Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 29, 2023

DALILI TATU ZA MTU MNAFIKI

  shekidele Mkude Simba Miwani kama fund' Werding' akimtafakari Mnafiki.
 

TAFAKARI.
Tabia.tatu za Mtu Mnafiki.
Mosi- Muongo.
Pili- Akiahidi kitu Hatekerezi.
Tatu- Akiaminiwa Haminiki.


Tuesday, November 28, 2023

UDAKUZI SPESHO. SEHEMU YA TANO MKE WA FUNDI UMEME ADAIWA KUTEKWA KIAINA NA BIBI YAKE.




 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

STORI iliishia  Fundi  Umeme kutii wito wa wazazi kijijini kwao Mkoani Mtwara kwa lengo la kujibu mashambulizi ya bibi wa mkewe anayedaiwa kumteka Mjukuu wake kwa Imani za kishirikina.

Fundi huyo baada ya kutinga kijiji kwao nini kilifanyika, twende pamoja sehemu ya tano na ya Mwisho ya stori hii ya tamu tamu.

               TUENDELEE SEHEMU YA 5.

 Fundi huyo aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa na Wazazi wake wanaoishi  Mtwara kwenye moja ya Vijiji vilivyopo  mpakani mwa nchini za Tanzania na Msumbiji.

 Alipowasili kikao cha familia kilicho jumuhisha  Wazee  Maarufu wa kijiji hicho akiwemo Mganga maarufu kijijini hapo ambaye ni kiboko cha wachawi.

Fundi huyo ‘Chinga Og’ alipewa nafasi ya kukieleza kikao hicho A-Z Matatizo yanayoikuta familiya yake na hatua alizochukua kukabilia na changamoto hizo.  

Wajumbe wa kikao hicho baada ya kusikia Madai hayo mazito, Wazee hao wa Kimakonde walivuta punzi kisha Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni baba wa fundi huyo alisimama huku akiwa na Jazba kwa mateso wanayofanyiwa wanaye pamoja na Mjukuu wake, akamsimamisha Mzee huyo Mganga kiboko cha Wachawi Kijijini hapo akimtaka kujibu mapigo kwa bibi huyo mtesi wawanae na mjuu wake.

Mganga huyo aliposimama alimuamulu Fundi huyo kumtajia majina matatu ya bibi huyo, baada ya kutajiwa majina hayo alitoka nje ya kikao na baada ya dakika 20 alirejea na kusema.

“Nimeangalia kweli bibi huyo nitatizo, nipeni maelekezo mnataka nimfanyeje nimuondoe hapa duniani kwa maana ya kumfanya Mzukule, au nimpelekee kombora na kumfanya awe chizi aokote makopo jalalani?”aliuliza Mganga huyo huku akiwa ana Usinga mkononi.

Baba wa Fundi walitoa jibu hili” lli tumdharirishe na iwe fundisho kwa wengine Mpelekee hilo kombora la kuwa chizi.” alisema

 

Wakati Mganga huyo akijiandaa kutoka nje na kutuma kombora hilo.

Fundi huyo alisimama na kupinga vikali kauli hiyo ya baba yake”Mimi nimesoma dini nina hofu ya Mungu hivyo sihitaji Mganga huyu kufanya chochote  sikujua kama  baba ulialika Mganga” alisema Fundi huyo.

Maneno hayo yalionekana kumkera Mganga huyo ambaye kwa hasira akibeba mkoba wake na kuondoka bila kuaga.

Baada ya malumbano ya takribani dakika 20 kikao kiliendelea kwa baba ya Fundi huyo kumuliza Mwanae anataka kifanyike nini baada ya kukataa huduma ya Mganga?.

Fundi kajibu. “ Mafundisho ya dini niliyosoma yanazuia kulipiza ubaya kwa aliyekufanyia ubaya.

Hivyo kwenye tatizo langu nahitaji kumshitakia Mwenyezimungu hivyo naomba kikao hiki kinitafutie Shehe anisomee aya hiyo ya kumshitakia Mungu ‘Ahlul-Badri’.

 Maneno hayo ya hekima yaliwagusa wazee wote walikuwepo kwenye kikao hicho na kwa kauli moja wote wameunga mkoni maneno hayo na wamekubaliana siku inayofuata waende kwa shehe.

 Fundi huyo alikieleza kikao kwamba aya hiyo inahitaji kusomwa na shehe Msafi kiroho na kimwili, kwa vile Mtwara Mjini ni mbali waliamua kupanda boda boda kutoka hapo kijijini mpaka baharini nauli ya boda ni elfu 2 tu.

Wakapanda Bodi mpaka Msumbiji nauli elfu 5 wakampata shehe baada ya kumueleza mkasa mzima kawapa masharti haya.

”Niwapongeze kwa uamuzi huu mzuri wa kupeleka malalamiko yenu kwa Mwenyezi Mungu huyu kijana mdogo kakutana na mambo makubwa mngeweza kumshauri vibaya kwenda kujibu mapigo kwa waganga wa kienyeji”alisema Shehe huyo na kuongeza,

“ Kwa leo siwezi kusoma aya hiyo mpaka huyu kijana aende kwenye familia hiyo ya kishirikia akawambie maneno haya.

