Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, November 3, 2023

UKURASA WA HABARA. KUNA UVUMILIVU WA KUFANYWA MJINGA KWENYE MAPENZI.


Mwandishi wa Makalla hii akipima Afya Sambamba na kuchangia damu kwenye Bank ya damu Mkoa wa Morogoro.

 




 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MPENDWA Msomaji wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, baada ya ukimya wa siku kadhaa hatimaye Leo tunarejea kwenye ukurasa wetu Pendwa wa somo la Mahusiano ya Kimapenzi’Mahaba’.

Somo la leo  tutazungumzia uvumilivu kwenye Mahusiano ya Kimapenzi, ni kweli Wazazi,  Marafiki na Viongozi wa dini wanapofungisha ndoa wanatuhasa tuvumiliane kwenye shida na raha, naungana na makundi  hayo kwenye lshu hiyo ya kuvumiliana.

Kwa sababu hapa chini ya jua hakuna mtu mkamilifu tumeumbwa kukosea na kusahau, hivyo mwenzi wako anapokosea unamrekebisha na anaposahu jambo unamkumbusha, usimfokee au kugombana naye kwa sababu amekosea au kusahau.

 Kumbuka Mkamilifu ni Mwenyezi Mungu Pekee lakini Paka, Kenge, Mbwa, na binadamu wote tunamapungufu, hivyo tunapaswa kubebeana Misalaba kwenye mapungufu yetu tuvumiliane.

Kuna baadhi ya wanandoa, Wachumba au Wapenzi hujificha kwenye kichaka hicho cha uvumilivu kuwatesa wenzi wao wakiwafanya Wajinga wanapowavumilia hii sio sawa kumbuka huyo ni binadamu hana moyo wa chuma ana moyo wa nyama unaobena maumivu kumbuka uvumilivu unakikomo.

 Mfano Mpenzi wako umemtoa kwenye ndimbwi la tope’umejitosa bila kujali maneno ya ndugu na Jamaa umemnasua kwenye tope kwa kuweka gia ya tope ‘Four Wheel Drive’ baada ya kunnasua umemsafisha jizo tope kawa msafi umamvuta ndani mkaishi kama  mke na Mume.

Hapa sijui naeleweka vizuri au nifunguke zaidi, Any Way ili twenda sawa ngoja nifunguke, mfano mke umemtoa kwenye madanguro anajiuza au umemkuta anafanya kazi ya ubaa medi umezungumza naye anakueleza kwamba anafanya hivyo si kwa utashi wake bali ni shida.

Hivyo unaamua kujitosa kumvua kimini chake cha ‘kudanga’ unatinga Kariakoo kwa Mpemba unamnunulia dera la bei mbaya kisha unamvuta ndani baada ya muda unafunga naye ndoa huku ukiziba masikio  kukwepa  meneno  ya ndugu na jamaa juu ya uamuzi wako huu wa kuona chagudoa.

 Au umemkuta Mwanamke kaiba mume wa mtu kapangiwa chumba akimtegema mume huyo wa mtu kwa asilimia mia moja, akidhurumu haki ya mwanamke mwenzie akidhurumu wa toto wa huyo mwanaume kwa kulipiwa chumba na kupewa pesa ya kula kila siku, huku familia ya huyo mwanaume ikitaabika kwa maisha magumu.

Unajitoka unamtoa mwanamke huyo kwenye tope hilo la dhambi ya kuiba mume wa mtu unamsafisha dhambia hiyo unafunga naye ndoa baada ya mwana analudi tena kwenye tabia ya kuiba waume za watu, hapo sasa unavumilia nini zaidi ya kumpiga chini aludi kwenye maisha aliyozoea ya kuiba waume za watu huku yake ataipata kesho kwa MUNGU.

Mwenye asili achia asili yake tabia ni kama ngozi utaipaka mgorogo unakuwa ‘Mzungu’Mwisho wa siku Mkorogo ukikata itarejea kwenye uhalisi wake ‘Black People’, Mwanamke huyo huyo uliyemsafisha tope Mwisho wa siku anafanya matendo ya kukupaka wewe yale Matope uliyomsafisha, akikusaliti kwa kuchepuka nje ya ndoa ukimuliza anakuwa mkali kama pilipiki kichaa huku akikutupia maneno ya ‘shombo’.

Hapo hakuna tena uvumilivu bali amekufanya Mjinga kwa kumtoa kwenye tope, ninalolisema kwa baadhi ya  wanawake nalisema pia kwa baadhi ya wanaume.

 Mwanamke umemuoa kwa wazazi wake akiwa na afya njema ana kula Vizuri ana lala Pazuri anavaa vizuri.

Kaja kwako akitimiza agizo la Mwenyezi Mungu kwamba ndoa ni lbada, kaacha vyote hivyo kwao kaja kuishi na wewe mwenye maisha ya chini kipato chako ni unga unga Mwana mpaka utoke ndio jioni mle.

Lakini bint wawatu aliyelelewa kwenye misingi ya dini  kakuvumilia mmeshirikiana kimawazo mkapambana Mungu kawajari mmetoboa kimaisha, Mmejenga nyumba, zamani mlikuwa ukitembelea usafiri wa Mwenyezi Mungu wa namba 11[Miguu 2] sasa mnatembelea Makalio[Mnatembea huku mmekaa kwenye Gari].

Baada ya mafaniko hayo Mwanaume unadadilika unalala baa unarejea nyumbani asubuhi, mkeo akiuliza unamfokea unadai ulikuwa kazini akizidi kukuhoji unamtamkia maneno ya Machafu kwamba  hamuendani  sasa hivi unapesa unahitaji kutafuta Mwanamke Mrembo wa kufanana na Pesa zake.

Hapo Mke hawezi kuvumilia na kama akiendelea kuvumilia basi ataingia  kwenye ulevumilivu wakufanywa Mjinga.

 Ulitii maagizo ya wazazi na Viongozi wa dini kwamba umvumilie mume wako kweli umemvumilia kwenye shida leo mmefanikiwa anakuludia asubuhi ili hali awari alipokuwa hana kitu saa 12 jioni kareja nyumbani akiketi na familia yake.

Mwaka jana nilisikia kwenye vyombo vya habari kwamba taasisi moja imefanya utafiti kwenye mmoja ya jiji kwa mwenzi talaka mia tatu zinatolewa, kwa maana ndoa mia tatu zinavunjika.

Utafiri huo Unathibitisha usaliti Umeongezeka kwa kasi  mkubwa wanandoa wanaamua kuvunja ndoa wakikwepa ule uvumiliwa wa kufanywa Mjinga.

Namalizi hadithi yangu kwa kuwakumbusha watanzania wenzangu UKIMWI Upo tusijisahaulishe, starehe ya dakika 10 isije akakupeleka Muhimbili na uzito wa kilo 10 ili hali ulikuwa na afya njema ya kilo zaidi ya 60.

 Tubaki njia Kuu Michepuko sio dili mwenye masikio na asikie asiye na Masikio kanyaga twende Makabuli ya Kolla Morogoro bado nafasi zipo.

Kwa leo naishi hapa Mungu akipenda tukutane wiki ijayo,kwa ushauri na maoni wasiliana nami kwa Whatspp no 0715 28 90 73.

                      


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...