Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, February 17, 2024

YANGA KWA KMC KAMA MUEMBE WAKE WA UANI ANACHUMA ATAK,AVYO.


Mabingwa wa kihistoria Dar Yanga Afrika leo wameendeleza ubabe kwa watoza ushuru wa Wilaya ya Kinondoni KMC Kwa kuwachapa bao 3-0 kwenye mchezo ulipigwa jioni ya leo uwanja wa Jamhuri Morogoro.
lkumbukwe kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa uwanja wa Chamazi jijini Dar Yanga waliichapa KMC bao 5-0. 
 
Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye gemu hiyo baadhi ya matukio hayo ni kauli ya mlemavu aliyeshiriki kushangilia bao la kwanza na wachezaji wa Yanga. na tukio la Kipa wa KMC kuzichapa kavu kavu na mchezaji wa timu yake, 
 
Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

Mdaka Mishale Djigul Diarra akiruka juu kama nyani na kunyana shuti kali lililopogwa na mshambuliaji wa Kino Boy KMC, Picha ni 2 Mdaka Mishale akinyaka mpira huku akizongwa na Waziri Jr

,,,Gooooo ni bao safi likifungwa dakika ya 2 na mzanzibar Mdathiri
Mzawa Mdathir akiwaigia simu wapinzania wa Yanga akiwaelezxa kwamba mnahesabu mabao yake ambao leo baada ya fungnga mabao 2 amefikika bao 6 kwenye ligi kuu Tanzania bara

Mdathit na Aziz K wakjmshukuru mungu kw akusujudi kwenye lami ya uwanja wa Jamhuri Morogoro
Mlemavu huyu ambaye habari zake zitaruka hewani hivi punde alishindwa kujiuzia kapiga gia baiskeli yake na kwenda kushangilia na wacheaji wa Yanga

                 Mabeki wa KMC wakimthibiti Mdathir
Bacome bhana acha hizo yaani unaucheze mpira utakavyo ona sasa unavyotoa pasi kama hutaki vile,
Mzee wa kuchomekea na Mwiko hata sisimizi hatiti Mkongo Man Max Nzingeli akifumua shuti katikatika ya mabeki wa Kino Boy. Picha zote na Dustan Shekidele Morogoro
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...