Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, December 10, 2023

SHUJAA ALIYEMUOPOA HAYATI SABRINI MTO MOROGORO HUYU HAPA


 

SHUJAA aliyezama Mto Morogoro wenye kina kirefu cha Maji na kumuopoa hayati Sabiri Mwamba huyo hapa Juma Sadick’Maarufu Juma Vigogo’

Huku akirekodiwa na Video Camera Juma Vigogo amefunguka mazito ugumu aliopata kiasi cha kupata mwili wa Mtoto Sabrini.

Kwa ushujaa huo juzi familya ya hayati Sabrini walimuita na kumkabidhi pesa kama shukrani, hata hivyo Juma Vigogo alizikataa pesa hizo akidai yeye alitenya kwa mapenzi na si kwa malipo.  

Baada ya kulazimishwa sana Juma alipokea pesa hiyo na kwenda kuzitoa sadaka Msikitini.

” Nyinyi mmefiwa ilitakiwa mimi niwape nyinyi pole kwa kuondokewa na mtoto wenu, kwa kuwa mmeniradhimisha sana nahsii nisipopokea hizi pesa nitazidi kuwapa simani hivyo pesa hizi nazichukua napeleka Msikitini”alisema Juma Vigogo ambaye ni Maarufuni Mkoani Morogoro kwa kukata Miti na kufukua Vigogo ndio maana amepachikwa jina la Juma Vigogo.

Baadae Mtandao huu utarusha Clip Video hiyo hivyo usicheze mbali na Mtandao wa Shekidele umsikie Shujaa huyo akisimulia kwa uchungu alivyopitia njia ngumu za kupata Mwili wa Mtoto Sabrina.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...