Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 16, 2024

KIGOGO WA POLISI ATOA SEHEMU YA MSHAHARA WAKE KUWANUNUOA VIFAA VYA SHULE MAWANAFUNZI 20 AMBAO WAZAZO WA WAMEKOSA UWEZO WA KUWANUNULIA.

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha[kulia] akikabidhi Vifaa hivyo
                         ....Akizungumza na Wanafunzi hao
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake naye akizungumza na Wanafunzi hao ambao baadhi yao wana sale za shule za chakavu.
 


                                          Na Dustan Shekidele,Morogoro.
 
Kigogo wa Polisi Wilaya ya Malinyi Mkoani hapa limekabidhi vifaa mbali mbali kwa Wanafunzi ‘Madent’ lshirini (20) wa shule ya msingi Ifungila iliyopo kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, waliorejea shule bila vifaa Vipya vya shule.
 
Hili limekuja baada ya wanafunzi hao kudai Wazazi na walezi wao wameshindwa kuwanunulia Vifaa hivyo kutokana na hali duni ya maisha. 
 
Kufuatia hali hiyo Kigogo wa Polisi Wilayani hapo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha liliguswa na kuamua kudhamini pambano hilo kwa kuwanunulia vifaa madent wote 20.
 
Vifaa alivyonunua Afande huyo ni pamoja na Uniform. Madaftari na Kalamu kwa madent wote 20.
 
Akizungumza na walimu na Wanafunzi wa shule hiyo Januari 16, 2024 wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Afande Michael Rasha ambaye ni Polisi Kata wa Kata hiyo amesema, Kitendo cha wanafunzi hawa kurudi shuleni mwaka mpya wakiwa na vifaa vya mwaka jana kimemsikitisha na kumgusa jambo ambalo limepelekea kuchukua maamuzi ya kununua Vifaa hivyo na kuwapelekea Wanafunzi hao.
 
Naye Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake anayehudumia Kata jirani na Usangule amewataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii ili waje kuwa msaada kwa familia zao.
 
Polisi Kata hao kwa ujumla wao walitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa Wanafunzi namna ya kujilinda na vitendo vya Ukatili, na kutoa taarifa maeneo husika huku wakiwataka kulindana wao kwa wao.
Aidha wanafunzi hao walifundishwa miladi ya Polisi Jamii ikiwemo Usalama wangu kwanza, Familia yangu haina muhalifu Pamoja na kauli mbiu ya Polisi Jamii.
 
Kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo Mwalimu Ally makambi Mohamed ametoa shukran za dhati kwa Askari hao na kuitaka Jamii kuiga mfano huo.
 
“Hapa shuleni kuna wanafunzi wengi ambao wanauhitaji wa vifaa vya shule, hivyo kama kuna mdau yoyote anaweza kufika na kutoa alicho jaaliwa itasaidia kuotoa tabaka kwa wanafunzi wenye nacho na wasio nacho”Alisema Mwalimu huyo. 
 
Kipekee Mtandao huu unampongeza sana Afande Michael Rasha kwa moyo wake wa huruma wa kuwakumbuka watu wenye uhitaji.
Kwa moyo wake huo wa Upendo Mtandao huu Unamuombea kwa Mwenyenzi Mungu azidi kumpatia Vyeo vya Juu Afande huyo ili azidi kuwasaidia Watu wenye uhitaji. 
 
Maaskali wengine hasa wale wenye vyeo wa Juu na wasio na Vyeo igeni mfano wa Afande Rasha wa kuisaidia Jamii yenye uhitaji.
Kipekee Mwandishi wa habari hizi anafurahishwa sana kuona mtu ana wanawakumbuka watu wenye uhita

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...