Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, February 14, 2024

JUMBE WA SIKU YA WAPENDANAO’VALENTINE DAY’2024.


Warumi 12:9-10

“Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni  lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.

Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu”

       UCHAMBUZI WA NENO HILI.

Naamini Upendo wa kweli hauna mipaka wala siku Maalumu ya Februari 14.ndio umuonyeshe upendo mtu unayempenda binafsi naona hilo haliko sawa kama maneno ya Mungu hapo juu yanavyodhibitisha.



 

Kwamba upendo wetu usiwe wa kinafiki wa kuonyesha upendo siku moja ya tarehe 14 pekee.

Anaye kupenda atakuonyesha upendo siku zote na siku moja ya tarehe 14 ndio aonyeshe upendo wa kukupa zawadi na kukutoa ‘Out’.

Pia upendo wa kweli mzani wake hauegemia kwenye pesa na mali unaegema kwenye matendo ya uwajibikaji siku zote January Mpaka December. Jumatatu mapaka Jumapili. Vile vile mzani wa Upendo wa kweli hauegemei kwenye furaja pekee unaegemea pia kwenye Shida na Machungu, kwenye eneo hili la shinda na machungu ndio utakapomjua mpenzi wa kweli au wa Magumashi.

Nifafanue hili  kwamba kumpa zawadi  mpenzi wako siku ya leo tarehe 14’Valentine Day’sio dhambi, ila dhani ni kutenga siku hii moja ya tarehe 14 kuomnyesha upendo wa dhati kwa mwenza wako huku siku nyingine unapuyanga ukimuacha patupu ukisubiri tena tarehe 14 ya mwakani ndio usambaze upendo.kama Mgao wa Umeme.

                  Happy Valentine day.

“Chukua tahadhari UKIMWI  bado upo na hauna dawa.

Nawapenda wote na Upendo wangu kwenu sio wa tarehe 14 pekee ni wasiku zote”

      .Shekidele Ez Come Ez Go’ sina hatia

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...