Rapa Mahiri wa band hiyo Yahya Masauti’Uchebe’ akirap kwa Style ya kumkoreza densa huyo, mzuka umempanda kaacha kurap anawakodolewa macho mashabiki Yahya bhana hayo machozi vp sasa Mlala Nje anakuona.
Na Mlala Nje Dustan Shekidele,Morogoro.
Densa Maarufu Mkoani Morogoro anayepiga kazi Band Pendwa ya Maisha Mapya ’Wana Full Vipaji’Omar Ally Maarufu ’Chiba Soon’amepata dili za kunengua kwenye Promotion ya kampuni mmoja ya Bia jina linahifadhiwa kwa sababu za kulinda haki za Matangazo.
Mcheza show[Densa] huyo ambaye kwa kipindi kirefu hajaonekana kwenye band hiyo inayoongozwa na vijana wengi waliokomaa vichwa kwa ugumu wa Maisha.
Jumamosi iliyopita Usiku Mnene Mlala Nje akiwa kwenye Pilikapilika zake za kusaka matukio kwenye kumbi za Starehe, Majira ya saa 6 usiku akiwa na Usafiri wake wa Pikipiki ya Mwendo Kasi ‘Boxer’alitinga Ukumbi Mmoja jina [kapuni] uliopo Modeko Kata ya Mazimbu Mkoani hapa alimshudia densa huyo mwenye ulemavu wa Mguu akiweka kando Magongo yake yanayomsaidia kutembea na kupanda jukwaani akinenguza zaidi ya nusu saa akitumia Mguu mmoja pekee kama anavyoonekana Pichani.
Kufuatia umahiri huo baadhi ya mashabiki walivutiwa na uchezaji wake na kuamua kupanda jukwaani kummwagia Mapesa a.k.a Maokoto.
Baada ya kushuka Jukwaani Mlala Nje alimfuata na kumuliza kulikoni kitambo kirefu hajaonekana kwenye show za band hiyo nini shida densa huyo alijibu.
”Ni kweli Shekidele kitambo sana sikuwa na wanangu wa Maisha Mpya nilipata dili ya kuzunguka mikoani kwenye Promotion ya Kampuni ya bia[anaitaja jina].
Kwenye Promotion hiyo nilikuwa na cheza shoo kwenye umati mkubwa wawatu, nilizunguka na kampuni hiyo zaidi ya Miaka 10 ya Tanzania Bara.
Promotion hiyo imetamatika mwezi uliopita hivyo nimerejea nyumbani kwenye band yangu ya Maisha Mapya”alisema Densa huyo anayemiliki mke na watoto kadhaa.
Mlala Nje kama kawaida alimpiga swali la nyongeza.
Mlala Nje. Mwamba Kwa ziara hiyo ya zaidi ya mikoa 10 na kampuni hiyo kubwa ya bia maokoto yako kwa sasa yako vizuri.
ChIba. Haaa Shekidele sihabari usiposhukuru kidogo hata kikubwa huwezi kushukuru namshukuru Mungu kwa hicho nilichopata pia nawashukuru Viongozi wangu wa band hii ya Maisha Mapya kunipa ruhusa ya kuzunguka mikoani zaidi ya miezi 4 na Kampunui hiyo ya Bia.
No comments:
Post a Comment