Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, January 10, 2024

HII KALI.SHUJAA JUMA VIGOGO AMEFANYA MAAJABU MENGINE




 


 Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Yule Shujaa Juma Sadick ’Almaarufu Juma Vigogo’aliyezama Mto Morogoro na kufanikiwa kuopoa mwili wa Dent wa darasa la 3  Hayati Sabrina[9] mwezi uliopita

Jana kafanya Maajabu mengine ya kuning’inia na kuruka sarakasi juu ya kilele cha Mti Mrefu.

Mara baada ya kufanya michezo hiyo ya hatari juu ya Mti huo ‘Muashoki’uliokuwa katikati ya nyumba aliukata kimiujiza  bila kuathiri kitu chochote zikiwemo kuta za Nyumba, karo pamoja na  maua yaliokuwa chini ya mti huo.

lkumbukwe takribani miaka 5 iliyopita Juma Vigogo alifanya Maajabu ya kupanda Juu ya Muwembe Mkubwa wenye umri wa zaidi ya miaka 100,na kuning’inia kwenye kitawi kidogo kilichopo juu ya kilele cha Mwembe huo uliopo jirani na Shule ya  Msingi Mwembesongo.

Baada ya kuona hivyo watu waliogopa wakihisi  anaweza kuanguka na kupoteza Maisha hivyo  baadhi yao wakiwemo ndugu zake waliamua kutoa taarifa Polisi.

Maafande hao Walipofika walimuamuru ashuke aliwagomea katu katu Polisi hao walitumia mbinu zote za kijeshi Juma Vigogo aligoma kushuka.

Baada ya juhuzi hizo kugonga mwamba taasisi nyingine zilifika eneo la tukio kuongeza nguvu,  taasisi hizo ni  Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Tanesco, Watu wa Msalana Mwekundu pamoja na Waandishi wa habari.

Baada ya taarisi zote  kufika eneo la tukio huku kundi kubwa la wananchi likiwa eneo la tukio  Juma Vigogo aliendelea kugoma kushuka juu ya mti huo.

Kuona hivyo Tanesco waliamua kutumia gari  lao lenye  kifaa maalumu cha kupanda juu ya miti mirefu, Juma Vigogo baada ya kuona winji hiyo inaelekezwa kwake alizidi kusogea kileleni mwa mti huo na gari hilo kushindwa kufika eneo hilo.

Maafande wa Zima Moto na Uokoaji walipanda juu ya mti huo lakini walishindwa kufika kwenye kitawi hicho chembamba alichokalia Juma Kigogo.

Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa wa kwanza kufika eneo hilo alipoelekeza kamera yake kumpiga Picha Juma Vigogo alitishia kuikojolea  kamera hiyo.

 Kwa mkwara huo Mwandishi huyo alitumia mbinu za kipaparaza na kufanikiwa kumpiga Picha Juma Vigogo bila yeye kujua

Baada ya juhudi zote hizo kuferi Mwandishi wa Mtandao huu alimfuta Mzee Ngozoma ambaye Muembe huo uko eneo la nyumba yake kwa lengo la kuhitaji maoni na mawazo yake juu ya  tukio hilo.

Mzee Ngozoma ambaye kwa sasa ni Marehemu alisema.

”Shekidele huyu hata mfanye nini hamuwezi kumshusha mpaka mwenyewe atakapo amua kushuka”alisema Hayati Mzee Ngozoma. Alipoulizwa nini kifanyike sasa, Mzee Ngozoma alisema ‘Wambiye Maaskari wawatawanye watu wote waondoke eneo hilo kisha na hao Polisi  waondoka hapa pakiwa peupe Juma Vigogo anashuka Mwenyewe msiwe na wasi wasi hawezi kuanguka ile ndio michezo yake huyu kijana” alisema Mzee Ngozoma.

Baada ya maelezo hayo Mwandishi wa Mtandao huu alimfuta aliyekuwa Mkuu wa kituo kikuu cha Polisi Wilaya ya Morogoro Afande ldd na kumueleza ushauri huo uliotolewa na Mzee Ngozoma.

Afande ldd ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Polisi OCD  Moja ya Wilaya za Mkoa wa Dodoma aliupokea ushauri huo na kuwatawanya watu hao.

Kweli baada ya watu kuondoka Juma Vigogo alishuka na kuelekea nyumbani kwake.

Kesho yake Mwandishi wa Mtandao huu alitinga nyumbani kwake na kumuliza kulikoni kufanya tukio lile na kuzigomea taasisi nyeti za Serikali.

Juma Vigogo alijibu

”Shekidele kwani kupanda juu ya mti ni kosa la jinai?ule Muemnbe unazidi ya kalne moja hivyo unamajini nilivyotoka kufanya kazi zangu za kukata miti nimenunua soda  nimekaa chini ya ule Muembe nimehisi  juu ya ule mti kuna majini nimeamua kuyafuata kule kule juu hata angekuja nani pale nisinge shuka ningeshuka kwa muda ninaotaka mimi”alisema Juma Vigogo.

Habari za tukio hilo ziliruka hewani kwenye Magazeti ya Global Publishers pamoja na Mitandao ya Global Publishers.

Ingia kurasa za Facebook za Shekidele Mkude Simba na ile ya Dustan Shekidele uangalia Clip Video Juma Vigogo akifanya maajabu juu ya Mti.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...