Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, February 22, 2024

HII SIO MANENO HALISI NI KAMA WANASEMA

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kigoma Malima[mwenye kofia] na Rais wa Yanga  Eng Hers Said, walinaswa na kamera za Mtandao huu kwenye mchezo wa  ligi kuu kati ya KMC na Yanga.

 Katika gemu hiyo iliyopigwa dimba la Uwanja wa Jamhuri Morogoro Yanga waliwabaniza wa utozaushuru hao wa Halamashauri ya Wilaya ya Kinondoni bao 3-0.

.Picha no 1  Mkuu wa Mkoa Malima“Hongera sana Rais nawaona Yanga Mmejichimbia pale kileleni mwa Msimamo wa Ligi kuu mkiziongoza timu zote.Rias Hers” Hii ndio yanga Mkuu sio kuongoza ligi tu na hili kombe tunalibeba hakuna wa kutuzuia hao wengine tumewachia wachukue makope ya  Mapinduzi Cup na Ngao ya Jamii.

 

Picha no 2 Mkuu wa Mkoa” Haaa siamini maneno yako ngoja kwanza nisalimiane na huyu jamaa kasha nimulize kama maneno yako yana ukweli”

Eng Hers “sawa kama sio Makolo atakuambia ukweli lakini kama ni Makolo hawezi kukluambia ukweli”


 

Picha no 3” Mkuu wa Mkoa Malima” Hebwana kweli hata huyu jamaa kasema kwa Moto wa Pacome na uimara wa Kipa Mdaka Mishale Diarra kombe lenu aisee” Eng Hers Haa jamaa kajibu vizuri sana anakunywa soda gani nimuagizie?. Mkuu wa Mkoa huyu sio mtoto mdogo wa kunywa soda jiongeze Rais. Picha no 4 Mkuu wa Mkoa Malima” Je ha leo hapa kwenye uwanja wangu wa Jamhuri Mtamfunga huyu KMC? Eng Hers Said “ Mkuu ngoja wesi upo kaa uone huyu mtoto mzunguko wa kwanza nilimpiga nyingi 5-0 pale chamazi na leo nampiga gori  nyingi sina mchezo na watoto mimi”

Haya sio maneno hali ni kama wanasema kwa muongoza wa Picha zilizopigwa na Dustan Shekidele.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...