Muonekano wa Mji wa Morogoro, Mdakuzi alipiga Picha hii akiwa juu kabisa ya kilele cha Milima ya Uluguru yanapotoka Maji hayo Mto Moroogoro.
Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro.
Kwa Masigitiko Makubwa Mdakuzi wa Mtandao huu anaripoti habari hii huku akiwa na hudhuni kubwa Moyoni kufuatia tukio hili la kusigitika na kuumiza moyo.
Habari hii leo naiandika kwa mfumo wa Udakuzi kwa sababu haijakamilika, Mungu akipenda tutaikamilisha kesho au keshokutwa baada ya kuzungumza na Wafiwa, Uongozi wa Serikali ya Mtaa pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro’RPC’
Majira ya saa 9 Alasiri Mwanafunzi wa kike aliyekuwa akisoma darasa la tatu anadaiwa kufariki dunia baada ya kusombwa na Maji ya Mto Morogoro yaliyokuwa yakiporomoka kwa kasi kutoka juu ya Milima ya Uluguru kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha siku ya leo. .
Baada ya kutokea kwa tukio hilo watu mbali mbali walimpigia Simu Mwandishi wa Mtandao huu akiwemo Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huyo ambao kwa sasa nahifadhi jina lamtaa huo na majina ya mashuhuda hao.
Fasta Mdakuzi alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendokasi na ndani ya dakika sifuri alifika eneo la tukio moja kwa moja aliingia mzigoni akiwahoji mashuhuda.
“ Shekidele mtoto anamtaja jina anasoma darasa la tatu anataja jina la shule, baada ya kutoka shule alipewa chakula na Mama yake alipomaliza kamuaga mama yake kwamba anakwenda kucheza na wenzie”alisema shuhuda huyo na kuendelea.
“ Kwa sababu tunaishi jirani na mto na leo mvua imenyesha zaidi kule juu ya Milima mto umejaa maji hivyo Mtoto huyo na wenzie waliamua kwenda mtoni kuangalia maji hayo yalivyojaa, kwa bahati mbaya wakati wakiendele kuyashangaa mtoto huyo katereza na kuzama kwenye mto na kusombw ana maji hayo yaliyokuwa yakienda kasi.
Kuona hivyo wenzie walikimbia kumueleza mama yake ambaye alipofika hakumuona mwanae kwa uchungua kaanza kuangua kilio akitaka kuzama kwenye maji kumtafuta mwanaye watuwamshika huku Uongozi wa mtaa umepiga simu Faya wamefika kwa sasa wamezama mtoni kumtafuta.
Maafande hao wa Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kumpata maeneo ya Mzambarauni darajani barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam pale wanapoosha Malori akiwa amefariki dunia.
Kaletwa sasa hivi baada ya kufika hapa mtaani kila mtu ni kilio”alisema shuhuda huyo.
Kesho Mdakuzi atafuatilia tukio hilo A-Z hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment