Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, November 5, 2023

RIPOTI YA C.A.G WABUNGE WA CHARUKA.


 Mama huyo wa kijiji cha Dakawa kilichopo kando kando ya barabara Kuu ya Morogoro-Dodoma alinaswa na Mwandishi wa habari hizi akichota maji ya Mvua kwenye toppe zito baada ya kijiji hicho kukosa Maji.

 

 MITHARI  28. 2-7

“Kwa sababu ya Maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi,bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa.

Mtu mhitaji awaoneaye masikini, nikama mvua ya dhoruba isiyosaza Chakula.

Wao waiachayo sheria huwasifu waovu, bali wao waishikao hushindana nao.

Watu wabaya hawaelewi na ukumu, bali wamfuatao bwana huelewa na yote.

Afadhari masikini aendaye katika unyofu wake,kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.

Yeye ashikaye sheria ni Mwana mwenye hekima. bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye” Hili ndilo neno letu la Leo Jumapili ya Novemba 5.

                      UCHAMBUZI.

Kama kawaida kila Jumapili Mtumishi wa Mungu, Mwandishi wa Mtandao huu huweka kando habari zote na kusoma neno la Mungu kwenye Biblia kisha kulichambua kwa ufupi.

Leo nilipofungua Biblia nimekutana na neno  la Mungu kutoka Mithari 28.2-7.nilipolisoma  nimebaini linaendana na tukio la sasa linalotikisa bunge letu.

Toka juzi wawakilishi wawananchi bungeni wanajadili ripoti ya Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa hesabu za Serikari’CAG’iliyobaini wizi wa mabilio ya fedha za Serikali ambazo ni kodi za wananchi wengi wao wakiwa wanyonge.

 Inauma sana wakati kuna baadhi ya wananchi Vijijini wanajifungua njiani na baadhi ya kupoteza maisha baada ya kijiji  kukosa Zahanati, kwenye ripoti ya CAG unasikia Kigogo mmoja wa Serikali katajwa kwenye ripoti ya CAG kaiba Mabilio ya fedha

Baadhi ya wabunge akiwemo dada yangu kipenzi Esther Bulaya niliyefanya naye kazi ya Uandishi wa habari hapa Morogoro  nilimshuhudia akiwashukia vikali mafisadi hao walioiba Pesa  za wananchi na kwa lengo la kujitajirisha wao binafsi.

Mjadara huo wa  kujadiri ripoti hiyo ya CAG utaendelea kesho Jumatatu kwenye Bunge letu Pendwa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  hivyo Mapema sana nitanjongea kwenye Tv kuwasikiliza kwa umakini wabunge wanaotete pesa za wananchi wanyonge na wale wabunge wanaowatetea Mafisadi walioiba Pesa za wanyonge.

Shekidele sina hatia siku zote ni mtetezi wawanyonge na kwenye tukio hilo naingia kwenye kapu la wabunge wanaotetea Pesa za wanyonge.

                              


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...