Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, February 24, 2024

MICHUANO YA NDONDO CUP. SHEHE MKUU ONGOZA IBADA YA KUWAOMBEA MAREHEMU

Nahodha wa Black People lbra Mkaa akikabidhiwa kombe na Milioni mbili na  Mbunge Aziz Abood.       

 


 

Nahodha lbra Mkaa akiwa jikoni jana kitengo cha chakula akisimamia ugawaji wa chakula kwenye lbada hiyo.
Shehe Mkuu wa Wilaya akisoma majina ya marehemu kwenye ibada hiyo.


 Rais wa  Black People Seif Kijiji akipokea dua wakati shehe Jaffar akitaja maji ya marehemu hao.


 

.

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 HII IMEKAA POA SANA.

Baada ya timu ya Black People’Taifa la watu weusi kutoka Mji Mpya,kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya Ndondo Cup na kukabidhiwa kombe na Pesa taslimu million 2.

Uongozi wa timu hiyo inayoongozwa na Rais wao Seif Kijiji jana ljumaa mara baada ya lbada kuu ya ljumaa kutamatika kwenye misikiti mbali mbali,wametumia kiasi cha Pesa hizo kufanya lbada ya kuwarehemu wachezaji na wadau wa soka waliotangulia mbele za haki.

lbada hiyo iliyofanyika Uwanja wa Shujaa Mji Mpya iliongozwa na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Thiney Jaffar, aliyesoma majina ya ndugu zetu hao waliotangulia mbele za haki.

Juzi Jioni Rais wa Black People Seif Kijiji alimtwangia simu Mwandishi wa Mtandao huu  akimpamwalika rasmi wa kuhudhuria lbada hiyo ambayo baada ya kutamatika watu walifinya chakula ya Mtume.

 Akihojiwa na Mwandishi wa habari Seif Kijiji alisema, baada ya kupata mafanikio hayo ya kutwaa kombe na kukabidhiwa Milioni 2 wameamua kurudia shukrani kwa mwenyezi Mungu.” Shekidele wewe shahidi mwenyezi Mungu katusimamia tumechukua zwadi nyingi za Ndondo Cup kwenye mkoa huu wa Morogoro Kilosa, Mvomero Gairo Manispaa kote huko tumechukua Ndondo sasa hii Pesa hii tuliyoipata juzi kama uongozi tumeshauriana tuitumia kufanya lbada ya kuwaombea wacheza na wadau wote wa soka wa Mkoani Morogoro waliotangulia mbele za haki”alisema Seif

Kwa kitendo hicho watu wengi wamewapongeza viongozi wa Black People kwa kufanya jambo hilo Jema mbele za wanadamu na mbele za Mwenyezi Mungu.

Miongoni mwa watu waliotoa pongezi hizo ni pamoja na Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro Hamis Suffi na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa A lssa Kitukwa Maarufu lssa Chabala ambaye pia ni kipa wa zamani wa timu ya Shooting Stars ya Mji Mpya.

 Ifahamike shughuri hiyo ilifanyika kwenye Mtaa huo wa Fumilwa. 

Michuano hiyo ya Ndondo Cup iliyoandaliwa na Mdau mmoja wa soka mkoani Morogoro ilishirikisha timu 8, zilizocheza ligi ya mtoani[Ngumi Jiwe] ukifungwa Out.

Mwisho wa Siku Black Peole kutoka Kata ya Mji Mpya na timu ya Damu Chafu kutoka Kata ya Mwembesongo zilifanikiwa kutinga fainali iliyopigwa February 16  uwanja wa  CCM Saba Saba Manispaa ya Morogoro.

Katika mchezo huo ambao mgeni rasm alikuwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Aziz Abood, Black People’Taifa la Watu weusi’ Waliwasafisha watu wenye damu chafu kwa kuwafunga Pelnaty 7-6 baada ya timu hizo kutoka sare dakika 90 za awari.

Mbunge Abood ambaye anatajwa kuwa tajiri namba moja mkoani Morogoro akimiliki Mabasi, Malori,Viwanda, Vyombo vya habari,na Vituo vya Mafuta’Shell’ alimkabidhi kombe na pesa taslimu milioni Mbili Nahodha wa Black People lbra Mkaa huku Damu chafu wakiambulia milioni Moja baada ya kushika nafasi ya pili.

Mastaa kibao wa ligi kuu kutoka timu za Mashujaa ya Kigoma, lhefu ya Mbeya, Mlandege ya Zanzibar,Mbeya City na Mtibwa sugar ya Morogoro walisheheni kwenye timu hizo mbili.

Picha za mastaa hao na matukio mbali mbali za fainali hiyo,sambamba na matukio ya lbada hiyo kuwarehemu marehemu wetu yataruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na mtandao huu muda wote.

lkumbukwe Vijana wa Damu Chafu ambao hivi karibuni nao walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya Kelvin John Ndondo Cup iliyoandaliwa na mchezaji Kelvin John anayecheza soka la Kulipwa Ulaya, wanafadhiri na mchezaji huyo ambaye nyumbani kwao ni jirani kabisa na maskani ya timu hiyo.

Baadhi ya wadau wa soka mkoa wa Morogoro walidai,Michuano hiyo ya Kelvin John iliyoanza kutimua vumbi uwanja wa wazi wa Kilakala  kabla ya mchezo wa fainali  uliowakutanisha Damu Chafu na  Washashi kupigwa uwanja wa Saba saba, yalifana sana tofauti na Michuano hii ya Ndondo Cup iliyoandaliwa juzi na mdau mmoja wa soka mkoani hapa.

                  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...