Ukimaliza kazi utavishwa taji.
Simon akimpongeza bint yake kwa kumvisha taji baada ya kupokea kipa lmara.
Gladys akiwasili nyumbani kwao Tubutu Mfuruni
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Juzi Jumapili ya Desemba 17 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania’KKKT’ Usharika wa Mji Mwema, limewabariki wahitimu zaidi ya 20 wa Mafunzo ya Kipa lmara, huku kivutio kikubwa ni hotuba ya mgeni rasmi Kigogo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro.
Kwenye tukio hilo la Kipa lmara Uongozi wa Usharika huo unaongozwa na Mchungaji Simba ulimwalika Afisa huyo wa Jeshi la Polisi kuwa mgeni rasmi, aliyetoa hotuba iliyogusa mioyo ya waumini waliofurika kwenye kanisani hilo ambalo lipo Nane Nane Tubuyu Kata ta Tungi Manispaa ya Morogoro.
Miongoni mwa wahitimu hao ni Gladys Simon Nkongolo ambaye baba yake Simon Nkongolo alisoma Uandishi wa habari na Mwandishi wa Mtandao huu kabla ya Kutimkia serikali na kupata ajira ya Afisa Mtendaji wa Moja ya Kata za Manispaa ya Morogoro.
Mpiga Picha Mzowefu wa Mtandao huu ndiye aliyepewa Jukumu na Familia ya Nkongolo Kupiga Picha matukio yote kuanzia kanisani mpaka ukumbini.
Ama kwa hakika Gladys Bint Simon Nkongolo’alidamshi ile ile’ alipendeza vilivyo hasa unywele wake uliowafunika wahitimu wote ‘Mwanamke Mwenye bhana uweka Upara Umefiwa?’
NINI MAANA YA KIPA IMARA.
Kwa Imani ya KKKT Mtoto mara baada ya kuzaliwa ni lazima abatizwe akisimamiwa na Wasimamizi wawili ambao jukumu la wazazi hao wa Kiroho ni kumsimamia na kumuongoza kuishi Maisha ya Kiroho mpaka atakapokuwa mtu mzima na kuwa Mkristo kamili.
Akishapata Kipa lmara majukumu ya Wazazi hao wa Kiroho yanapungua kwa asilimia kubwa kwenye maisha ya Mtoto wao huyo wa Kiroho.
Sheria ya kanisa hilo huwezi kuingizwa kanisani hapo kama hujapitia mafunzo hayo ya miaka 2 ya Kipa lmara.
Mara baada ya kutoka Kanisani Gladys aliandaliwa sherehe kabambwe iliyofanyika nyumbani kwao Tubuyu Mtaa wa Mfuruni jirani na Ofisi Kuu za NIDA Mkoa wa Morogoro ambapo watu walikula na Kunywa Mwanzo Mwisho.
Kama kawaida picha nyingine kali la matukio hayo zipo chini ya Story hii au fungua Profali la Mtandao huu kuangalia Picha hizo.
No comments:
Post a Comment