiwa na Mtandao huu. 


        Na Dunstan Shekidele Morogoro.

 UNDANI madai ya baadhi ya mashabiki wa timu ya Black People kutwangana makonde kisa kikidaiwa kupinga wazo la  kutumilia milioni 2 walizonyakua kwenye michuano ya Ndondo Cup na kuzitumia kusoma dua ya kuwarehemu wachezaji na wadau wa soka  waliofariki dunia.

Baada ya kupokea taarifa hizo nzito Mwandishi wa Mtandao huu juzi na jana alitia timu kwenye maskani ya timu hyo Maeneo ya Uwanja wa Shujaa kwenye Pub mmoja iliyopo jirani na kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya  na kufanikiwa kupata ‘Black and White’ ya habari hiyo. 

HAWA HAPA MASHABIKI WA TIMU HIYO.” Shekidele wewe mwenyewe ni shahidi unatuona kila siku pale Uwanja wa Saba saba tukijichetua na kujitoa fahamu tukisapoti chama letu la Black People.

Mara nyingine tunapigana na mashabiki wa timu pinzania tukiitetea Black mara nyingine kunapigwa na Mapolisi wenye Mbwa kwa sababu ya kuisapoti Black.

 Leo timu imefanikiwa kupata milioni 2 Viogozi wamegawana pesa zilizobaki ‘wamezuga’wamenunua mchezo kidogo na nyama wamesoma dua ya kuwarehemnu marehemu huku sisi wahuni tunaoipambania timu,  hatukupewa hata sent tano  wanatuambia pesa zote wametumia kusoma dua.

 Wangetupa  hata laki tatu tununue pombe tunywe hapa kwenye Pub yetu tungelizika ”alisema Suma na kuongeza.

Mjomba Shekidele angalia miguu angalia mbavuni haya ni makonde tuliopigana humu ndani kisha ni hizo milioni 2”alimalizia kusema Suma kwa niaba ya wenzake.

Alipoulizwa mbona  kwenye lbada hiyo ya kuwarehemu marehemu alishuhudiwa na Mtandao huu akigonga pilau iweje leo apinge wazo hilo zuri la viongozi wake?

 Alijibu “Ni kweli mimi na wenzangu tulikuwepo pale kwenye lbada lengo la kuwepo pale ni kuchunguza kama chakula kilichonunuliwa kinalingana na Milioni 2 tumepata jibu chakula kile hakizidi hata laki 5 pesa zingine viongozi wamekula”

Alipoulizwa yeye na kundi lake wanampango gani sasa kuhusiana na tukio hilo?

Alijubu” Sisi tumejitoa Black People tumeanzisha timu yetu inaitwa Black Tiger na tunasikia  Radio Planet wanajiandaa kuanzisha Michuano Mikubwa ya Ndondo Cup kupitia mtandao wako wenye wasomaji wengi tunamuomba mwandaji  huyo atupange na Black People tuwanyooshe mapema”alimalizia kusema Suma huku akiwa na majeraha kibao mwilini.

      MALIKIWA WA NYUKI HUYU HAPA.

Baada ya kutoka kwenye Pub hiyo Mwandishi wa habari hizi alitinga Mtaa wa Holowera Kata ya Mji Mpya nyumbani kwa Mwamini Mnyepe kiongozi wa timu hiyo Mwenye cheo cha ‘Malikia wa Nyuki Black Peole Fans’

Ni kweli Shekidele watu wametwagana sana pale maskani kisa ni ile million 2 ya Ndondo Cup kweli wale wahuni wanafanya kazi kubwa sana timu yetu inapocheza mara nyingine hata ukiwatuma kwenda Makaburini  wana kwenda sasa kwenye ile million 2 viongozi wenzangu wangewapa hata laki 2 wanunue pombe pale Pub”:alisema Mwamin ambaye Marehemu baba yake Mzee Mnyepe alikuwa beki kisiki wa timu ya Nyota Afrika yenye undugu na timu ya Yanga ya Dar. lfahamike miaka ya nyuma mkoa wa Morogoro ulikuwa na timu mbili kubwa za Nyota na Shujaa ,

Nyota ni ndugu wa Yanga na Shujaa ni ndugu wa Simba hadi sasa tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro lililopo Mji Mpya linajulikana kwa jina la Shujaa. Mwamini Mnyepe ni Mwanachama wa Simba kupitia hawi hilo la Shujaa alihasi timu ya Marehmu baba yake.

       MAJIBU YA VIONGOZI HAYA HAYA.

Baada ya kutoka kwa Malikia wa Nyuki Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Rais wa Black People Seif Kijiji alipolizwa juu ya habari hiyo alijiri kwa ufupi.

 “Hakuna kitu kama hicho sisi tuko pamoja na tutaendelea kuwa wamoja siku zote hao wahuni wachache wanaoleta choko choko kwenye timu yetu na wajua hawatusumbui”. Alisema  Seif Kijiji  

Hii ni kama mara ya pili Black People  wanaingia kwenye mgogoro na mashabiki baada ya kutokea kwa mgogoro huo, baadhi ya wachezaji na mashabiki walijiondoa na kwenda kuanzisha timu yao.

   Mashabiki hao ni Kubwa Membe, Rashid Maarufu Chid Boy kwa upande wa wachezaji waliojiondoa ni Said Kaera, Jabu na beki anayekiiga Msibwa Sugar Nasri KomboMaarufu Nassri Scobb, .

Baada ya kujiondoa walianzisha timu yao walioipa jina la Rizibon Fc.huku aliyekuwa kocha wa timu hiyo ya Black People Yahaya Mkesa yeye akitimkia Moro Kids akifundisha timu ya umri chini ya miaka 17 ‘Under 17’

Kama hiyo haitoshi baada ya muda Rizibon wametofautiana tena na kumeguka vipande viwili Kapetera na wenzake wameenda   kuanzishia timu yao ya Washashi Fc ambayo kwenye michuano hiyo ya Ndondo Cup ilifungwa bao 1-0 na Black People na kutupwa nje ya michuano hiyo huku Mwamba Black People akitinga fainali.

Wakati hayo yakitokea kwa Rizibon,  Taifa la watu weusi Black People wao wamesimama lmara kama chuma cha Mjerumani  wakiendelea kutwaa makombe na kuvuna Pesa za Ndondo Cup.  

                             

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...