Na Dustan Shekidele,Morogoro.
UBORA wa Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua raia wa lvory Coast kuzalisha mashambulizi mara kwa mara umesabaisha wachezaji wawili wa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni’KMC’ kutwangana Makonde ‘Live’ uwanjani.
Tukio la kustaajabisha lililoshuhudiwa ‘Mubashara’ na Mwandishi wa Mtandao huu limetokea jana dakika ya 36 ambapo kipa wa KMC Wilbol Massawe alilushiana Makonde na mwenzae winga wa kulia lbrahim Elias’Rasta’.
Chanzo cha ugomvi huo ni Kiungo ‘Fundi’ wa Yanga Pacome kuzalisha mashambuliaji mara kwa mara kwenye lango la watoza ushuru hao wa Kinondoni Dar es salaam, waliotumia kanuni ya TFF Kuhamisha mchezo huo kutoka Dar Kuja Morogoro wakiwa wenyeji wa Yanga yenye maskani yake Makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwa eneo la Mafuriko Dar es salaam.
Mara kwa mara Kipa huyo alimuelekeza Rasta huyo aliyeamua kutoka mbele kwenye nafasi yake kuja nyuma kusaidi ulinzi wa kumchunga Pacome ‘Mzee wa Brichi Kichwani’.
Winga huyo alipoona lawama zinazidi hasira zimepanda naye kaamua kumfokea kipa huyo akidai kazi yake si ya ulinzi,kwamba ameamua kujitoa kushuka chini kuimalisha ulinzi wa kubani safu hiyo kali ya washambuliaji wa Yanga.
Hivyo kitendo hicho cha kufokewa mara kwa mara kimemkera na kuamua naye kumfokea kipa huyo.
Chaajabu Kipa huyo kwa hasira ya kufokewa alijibu mashambulizi kwa kumsukuma Elias aliyekosa stamina kuanguka chini.
Rasta huyo alipoinua alijibu mashambulizi kwa kumtwanga konde la uso Kipa wake huyo kabla na Nahodha wa timu hiyo Awesu Awesu kutumia mamlaka yake ya Uongozi ndani ya Uwanja na kumtuliza kipa huyo huku beki Andrew Vicent’Dante’ naye akibeba jukumu la kumtulia Elias kana wanavyoonekana Pichani.
Katika hali ya kushangaza refa Mdowe kutoka Tanga hakuwapa adhabu yoyote wachezaji hao kwa kosa la kuchapana makonde uwanjani badala yake alisikika akisema ”Oya tatizo nini chezeni mpira” baada ya kusema hivyo refa huyo aliamuru gemu hiyo kuendelea.
Kitendo cha wachezaji hao kutwangana makonde kilionekana kuwachefua makocha wa timu hiyo ambapo mara baada ya ugomvi huo kuamuliwa walimuinua kipa wa hakiba Denis Richard aliyeingia kuchukua nafasi ya Kipa Massawe.
No comments:
Post a Comment