Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, November 28, 2023

UDAKUZI SPESHO. SEHEMU YA TANO MKE WA FUNDI UMEME ADAIWA KUTEKWA KIAINA NA BIBI YAKE.




 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

STORI iliishia  Fundi  Umeme kutii wito wa wazazi kijijini kwao Mkoani Mtwara kwa lengo la kujibu mashambulizi ya bibi wa mkewe anayedaiwa kumteka Mjukuu wake kwa Imani za kishirikina.

Fundi huyo baada ya kutinga kijiji kwao nini kilifanyika, twende pamoja sehemu ya tano na ya Mwisho ya stori hii ya tamu tamu.

               TUENDELEE SEHEMU YA 5.

 Fundi huyo aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa na Wazazi wake wanaoishi  Mtwara kwenye moja ya Vijiji vilivyopo  mpakani mwa nchini za Tanzania na Msumbiji.

 Alipowasili kikao cha familia kilicho jumuhisha  Wazee  Maarufu wa kijiji hicho akiwemo Mganga maarufu kijijini hapo ambaye ni kiboko cha wachawi.

Fundi huyo ‘Chinga Og’ alipewa nafasi ya kukieleza kikao hicho A-Z Matatizo yanayoikuta familiya yake na hatua alizochukua kukabilia na changamoto hizo.  

Wajumbe wa kikao hicho baada ya kusikia Madai hayo mazito, Wazee hao wa Kimakonde walivuta punzi kisha Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni baba wa fundi huyo alisimama huku akiwa na Jazba kwa mateso wanayofanyiwa wanaye pamoja na Mjukuu wake, akamsimamisha Mzee huyo Mganga kiboko cha Wachawi Kijijini hapo akimtaka kujibu mapigo kwa bibi huyo mtesi wawanae na mjuu wake.

Mganga huyo aliposimama alimuamulu Fundi huyo kumtajia majina matatu ya bibi huyo, baada ya kutajiwa majina hayo alitoka nje ya kikao na baada ya dakika 20 alirejea na kusema.

“Nimeangalia kweli bibi huyo nitatizo, nipeni maelekezo mnataka nimfanyeje nimuondoe hapa duniani kwa maana ya kumfanya Mzukule, au nimpelekee kombora na kumfanya awe chizi aokote makopo jalalani?”aliuliza Mganga huyo huku akiwa ana Usinga mkononi.

Baba wa Fundi walitoa jibu hili” lli tumdharirishe na iwe fundisho kwa wengine Mpelekee hilo kombora la kuwa chizi.” alisema

 

Wakati Mganga huyo akijiandaa kutoka nje na kutuma kombora hilo.

Fundi huyo alisimama na kupinga vikali kauli hiyo ya baba yake”Mimi nimesoma dini nina hofu ya Mungu hivyo sihitaji Mganga huyu kufanya chochote  sikujua kama  baba ulialika Mganga” alisema Fundi huyo.

Maneno hayo yalionekana kumkera Mganga huyo ambaye kwa hasira akibeba mkoba wake na kuondoka bila kuaga.

Baada ya malumbano ya takribani dakika 20 kikao kiliendelea kwa baba ya Fundi huyo kumuliza Mwanae anataka kifanyike nini baada ya kukataa huduma ya Mganga?.

Fundi kajibu. “ Mafundisho ya dini niliyosoma yanazuia kulipiza ubaya kwa aliyekufanyia ubaya.

Hivyo kwenye tatizo langu nahitaji kumshitakia Mwenyezimungu hivyo naomba kikao hiki kinitafutie Shehe anisomee aya hiyo ya kumshitakia Mungu ‘Ahlul-Badri’.

 Maneno hayo ya hekima yaliwagusa wazee wote walikuwepo kwenye kikao hicho na kwa kauli moja wote wameunga mkoni maneno hayo na wamekubaliana siku inayofuata waende kwa shehe.

 Fundi huyo alikieleza kikao kwamba aya hiyo inahitaji kusomwa na shehe Msafi kiroho na kimwili, kwa vile Mtwara Mjini ni mbali waliamua kupanda boda boda kutoka hapo kijijini mpaka baharini nauli ya boda ni elfu 2 tu.

Wakapanda Bodi mpaka Msumbiji nauli elfu 5 wakampata shehe baada ya kumueleza mkasa mzima kawapa masharti haya.

”Niwapongeze kwa uamuzi huu mzuri wa kupeleka malalamiko yenu kwa Mwenyezi Mungu huyu kijana mdogo kakutana na mambo makubwa mngeweza kumshauri vibaya kwenda kujibu mapigo kwa waganga wa kienyeji”alisema Shehe huyo na kuongeza,

“ Kwa leo siwezi kusoma aya hiyo mpaka huyu kijana aende kwenye familia hiyo ya kishirikia akawambie maneno haya.

Waache ushirikina ndani ya siku 21 kwa maana ya wiki 3, watupe tunguliza zao na wawaopoe watu wote waliowaroga kishirikina, wakitekeleza hayo ndani ya muda huo basi huna haja tena ya kumshitakia mwenyezimungu, la wakikaidia ndani ya muda huo uje sasa tusome aya hiyo  na Mwenyezimungu Mwingi wa Rehema atajibu maombi yako na yakijibiwa  adui  zako wote wataangamia na wale waliowatesa wote watapona”alisema Shehe huyo.

Wiki iliyopita fundi huyo karejea Morogoro na Moja kwa moja katinga nyumbani kwa wake zake na kuitisha  kikao cha familya kilichohudhuriwa pia na bibi huyo kinara wa tuhuma hizo.

 Katoa siku 21 [wiki tatu] kwa watu wote wanaomtesa mkewe na mwanae kuacha jambo  hilo ikiwemo kuchoma moto tunguli zao baada ya muda huo kufika  anakusudia kusoma aya ya kumshitakia Mwenyezimungu ‘AHLUL-BADRI’.

Katika hali ya kushangaza  mtoto wa kiume wa bibi huyo anayedaiwa kushirikiana na mama yake kwenye mambo hayo ya kishirikina,kamjia juu Fundi huyo akidai anaidharirisha familia hiyo yao kw akuwaita wachawi hivyo atakwenda Polisi kumshitaki.

Fundi huyo naye hakuwa Mjonyonge kamjibu

”Wewe Mjomba ndio unashirikiana na mama yako kumtesa mkewe wangu na Mwanangu hivi kwa kufanya haya mnapata faida gani?nenda polisi sasa hivi kama huna nauli nikupe ili uwahi kufika” baada ya maneno hayo kikao kilivunjika Fundi kamchukua mkewe na Mwanae wamekusanya kila kilicho chao na kurejea  nyumbani kwao Kasanga.

Baada  ya muda baadhi ya wanafamilia hiyo wanaochukizwa na vitendo hivyo wa kishirikina  walimpigia simu Fundi huyo wakimpongeza kwa ujasili aliouonyesha  huku wakimuahidi kuwa pamoja naye huku wakimkana bibi yao huyo ‘

               

Stori hii ya kidakuzi inaishia hapa ngoja tusubiri hizo wiki tatu nini kitatokea,Mdakuzi juzi alifanya Udakuzi wa kumpigia simu Fundi huyo alimuliza kama kweli Mjomba’ke alienda Polisi, alijibu.

”Hawezi kwenda Polisi wanatapatapa baada ya siri yao kufichukia wanatafuta kichaka cha kujificha, we subiri wiki siku 21 zitimie nitakupa mrejesho utoe habari kamili”alisema Fundi huyo

                       MWISHO.

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...