Na Dustan Shekidele,Morogoro.
STORI iliishia sehemu ambapo Fundi Umeme ametinga kwa Mganga na kupewa majibu ya tatizo lake na hatua za kuchukua kumnusuru mkewe pamoja na Mwanaye.
TUENDELEE SEHEMU YA 3.
Fundi huyo alifunga safari kutoka Morogoro Mpaka Manyara kufuata huduma ya Mganga huyo wa kienyeji alipofika alimsimulia matatizo yanayoikabiri familia yake.
Baada ya kumsikia mteja wake Mganga huyo alimuacha ofisini na kuzama kwenye chumba c Maalumu chenye vifaa vya Tiba asili kilichounganishwa Enternet ya kishirikina inayobaini mambo ya kichawi’ ‘Wich Dokta’ alirejea Ofisini akiwa na Majibu ya Fundi huyo na moja kwa moja alimsomea majibu hayo na hatua za kuchukua.
”Kijana unamatatizo Makubwa sana yanayosababishwa na familia ya mkeo, Majibu yangu yananionyesha mkeo ulisoma mambo ya dini, na mmoja wa bibi zake ni mshirikia hivyo kati ya wajukuu zake umemchagua huyu aliyesoma dini amlisishe mikoba hiyo ya uchawi ili amuasi Mungu.
Kama tunavyojua washirikina hawapendi mtu Mchamungu, kitendo cha mkeo kusoma dini kilimchukiza bibi huyo, kamua kumvuta kishirikina aishi naye pale nyumbani ili baadae amfundishe mambo hayo ya kishirikina”alisema Mganga huyo na kuongeza kudadavua.
“Mke na Mwanao wanamajeraha ambayo hayawezi kupona mpaka waondoke kwenye nyumba ya bibi huyo wakitoka tu ndani ya muda mfupi majeraha yao yatapona hivyo tatizo lako halihitaji nikupe dawa yoyote daya ninayokupa ni hiyo ya kuhakikisha unamtoa haraka mkeo na mwao pale kwa bibi yao.
Nakuomba usitumia nguvu wala hasira ya kugombana na huyo bibi utazidisha tatizo tumia hekima na busara za kuongea na mkeo aondoke pale, mpaka sasa mkeo hajui kama bibi yake huyo na mshirikina sasa naye utumie hekima kubwa kuongea naye juu ya jambo hilo”alimalizia kusema Mganga huyo.
Baada ya kureja Morogoro Fundi huyo alikuta hali nyingine tofauti kwa mwanaye ambaye licha ya jeraha lake la suna kuchelewa kupona, kiumbe huyo asiye na hatia amepata tatizo lingi la sikio kutoa usaha na harufu mbaya.
“Kama hiyo haitoshi Usiku licha ya baridi kali mwanangu pekee hatakia kulala na nguo wala kujifunika shuka, anataka kulala mtupu, na hataki kulala kwenye kitandani anataka kulala chini ya sakafu akiwa uchi wa mnyama mkimvisha nguo na kumlaza kitandani hamlali atalia usiku kucha”alisema Fundi huyo kwa sauti ya upole.
Siku iliyofuata Fundi huyo aliamua kumsimulia mkewe majibu ya Mganga je Mkewe ameayapokeaje majibu hayo, atakuwa upande wa Mume wake kuondoka hapo kwa bibi yake au atakuwa upande wa bibi yake aendelee kusalia hapo.?
Sehemu ya nne ya stori hii inamajibu ya maswali hayo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment