Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 22, 2023

UDAKUZ SPESHO. IMANI ZA KISHIRIKINA. MKE WA MFUNDI UMEME ATEKWA KIAINA NA BIBI YAKE.

Baada ya vifaa vya Umeme vya fundi huyo vikiwa stoo nyumbani kwa Mdakuzi.

 


Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro. 

UKISTAAJABU ya Mussa, hutayaona ya Filahuni, Msemo huo umetimika baada ya Mke wa Fundi Maarufu wa Umeme wa Majumbani Mkoa wa Morogoro[Jina kapuni kwa sababuzi za kiudakuzi]  anaishi peke yake zaidi ya Miaka Miwili baada ya mkewe Kipenzi kutekwa kiaina na bibi yake anayedaiwa kujihusisha na mambo ya kishirikina.

Picha hilo  liko hivi, takribani miaka 6 iliyopita fundi huyo ambaye pia ni fundi Mkuu wa maswala ya Umeme nyumbani kwa Mwandishi wa Mtandao huu alimpa taarifa Mdakuzi akisema.

“Kaka mbali na kufanya kazi za umeme nyumbani kwako nimekuona ni mtu mwenye hekima na busara hivyo nimeona nikushirikishe kwenye mambo yangu ya kifamilia, nataka kuoa na tayari nimeshapata mchumba, kama unavyojua mimi ni Mtu wa dini nimeamua kabla ya kuoa  nimsomeshe Elimu ya Ahera kwani tayari wazazi wake wameshamsomesha Elimu ya dunia kahitimu kidato cha 4.

Hivyo nimempeleka Madrasa akihitimu mafunzo hayo ya Mwenyezi Mungu tunafunga ndoa”alisema fundi huyo aliyepata Elimu  hiyo ya Ufundi wa Umeme Chuo Cha VETA.

Baada ya Mchumb’ake huyo kuhitimu mafundisho hayo ya dini ‘wamechoma ubani’ wamefunga ndoa na Mpiga Picha wa harusi hiyo iliyofana alikuwa Mpiga Picha Mashuhuri wa Mtandao huu anayemili Kamera za Kisasa zenye ‘Photo Shoot’ ndani yake.

 

Baada ya Mwaka mmoja ndoa imejibu kwa maana wamejaliwa kupata Mtoto wa kiume huku mkewe  akijifungua kwa njia ya Upasuaji’Uparesheni’.

Kwa sababu mama mzazi wa mke wa fundi huyo alishafariki dunia hivyo aliamua kwenda kuugulia jeraha hilo kwa bibi yake mzaa mama kwa ruhusa ya mumewe bila kujua kama bibi yao huyo ni mshirikina.

Nini kiliendelea huko udakuzi huu nutaendelea baadae hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu Muda wote.

                        


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...