Picha za ushahidi wa Udakuzi huu, baadhi ya vifaa vya fundi huyo mpaka sasa bado vipo Stoo nyumbani kwa Mdakuzi.
Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro.
MPENDWA Msomani wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, Stori yetu ya Udakuzi wa Mke wa Fundi Umeme kudaiwa kutekwa kiaina na bibi yake, tuliyoianza jana sehemu ya pili inaendelea leo hivyo bila kupoteza muda tuendele pale tulipoishia.
Jana tuliishie sehemu ya mke wa Fundi huyo baada ya kujifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji alikwenda kuuguza jeraha kwa bibi yake huyo Mzaa Mama kufuatia mama yake mzazi kufariki dunia. Bibi huyo anadaiwa kuwa mshirikia[Mchawi]
TUENDELEE SASA.
Madaktari walimueleza jereha hiyo litapona baada ya miezi 6 na kwamba kwa kipindi hicho hatakiwi kufanya kazi ngumu ikiwemo tendo la ndoa.
Chaajabu miezi 6 imefika jereha hilo halikupona amekaa miezi 6 mingine kwa maana ya mwaka mmoja bado jereha hilo ndio kwanza linazidi kuwa bichi, Mtoto wao alipotimiza mwaka mmoja bibi yao aliwashauri wamwingize suna.
Kwa Mujibu wa ngaliba aliyemtahiri aliwaeleza ndani ya wiki 3 mpaka 4 jeraha la mtoto huyo litapona kabisa.
Chaajabu mpaka sasa ni zaidi ya mwaka mmoja jereha la mtoto huyo nalo halijapona.
Kwa mijibu wa Fundi huyo hata upatikanaji wake wa riziki kwa sasa umeshuka sana tofauti na awari kabla mkewe hajajifungua.
Nakumbuka Mwaka jana Fundi huyo alikuwa akifanya kazi ya ‘Wayaring’ kwenye moja ya Frem za Maduka pale nyumbani, akiwa juu ya paa alipigiwa simu akihitajika fasta Kilosa kwenye Enterview kampuni inayojenga Reli ya Mwendokasi.
Aliacha vifaa vyake vya kazi kwenye stoo yangu nikampa ruhusa kaenda Msamvu kapanda gari kaelekea Kilosa, baada ya siku 3 kanipigia simu kanieleza kwamba amefanikiwa kupata kazi kwenye kampuni hiyo na Mshahara wake ni Mnono.
Chakushangaza amedai aliporipoti kazini amefanya kazi siku 3 baadae kaondolewa kazini, hali hiyo ya Majeraha ya sio pona ya mkewe pamoja na mwanaye sambamba na hali ya kukosa kazi zilipelekea fundi huyo muda wote kuwa na dimbwi la mawazo.
Hivi karibuni Fundi huyo alimtafuta Mwandishi wa Mtandao huu na kumueleza
”Kuna boss wangu huwa namfanyia kazi kwenye nyumba yake yeye ni dereva wa mabasi[anataja jina la kampuni hiyo ya mabasi] ni mtu wangu wa karibu kama ulivyo wewe na matatizo yangu anayajua, hivyo baada ya kuniona hali yangu inazidi kuwa mbaya huku nikizidi kukonda kwa mawazo.
Kanipa nauli lakini moja niende Manyaka kwa mtaalamu[Mganga] akaangalie kwa nini majeraha ya mke wangu na mwanangu hayaponi”alisema Fundi huyo na kubeba begi lake akielekea Stend ya mabasi Msamvu tayari kwa safari ya Manyara kuonana na mganga huyo aliyeunganishiwa na dereva huyo.
Baada ya siku 3 Fundi huyo alireja Morogoro na moja kwa moja alimtafuta Mwandishi wa Mtandao huu na kumueleza A-Z alichoambaiwa na Mganga huyo.
Nini ameambiwa endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kufuatilia Udakuzi huu Mtamu.
No comments:
Post a Comment