Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 23, 2024

UDAKUZ SPESHO. SEHEMU YA PILI MREMBO ALIYEFARIKI DUNIA KWENYE BODA BODA NGONGOLA MBOTO DAR.

                    Pikipiki ya Mdakuzi wa Mtandao huu
 

 

Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro.

INA UMIZA SANA.KAMA UNAMOYO MDOGO UKISOMA HABARI HII LAZIMA UTOKWE NA MACHOZI.

Wiki iliyopita Mtandao Pedwa wa Shekidele uliriripoti kifo cha Mrembo aliyefariki dunia kwenye ajali ya boda boda akitokea nyumbani kwake Gongolamboto akielekea kazini Kariakoo.

Mrembo huyo aliyebariki ndoa yake kanisani hivi karibuni ameacha watoto wawili wa kwanza yuko darasa la kwanza na wa pili anaumri wa Mwaka mmoja.

Habari ya kuhudhunisha inayoendelea kuliza wengi ni matukio ya watoto wa Marehemu yanayoendelea kwa sasa baada ya Pendwa Mama yao kufariki dunia ghafla.

Jana Mdakuzi wa Mtandao huu aliamua kumpigia simu Bi Glory ambaye ni Shangazi wa Marehemu na kumuliza Maendeleo ya Maisha Mapya ya watoto hao  bila Malezi ya Mama yao.

Glory anayeishi Jijini Tanga alijikaza na kujibu swali hilo hukua akikatisha maongezi  mara kwa mara kwa Vilio.

”Dunstan watoto wa Marehemu wanaendelea kutuliza huyo mkubwa awari tulimficha juu ya kifo cha Mama yake. Kesho yake kauliza jamani mbona Mama harudi kazini toka jana? Tukamwambia atarudi akaenda nje kucheza wenzie uko kwenye michezp yao wakamwambia mama yako amefariki na ajali ya bodaboda, basi tukawa hatuja jinsi tukaamua kumueleza ukweli.

Shekidele huyo Mtoto anaakili za ajabu baada ya kumpa taarifa hizo  kasema maneno haya.” Sasa nani atamnyonyesha mdogo wangu? Tukamwambia atakunywa maziwa ya kopo baadae kasema hatakia kukaa hapo nyumbani kwa baba yake anataka kwenda kukaa kwa mama yake mdogo anayeishi hapo hapo Dar anasema akikaa hapo kila wakati atamkumbuka  Mama yake, tumetii ombi lake tumempeleka kwa Mama yake mdogo ingawa kwenye kikao cha familia tumekubaliana badae tumpeleka Bording kwa utulivu zaidi”alisema Glory na kuongeza.

“ Wifi yangu kwa Maana ya Mama Mdogo wa Marehemu amemchukua Mjukuu wake huyo wa Mwaka Mmoja na kuja naye huku Tanga kama unavyojua huyo Mtoto ana umri wa Mwaka mmoja alikuwa bado ana nyonya zima la Mama yake hivyo ghafla tumemuanzisha maziwa ya kopo kwa vile hakuyazowea ameanza kudhoofu afya yake, kwani pia alikuwa akihitaji zaidi joto la marehemu Mama yake”alisema Glory na kuangua kilio kisha kukata simu kwa uchungu.

Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuipa faraja familia hiyo katika kipindi hiki kigumu huku tukiendelea kumuomba Mungu awalinde na kuwakuza watoto hao sambamba na kumtia nguvu na kumpa ujasiri wa Uvumilivu Mgane’Mume’ wa Marehemu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...