Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, January 15, 2024

UDAKUZ SPESHO. AMA KWA HAKIKA KIFO KIKIFIKA UNAKITAFUTA MWENYEWE.


                 Pikipi ya Mwandishi wa Mtandao huu


Na Mdakuzi Dustan Shekidele.

Mdakuzi wa Mtandao huu leo anaripoti udakuzi kutoka Gongola Mboto Jijini Dar es salaam.

 Kama kawaida habari hii ya kuhudhunia tunairipoti kwa Mfumo wa Udakuzi kwa sababu haijakamilika kwa maana ya kuzungumza na Wahusika’Ndugu wa Marehemu pamoja na Mamlaka za Serikali.

Ama kwa hakika siku  ya kifo inapofika unakifuata mwenyewe, kauli hii imetimia juzi January 12 siku ya Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo dada mmoja Mrembo Jina linahifadhiwa kwa sababu za kiudakuzi  nilizozitaja hapo juu.

Mahuhuda wanadai,Mrembo huyo anayeishi Gongo la Mboto anafanya kazi kwenye moja ya hotel kubwa iliyopo Kariakoo, hivyo siku hiyo ya January 12 alidamka asubuhi na mapema akamuaga Mpendwa Mume wake, pamoja na watoto wake wawili, mdogo akiwa na Umri wa Mwaka mmoja na mwingine miaka 5.

 Alipolmaliza kuagana na familia yake Mrembo huyo huyo alielekea kituo cha daladala akapanda basi la Kariakoo.

 Kwa sababau siku hiyo ya  ilikuwa ni siku ya mapunziko ya Sikuu ya Mapinduzi watu wengi hawakwenda makazini, hivyo daladala zilichelewa kujaa muda huo wa asubuhi. Mrembo huyo baada ya kuona muda unasonga na daladala haijai yeye na abiri mwingine walishauriana wachange pesa wakodi boda boda iwakimbize Kariakoo.

Mashuhuda wa tukio hilo waliendelea kudadavua kwamba boda boda hiyo ilipofika mbele kidogo iligongana uso kwa uso na gari ambapo boda boda na mrembo huyo ambaye kabila lake ni Msambaa walikufa hapo hapo huku yule abiri wa pili aliyekaa Mwisho wa Pikipiki kwa sasa imeelezwa yuko hospital chumba cha  I.C.U akipumulia mashine kuokoa maisha yake.

 Baada ya kupokea taarifa hizo Mdakuzi alimtwangia simu Glory ambaye ni shangazi wa Marehemu

” Dustan ni kweli [anamtaja jina] amefariki kwa ajari ya pikipiki, kama unavyojua hivi karibuni alibariki ndoa yake na mzazi mwenzake ambaye ni Muha wa Kigoma.

Hivyo Mumewe ambaye kimsingi ndiye mwenye mamlaka ya kuamua mkewe azikwe wapia ameamua  azikwe hapo hapo Dar.

Juzi ndugu wengi akiwemo mama yake mdogo wametoka huku Tanga wameenda Dar tulipozungumza nao jana wamedai mazishi Leo jumatatu baada ya taratibu za kipolisi kukamilika”alisema Shangazi huyo Mkazi wa Jijini Tanga na kuongeza.

”Shekidele kinachotumiza huyo marehemu baada ya kuzaliza tu kesho yake Mama yake amefariki hivyo alilelewa na Mama yake Mdogo, na yeye amefariki juzi ameacha watoto wawili akiwemo wa mwaka mmoja ambaye mama yake huyo mdogo atabena tena jukumu la kumlea mtoto huyo akama alivyofanya kwa mama wa mtoto”alisema Glory na kuangua kilio.

Takribani miezi Miwili iliyopita Mwandishi wa habari hizi alichati na Marehemu huyo kwa mtandao wa Whatspp ambapo kwenye Profaili aliweka Picha ya harusi akiwa na shera huku akimkumbatia Mpendwa Mume wake.

“ Umezimika kama Mshumaa.Mwendo umeumaliza mama wawili nenda salama tutaonana Baadae”

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe wote tuseme amen”

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...