Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, March 29, 2024

TUSIIFANYE MIOYO YETU KLUWA MIGUMU

LEO ni ljumaa kuu Mwana wa Mungu Yesu Kristo anasulubiwa na wayahudi mida ya saa 9 Alasiri na kutundikwa msalamani huku akivishwa taji la Miba.

 Kwa ukuu wake Yesu Kristo au Nabii lssa kama anavyojulikana na waru wa dini nyingine alikuwa na uwezo wa kukiupeka kikombe hicho cha mateso, lakini kwa upendo wake kwa wanadamu amekubari kutoa mwili wake sadaka kwa lengo la kutukomboa sisi wanadamu tunaoishi chini ya jua.

Hata hivyo kwa Ukuu wa Mwenyezi Mungu baada ya siku tatu alimfufua mwanae huyo aliyezikwa kwenye kaburi lililosindikwa na jiwe kubwa.



 

Watu wengi hakukuamini ufufuo huo wa Yesu akiwemo Thomaso ambaye licha ya kupata habari hizo za yesu kufufuka alibisha akisema  hawezi kuziamini mpaka  amuone Live Yesu. Kwa ukuu wake Yesu alimtokea Thomaso na kumthibitishia kwamba  kwakumuoryesha makovu yaliyokuwa sehemu mbali mbali za mwili.

 Kwa ushahidi huo ndipo Thomaso alipoamini na kuendeleza kusambaza habari hizo vyema za ufufuo wa Yesu.

Hivyo  wewe unayesoma habari hizi nakusihi na kuihusia pia nafisi yangu kwamba tubakidirike kitabia tumpokee yesu[Nabii lssa] anayegonga hodi kwenye mioyo yetu tumfungilie aingie tusiifanye mioyo yetu kuwa migumu.

Tuache kiburi cha uhai tulionao na afya njema, vitabu vya dini kuitia Mandiko matakatifu yanatuambia kwamba kila nafsi itaonja umauti.

Mwenye masikio na sikie asiye na masikio[;;;;]

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...