Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, February 21, 2024

MCHEZAJI WA YANGA MUDATHIR ATIMIZA AHADI YAKE KWA MLEMAVU.


 
 Mudathir Matelephone akishangilia baada ya kupachika bao la kwanza
.        .......Akiswali uwanja wa Jamhuri akimshukuru Mungu
,,,Godson akipuliza vuvuzela akishangilia bao hilo
....Mudathir[Kati] Aziz Ki [kulia] na Job kwa pamoja wakishangilia bao hilo na Mlemavu Godson



                       ...Mudathir akizungumza na mlemavu huyo
.....Aziz Ki akimuamulu Mudathir kurejea uwanjani

     Mwamba Nuru Godson akizungumza na Mtandao huu juzi


       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MCHEZAJI Nyota wa Yanga Mudathir Yahaya aliyepachikwa jina jipya na Mtandao huu la ’Mudathir Matelephone’ametimiza ahadi aliyomuahidi Mlemavu wa Miguu  Bw Nuru Godson Mkazi wa Chamwino Mkoani hapa.

 Mara baada ya kufunga bao  dakika ya kwanza ya mchezo dhidi ya KMC Mudathir  alishangilia  kwa Style yake ya kupiga simu. 

Baada ya kukata simu hiyo ya ‘Mchongo’ aliyoichomoa kwenye soksi zake’Shinigan’alipiga goti na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumsujudi kwenye Lami ya Uwanja wa Jamhuri akimshukuru kwa kumfanyia wepesi wa kufunga mabao na kuisaidia kuipaisha timu yake ya Yanga kwenye kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.

Mudathir alipomaliza kuswali Mlemavu huyo alitoka jukwaani na kwenda kumpongeza  kwa kumpa furaha aliyoifungia safari kutoka nyumbani wake Chamwingo hadi Jamhuri umbali wa takribani kilometa 3.

Kwa Upendo Mkubwa Mudathir Matelephone Mwenyeji wa  Zanzibar[Kati] aliyesindikizwa na Stephane Aziz Ki Raia wa Burkinafaso[kulia] na Dikson Nikson Job Mzaliwa wa eneo la Vibandani Kata ya Mbuyuni  Morogoro kwa pamoja walimkumbatia mlemavu huyo aliyejichora uso jina la Pacome, wakishangila naye bao hilo.

Mara baada ya kushangilia Mudathir Matelephone alimuahidi Mlemavu huyo kwamba kwa uwezo wa Mwenmyezi Mungu atafunga tena bao la pili na kuja kushangilia naye hapo alipoketi.

Mungu alijibu Maombi ya Mudathir ambapo kipindi cha Pili alifanikiwa kufunga bao la Pili hata hivyo hakuweza kuja kushangilia na Mlemvu huyo kama alivyoahidi kwa sababu ya umbali.

 lfahamike Mudathir alifunga bao la kwanza gori la Kusini mwa uwanja wa Jamhuri jirani na jukwaa aliloketi Mlemevu huyo, huku bao la Pili akilifunga kipindi cha Pili gori la Mashariki mwa Uwanja wa Jamhuri, hivyo amemuwia vigumu kuja kushangilia na Godson.

Mpira ulipokwisha Mwandishi wa Mtandao huu alimfuta Mlemavu huyo na kufanya naye mahojiano ambapo alisema.

 “Naitwa Nuru Godson usishangae hilo jina la kike ndio jina langu halisi,naipenda sana yanga nimetoka nyumbani Chamwino juka kushangilia chama langu Kipekee nawashukuru wachezaji wangu Job, Aziz Ki na Mudathir kunipa maneno ya faraja, naomba Picha zangu hizo uniletee nyumbani Chamwingo”alimalizia kusema Godson huku akipuliza vuvuzera.

Katika gemu hiyo Yanga iliibukiza KMC bao 3-0  Mudathiri akifunga bao la kwanza na la Pili huku la tatu likipachikwa na Pacome Raia wa lvory Coast.

Hadi sasa ‘Mwamba’ Mudathir Matelephone anayecheza nafasi ya kati[Kiungo] ameshapachika mabao 6 ligi kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...