Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, February 13, 2024

BURIANI ENDWARD LOWASSA.1953-2024.


 

 

         Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TAA Iliyokuwa ikiangaza kwenye siasa za Tanzania imezimika, Mwanasiasa Mkongwe nchini aliyewahi kuvitumikia vyama vikuu vya siasa nchini kwa vyakati tofauti,Chama cha Mapinduzi’CCM’ na Chama cha Demokrasia na Maendeleo’CHADEMA’ Mh Edward Lowassa ameumaliza mwendo hapa duniani na jumamosi iliyopita majira saa 8 mchana aliitwa na Mungu akaitika wakati akiatiwa matibabu  hospital ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam.

Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu anatarajiwa kupunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele Februar 17 Mkoani Arusha.

           SIFA ZA MH LOWASSA.

Mimi Dustan Shekidele babu yangu aliwahi kunihusia kwamba kabla ya kugombea Uongozi kwenye vyama vya siasa au vyama vya Mpira  kwanza nijitathmini kama naweza kuyamudu mambo mawili.

Nilimuliza mambo gani hayo akanijibu, kama ninahasira au aibu nisigombee uongozi kwani huko kunahitajika kiwango cha ziada cha uvumilivu na ukomavu wa hekima busara na kusamehe.

Kwa hayati Lowassa kipaji hicho cha uvumilivu alikuwa nacho. Sote ni mashahidi wakati akijiudhuri uwaziri Mkuu wapinzani hasa Chadema walimtupia maneno mengi ya shombo lakini Mh Lowasa hakuinua mdomo  wake kuwajibu badala yake aliendelea na mambo yake.

Mwaka 2015 Mh Lowassa alihama CCM na kujiunga na Muungano wa Vyama vya SIasa nchini’UKAWA’ na kuteuliwa kugombea urais kupitia UKAWA.

Kwenye mikutano ya kampeni ya CCM baadhi ya wagombea walimpiga vijembe vikali Mh Lowassa lakini hakujibu, aliendelea kumwaga sera zake za kuelekea lkulu.

Katika uchaguzi huo 2o15 Mgombea wa CCM Hayati John Magufuli aliibuka mshindi huku Lowassa akiambulia nafasi ya pili.

Pichani Waziri Mkuu Mstaafu  Edward Lowasa[kulia] akimuonyesha  Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Tluway Sumaye moja ya habari zake zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi kwenye Mkutano wa kampeni wa UKAWA uliofanyika 2015 viwanja wa shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Morogoro.

Jinsi Lowassa anavyoonekana  kukasilika huenda habari hiyo haikumfuraisha lakini kwenye mkutano huo  Mwandishi wa habari hizi alimshuhudi Mh Lowasa akimwaha sera zake na hakuzungumza chochote juu ya habari hiyo ya kwenye gazeti.

 Ikumbukwe Sumaye naye alikihama chama cha mainduzi CCM na kujiunga na Chadema baadae Mawari hao wakuu wa Mstaafu wote walitangaza kureja nyumbani kwenye chama chao cha CCM.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Tangulia kamanda tutaonana baadae

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...