Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 27, 2023

UDAKUZI SPESHO. SEHEMU YA NNE MKE WA FUNDI UMEME ADAIWA KUTEKWA KIAINA NA BIBI YAKE.



 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

STORI  iliishia sehemu  Fundi Umeme kutinga kwa Mganga na kupewa majibu ya tatizo na hatua za kuchukua kumnusuru mkewe pamoja na Mwanae.

Je mke baada ya kupata taarifa hizo alizipokeaje? alikubali kumkana bibi yake na kuondoka hapo nyumbani akiambatana na mumewe au aliamua kuachana na mumewe na kusalia hapo  kwa bibi yake?

               TUENDELEE SEHEMU YA 4.

Wakati fundi huyo akitafakari jinsi ya kumueleza Mpendwa mkewe majibu kutoka kwa Mganga, ghafla kapokea simu kutoka kwa Mjomba mkubwa wa Mkewe ambaye ni dereva wa daladala Stend Mpya ya daladala ya Mafinga Manispaa ya Morogoro.

”Mjomba jitahidi mida ya saa 7 uje Stend Mafiga ninamazungumzo muhimu na wewe” Alipofika Mjomba’ke huyo  alijiripua na mumwambia kila kitu kinachoitesa familia yake.

”Mjomba sisi wanaume Mungu katupa koromero hili hapa shingoni la kuhifadhi vitu wenzetu wanawake hili hawana, hivyo nimeamua kukuita wewe mwanaume kukueleza mambo haya mazito.

Najua Mkeo na Mwanao wako pale kwa Mama yangu mzazi ambaye nyinyi ni bibi yenu, taarifa ni kwamba  mama sio mtu mzuri hivyo ukitaka mkeo na mwanao wapone majeraha yao waondoe pale kwa mama ambaye mambo yake anashirikiana na Mdogo wangu kwa maana ya mjomba wenu mdogo”alisema dereva huyo.

Kauli hiyo ilimpa nguvu  Fundi huyo kumueleza mkewe ambapo moja kwa moja alienda kwa mkewe na kumueleza majibu ya Mganga na maelezo aliyoambiwa na Mjomba wao. 

Baada ya kuelezwa taarifa hizo kwamba bibi yake ni mshirikina na mateso hayo anayoyapata yeye ni mwanae yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na na bibi yake.

Mke huyo baada ya kupokea taarifa hizo nzito alivuta punzi  kisha kaangua kilio na mumewe kubeba jukumu la kumbembeleza huku akiwa na shauku la kusubiri jibu kutoka kwa mkewe kama atakubari kuondoka au kusalia hapo kwa bibi yake.

Aliponyamaza mke katoa majibu haya.

” Vita hii sio yako peke yako Mume wangu ni yetu sote  hakuna mtu yoyote anayependa kuishi na mshirikini, hivyo kama mganga na mjomba wote wamekueleza uniondoe hapa niko tayari hata sasa hivi  kuondoka hapa na kuambatana nawe, natii na kuheshimu maelekezo yako  Mume wangu ambaye ni kichwa cha familia, 

kumbe anayetutesa mimi na mwanangu ni bibi yangu nayamini hayo maneno kwa kiwangu kikubwa kwani hapa nyumbani kuna chumba kimoja toka nifike hapa bibi hajakifungua huenda ndio kahifadhi mambo yake hayo”alisema mke huyo.

Baada ya majibu hayo ya mkewe fundi huyo naye kamueleza hivi.

” Asante mkewe wangu kwa kuungana nami kwenye vita hii awari nilihisi kwa muda mrefu uliokaa hapa bila sisi kujua kama bibi ni mshirikini  huenda dawa zimeshakukolea utanikana na kuungana na bibi yako.

Kama unavyojua mimi na wewe bado ni vijana wadogo wewe unaumri wa miaka 22 na mimi nina  miaka 28 tumekutana na mambo haya makubwa, awari niliwaeleza wazazi wangu kila kitu ikiwemo majibu ya Mganga na yale maelezo aliyonipa Mjomba.

Wakaniambia nikueleze wewe tujue utasimama  upande gani wa kwangu au wa bibi yako kwa hiyo baada ya majibu yako nimewapigia simu sasa hivi wameniambia kesho nipande gari niende fasta nyumbani Mtwara huku  ukiendelea kukaa hapa mpaka nitakaporudi baada ya siku 4”:alisema Fundi huyo.

Baada ya kikao kizito cha familia  huko Mtwara walimuita kijana wao kwa lengo la kujibu mapigo nini nimeamuliwa huko majibu ya kikao hicho yataruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...