Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, January 14, 2024

UJUMBE WA NENO LA MUNGU, TUWAKUKUMBE WAJANE NA YATIMA.

 Mwana Birthday Dustan Shekidele akimlisha Keki Kassim.
.........Akiwapa zawadi za nguo



                                    Dustan Shekidele

 

               Kumbukumbu la  Torati 15-14

“Nawe utafurahi katika sikukuu yako,wewe na ,mwanao na bint yako,na mtumwa wako,na Mjakazi wako,na Mlawi, na Mgeni, na Yatima,na Mjane aliyefiwa na Mumewe,waliondani ya Malango yako”

”And thou shalt  rejoice in thy feast,thou and thy son and thy daughter and thy  manservant, and thy  maidservant and  the Levite the stranger and the fatheriess and the widow that are within thy  gater” Huu ndio ujumbe wetu wa Leo Jumapili ya January 14.

           UCHAMBUZI WA NENO HILO.

Naamini ‘l Believe’ mafanikio tuliyoyapata au tunayoendelea kuyapata si kwa ujanja wetu bali ni Kwa Rehema za Mwenyezi Mungu.

Kama hivyo ndivyo basi sehemu ya mafanikio yetu tunapaswa kuwakumbuka  ndugu zetu wenye uhitaji Yatima, Wajane na Jirani zetu wenyechangamoto mbali mbali.

Mitume wote wa Mwenyezi wangu wanasema ‘lbada njema huanzia nyumbani’.

Desemba 25 siku ya siku kuu ya X Mas ndio ilikuwa pia kumbukizi yangu ya kuzaliwa’Happy Birthday’.  

Kwenye siku yangu hiyo bint yangu Tumain ‘Rehema’ Dustan Shekidele alinitumia zawadi ya keki.

Nilipokea keki hiyo nikaipakia kwenye pikipiki nikambeba Mjakazi wangu tukaelekea kituo cha watoto yatima cha Mehayo kilichopo Mazimbu FK Manispaa ya Morogoro, nikasheherekea siku yangu hiyo na ndugu zangu hao  Yatima na Wajane tuliikata keki hiyo tukarishana kwa upendo mkubwa.

Naamini kwenye mali zangu na mafanikio yangu si zangu peke yangu bali ni maliza za watu wote wenye uhitaji.

Kamwe ziwezi kuwa mrafi wa kujilimbikizia mali na kuzitumia binafsi ili hali kuna ndugu zangu wenye uhitaji.

 Naamini kesho nitakapoiaga hii dunia’ sitaondoka na mali zangu nitaingizwa kaburini na sandugu la pembe nne au Vipande vitatu vya Sanda, hivyo kwangu mimi mali hazina dhamani kwenye maisha yangu bali utu upendo na moyo wa kusaidi wenye uhitaji ndio kipaumbele namba moja katika maisha yangu.

‘Hasara roho Pesa Makaratasi.’ binadamu tumeumbwa  kujisahau na kukosea,hivyo nawasihi na kuisia pia nafsi yangu kama tulijisaua kuwasaidi yatima na wajane na majirani zetu wenye uhitaji nawakumbusha na kuikumbsuha pia nafsi yangu tufanye hivyo sasa hapa duniani tunapia tu kuna maisha mengine tena marefu baada ya haya yaliyojaa tabu na shida nyingi.

Kama tulijisaua kwa kutumia maliza zetu nafamilia zetu pekee na kuwapa kisogo Yatima na Wajane nawakumbusha na kuikumbusha pia nafsi yangu tuwakumbuke ndugu zetu hao kwani , tukakapokufa kesho tutaziacha hizo mali tutaenda kwa Mungu na Roho zetu Pekee.

 Mifano iko hai matajili wangapi wamekufa na kuziacha mali zao ambazo kwa sasa zinagombewa na watu kiasi cha kupelekeana mahakamani kila mtu akisaka uhalali wa kumiliki mali hizo.

Wakati hayo yakitokea duniani Mwenye mali naye  roho yake iko mbele ya hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Yesu alisema ‘Tajiri kuingia Peponi ugumu wake ni sawa na Ngamia kupenye kwenye Tundu la Sindano’ Kauli hiyo ilimstua mmoja wawanafunzi wa Yesu ambaye alibeba ujasili wa kumuliza swali” Mwalimu’Yesu’ Kama hivyo ndivyo hakuna tajari atakayeingia pepo?. Yesu akamjibu.

” Atakaye ingia ataingia kwa Neema ya Mungu Pekee” Kwa kauli hiyo na Yesu Kristo[Nabii lssa] ni kwamba kuwa tajiri sio dhambi bali utaji wako unautumiaje? Unawakumbuka wenye uhitaji Yatima na Wajane? Unaikumbuka siku ya Bwana kuitakasa’kwa maana kwenda kwenye lbada? Auko uko bize na mali zako?

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...