Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 16, 2023

KIGOGO WA CHUO CHA BIBLIA ATINGA KWENYE KIPA IMARA.

               Jackline akiingia ukumbini kwa madaha


                             ....Wazazi nao wakiingia ukumbini


Kila hatua ni sara,
Mwana Kipa lmara Jackline Daniely Dolnad akiangusha maombi mara baada ya kuwasiri ukumbini

Jackline kulia akiwa tambulisha wazaza wake kushoto ni Baba yake Mazazi Daniely Dolnad kati ni mama yake mzazi Judith Kijangwa


                      Jackline akiwarisha keki wazazi wake

Jacline akimrisha Keki Anjalina Tamilwai Shekidele ambaye ni Mama mzazi wa Mama yake.

Wazazi wakimuhusia binti yao baada ya kuwa mkristo kamili


Ninaposema shughuri ilinoga namaanisha kweli kweli,
Mpiga Picha wa Mtandao huu akishuhudia show kali ya Baba Jackline akionyesha umwamba wa kulisakata Rhumba na Mjomba'ke

                                       Dustan Peter Shekidele

Peter Kijangwa na mkewe ambao ni baba na mama wa ubatizo wa Jackline wakimpa zawadi ya Maokoto Mtoto wao wa Kiroho waliyemuongoza vyema mpaka alipopokea Kipa lmara na kuwa Mkristo kamili. Maokoto hayo si ya kitoto nyekundu nyekundu kama 10

Chalii Tamilwai Zakaria Shekidele aliyefuka safari kutoka Mitaa ya Unga Limited Arusha Mpaka Mitaa ya Nane Nane Morogoro akimpa zawadi dada yake



 Matron wa Chuo cha Biblia Vuga Christina kulia akiwa na Jackline


       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 KIGOGO wa Chuo Cha Biblia  Christina Shekidele ametinga kwenye Sherehe ya Kipa lmara ya Jackline Daniely Dolnad.

 Sherehe hiyo iliyoratibiwa kisomi imefanyika Jumamosi iliyopita Ukumbi wa Road View Motel Mtaa wa Area Six,Nane Nane Oil Com kando kando ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam.

Watu kutoka Mikoa mbali mbali ikiwemo  Arusha, Dar-es Salaam, Tanga na Morogoro wakiongozwa na Matroni huyo wa  Vuga Bible School, Bi Christina Shekidele walihudhuria sherehe hiyo iliyonoga vilivyo.

Chuo hicho cha Biblia Kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri Tanzania’KKKT;kipo Tarafa ya Vuga Wilaya ya Lushoto Mkoa Tanga. lfahamike Chuo hicho pia ninazalisha watumishi wa Mungu wakiwemo Wainjiristi na Mapalishiweka.

 Jackline alipokea Kipa lmara hiyo Mwaka jana KKKT Usharika wa Mji Mwema Uliopo Nane Nane Tubuyu Manispaa ya Morogoro.

Kwa Mapenzi wa Mungu usiku wa Jumapili ya Desemba 18-2022 siku ambayo Jackline anapokea Kipa lmara Mama yake Mkubwa kwa Maana ya bibi wa Mama yake alifariki dunia.

Hivyo kwa hekima Asubuhi Jackline alijikaza na kwenda kanisani Kupokea Sakramenti hiyo ya Kipa lmara’ na baada ya kutoka kanisani alikuja Mtaa wa Mji Mwema kumzika Mama yake Mkubwa aliyezikwa siku hiyo hiyo ya Jumapili Makaburi ya Kolla Mkoani hapa.

Kufuatia Msiba huo Mzito Kamati ya Maandalizi ya Sherehe kwa kushirikiana na familia waliamua kuahirisha kwa kipindi cha  Mwaka mmoja hatimaye Jumamosi ya Desemba 9-2023 kamati  ilifanya sherehe hiyo Kabambe.

Mpiga Picha wa Mtandao huu ambaye pia ni sehemu ya ndugu wa familia ya Jackline ndiye aliyepewa jukumu la Kupiga Picha  za Video na Mnato Matukio yote ya Sherehe hiyo ya ‘Kijanja’.

Mtandao huu uliripoti Kifo cha Mama huyo ambapo wadau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele wanakumbuka vizuri matukio ya Picha za Msiba huo

Kesho Jumapili Desemba 17 Kanisa hilo la KKKT Usharika wa Mji Mwema wahitimu wa Mafunzo ya  Kipa lmara wanabarikiwa.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...