Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 13, 2023

KUMBUKIZI YA KIONGOZI WA SIMBA KUSHIRIKI MICHUANO YA TAIFA YA NETBALL.


Veronika alikitaja kikosi hicho kilichoshiriki michuano ya Taifa, kutoka kushoto walioketi ni Amina Chuchunge ambaye ni kigogo wa shirika la Tanesco Mkoa wa Morogoro aliyestaafu mwaka 2020.Ania Morania ambaye kwa sasa ni marehemu.Rose John.Ashura Mfuru ambaye pia amefariki dunia.

Tausi Kizee.Petronia Banzi.na wa mwisho kulia anayecheka ni Mwalimu Mwammvua ambaye ni Mke  wa Marehemu Amri lbrahimu mchezaji wa zamani wa Simba.

Waliosimama kulia ni Veronica Mlangwa na kushoto ni Mwalimu Banzi jina la kwana amelisahamu.

                          Veronica Mlangwa mwaka 1980
Bi veronika alipochaguliwa na wanachama wa Simba mkoa wa Morogoro kuwa Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa tawi kuu la simba kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba 15-2019.
 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kama kawaida Mtandao huu huchimba habari za chini ya Kapeti ambazo huwezi kusipata Popote zaidi ya Mtandao Pendwa wa www.Shekideletz.blogspot.com unaosomwa na watu wengi Pande zote za dunia.

Leo Mtandao huu unakuretea habari ya Kiongozi wa tawi kuu la Simba Mkoa Morogoro Maarufu ‘Shujaa ngome kuu’ Veronica Mlangwa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa tawi hilo’

 Bi,Veronia Maarufu Mama Makame ambaye pia ni mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Netball ya Mkoa wa Morogoro’Moro Stars amefunguka Mazito juu ya maisha yake ya kimichezo.

Akizungumza na Mwandishi wa  habari hizi kwenye Mahojiano Maalumu ndani ya tawi la shujaa lililopo Kata ya Mji Mpya, Bimkubwa huyo alisema toka utotoni mwake alikuwa akiupenda mpira wa Miguu na mahaba yake Makubwa mpaka sasa yapo kwenye timu ya Simba.

”Japo nilikuwa mchezaji wa Netball nikiitumikia timu ya mkoa wangu wa Morogoro’Moro Stars kwenye michuano ya ‘Taifa Cup’ iliyofanyika Uwanja wa Gerezaji Jijini Dar es salaam, lakini mapenzi yangu makubwa yalikuwa kwenye mpira wa Miguu nikiishabikia timu ya Simba.

Nashukuru baadae nilifanikiwa kupata kadi ya uwanachama wa Simba, kama hiyo haitoshi uchaguzi Mkuu wa tawi hili la Simba uliofanyika Desemba 15-2019 nilichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji nakumbuka kwenye uchaguzi huo Shekidele ulikuwepo ukatupiga Picha na kuposti kwenye mtandao wako”alisema Veronica ambaye kabla ya tawi hilo la Simba kuhamia  ofisi za CCM Kata ya Mji Mpya.Ofisi za tawi hilo zilikuwa kwenye nyumba yao iliyopo jirani na ofisi hizo za CCM.

Mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo Bi Veronika alimkabidhi picha ya kikosi cha timu ya Netball ya Mkoa wa Morogoro cha mwaka 1980 ambapo alitaja majina ya wachezaji wenzake kwenye picha hapo juu.


 Leo viongozi wa matawi yote ya simba Mkoani Morogoro akiwemo Bi Veronika wanakikao cha dharura kitakachofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Front iliyopo Msamvu ambapo moja ya agenda za kikao hicho ni kujadili mwendo wa timu yao kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...