Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, January 21, 2024

UJUMBE WA NENO LA MUNGU. MTETEENI MJANE.


 


Isaya 1-17

“Jifunzeni kutenda Mema.takeni hukumu na haki wasaidieni walioonewa,Mpatieni Yatima haki yake, Mteteeni Mjane”

“Learn to do well seek judgment relleve the oppressed,judge the fatherless plead for the widow”.

                          UCHAMBUZI.

Neno la Mungu linatukumbusha kutema mema, wale wenye mamlaka yakutoa hukumu wamekumbushwa kutoa hukumu ya haki.

Tunakumbushwa pia kuwasaidia wanaoonewa kwa namna yoyote ile, Pia tuna kumbushwa kumpatia Yatima haki yake na kumtetea Mjane.

 Leo kwenye jamii yetu baadhi ya watu wamekosa hofu ya Mungu wanawadhuruma Yatima na Wajane haki zao, mbaya zaidi wanaofanya hivyo wengi wao  ni ndugu wa  familia ya Yatima na Mjane huyo, Kisa ni tamaa ya Mali iliyoachwa na  Wazazi wa Yatima huyo au Mume wa Mjane huyo aliyefariki dunia, hii ni dhuruma kubwa ambayo ni chukizo mbele za Mungu.

Hilo ndilo neno la Mungu leo Jumapili ya January 21, Mwenye Masikio na asikie asiye na Masikio, aendelee kuwadhurumu Yatima na Wajane,kiburi chake kiyaishia kaburini siku yake ya mwisho.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...