Viongozi wa MOROPC waliotinga kwenye kikao hicho kutoka Kulia ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji Mohamed lssa. Mhasibu Loveness Nyawila. Katibu Mkuu Lilian Lucas Kasenene, RPC Mkama. Mwenyekiti Nikson Mkilanya na Mratibu wa MOROPC Thadei Hafigwa wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kikao kazi hicho.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Uongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro umekutana na Uongozi wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro wakijadili mambo mbali mbali ikiwemo utendaji kazi wa taasisi hizo.
Kikao kazi hicho kimefanyika jana Majira ya saa 4 asubuhi ndani ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama.
Akitoa taarifa za kikao hicho kwenye Group la WhatSapp la Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ Mwenyekiti wa chama hicho Niksoni Mkilanya alisema.
”Lengo la Uongozi wa MOROPC ni kukutana na wadao wa habari Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri na kujadili changamoto zinazoibuka baina ya waandishi wa habari na wadau hao.
Leo tumekutana na RPC tumezungumza naye mambo mengi ukiahidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro litaendelea kuweka Mazingira Mazuri ya kikazi kati ya Polisi na Waandishi wa habari”alisema Mwenyekiti huyo.
Baadhi ya wadau wengine wa habari mkoa wa Morogoro ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.Ofisi za wabunge wa Mkoa wa Morogoro, TAKUKURU, Uhamiaji. Jeshi la Zima Moto na Uokoaji.na Sekta Binafsi.
No comments:
Post a Comment