Waache ushirikina ndani ya siku 21 kwa maana ya wiki 3, watupe tunguliza zao na wawaopoe watu wote waliowaroga kishirikina, wakitekeleza hayo ndani ya muda huo basi huna haja tena ya kumshitakia mwenyezimungu, la wakikaidia ndani ya muda huo uje sasa tusome aya hiyo  na Mwenyezimungu Mwingi wa Rehema atajibu maombi yako na yakijibiwa  adui  zako wote wataangamia na wale waliowatesa wote watapona”alisema Shehe huyo.

Wiki iliyopita fundi huyo karejea Morogoro na Moja kwa moja katinga nyumbani kwa wake zake na kuitisha  kikao cha familya kilichohudhuriwa pia na bibi huyo kinara wa tuhuma hizo.

 Katoa siku 21 [wiki tatu] kwa watu wote wanaomtesa mkewe na mwanae kuacha jambo  hilo ikiwemo kuchoma moto tunguli zao baada ya muda huo kufika  anakusudia kusoma aya ya kumshitakia Mwenyezimungu ‘AHLUL-BADRI’.

Katika hali ya kushangaza  mtoto wa kiume wa bibi huyo anayedaiwa kushirikiana na mama yake kwenye mambo hayo ya kishirikina,kamjia juu Fundi huyo akidai anaidharirisha familia hiyo yao kw akuwaita wachawi hivyo atakwenda Polisi kumshitaki.

Fundi huyo naye hakuwa Mjonyonge kamjibu

”Wewe Mjomba ndio unashirikiana na mama yako kumtesa mkewe wangu na Mwanangu hivi kwa kufanya haya mnapata faida gani?nenda polisi sasa hivi kama huna nauli nikupe ili uwahi kufika” baada ya maneno hayo kikao kilivunjika Fundi kamchukua mkewe na Mwanae wamekusanya kila kilicho chao na kurejea  nyumbani kwao Kasanga.

Baada  ya muda baadhi ya wanafamilia hiyo wanaochukizwa na vitendo hivyo wa kishirikina  walimpigia simu Fundi huyo wakimpongeza kwa ujasili aliouonyesha  huku wakimuahidi kuwa pamoja naye huku wakimkana bibi yao huyo ‘

               

Stori hii ya kidakuzi inaishia hapa ngoja tusubiri hizo wiki tatu nini kitatokea,Mdakuzi juzi alifanya Udakuzi wa kumpigia simu Fundi huyo alimuliza kama kweli Mjomba’ke alienda Polisi, alijibu.

”Hawezi kwenda Polisi wanatapatapa baada ya siri yao kufichukia wanatafuta kichaka cha kujificha, we subiri wiki siku 21 zitimie nitakupa mrejesho utoe habari kamili”alisema Fundi huyo

                       MWISHO.

 

 

Monday, November 27, 2023

UDAKUZI SPESHO. SEHEMU YA NNE MKE WA FUNDI UMEME ADAIWA KUTEKWA KIAINA NA BIBI YAKE.



 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

STORI  iliishia sehemu  Fundi Umeme kutinga kwa Mganga na kupewa majibu ya tatizo na hatua za kuchukua kumnusuru mkewe pamoja na Mwanae.

Je mke baada ya kupata taarifa hizo alizipokeaje? alikubali kumkana bibi yake na kuondoka hapo nyumbani akiambatana na mumewe au aliamua kuachana na mumewe na kusalia hapo  kwa bibi yake?

               TUENDELEE SEHEMU YA 4.

Wakati fundi huyo akitafakari jinsi ya kumueleza Mpendwa mkewe majibu kutoka kwa Mganga, ghafla kapokea simu kutoka kwa Mjomba mkubwa wa Mkewe ambaye ni dereva wa daladala Stend Mpya ya daladala ya Mafinga Manispaa ya Morogoro.

”Mjomba jitahidi mida ya saa 7 uje Stend Mafiga ninamazungumzo muhimu na wewe” Alipofika Mjomba’ke huyo  alijiripua na mumwambia kila kitu kinachoitesa familia yake.

”Mjomba sisi wanaume Mungu katupa koromero hili hapa shingoni la kuhifadhi vitu wenzetu wanawake hili hawana, hivyo nimeamua kukuita wewe mwanaume kukueleza mambo haya mazito.

Najua Mkeo na Mwanao wako pale kwa Mama yangu mzazi ambaye nyinyi ni bibi yenu, taarifa ni kwamba  mama sio mtu mzuri hivyo ukitaka mkeo na mwanao wapone majeraha yao waondoe pale kwa mama ambaye mambo yake anashirikiana na Mdogo wangu kwa maana ya mjomba wenu mdogo”alisema dereva huyo.

Kauli hiyo ilimpa nguvu  Fundi huyo kumueleza mkewe ambapo moja kwa moja alienda kwa mkewe na kumueleza majibu ya Mganga na maelezo aliyoambiwa na Mjomba wao. 

Baada ya kuelezwa taarifa hizo kwamba bibi yake ni mshirikina na mateso hayo anayoyapata yeye ni mwanae yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na na bibi yake.

Mke huyo baada ya kupokea taarifa hizo nzito alivuta punzi  kisha kaangua kilio na mumewe kubeba jukumu la kumbembeleza huku akiwa na shauku la kusubiri jibu kutoka kwa mkewe kama atakubari kuondoka au kusalia hapo kwa bibi yake.

Aliponyamaza mke katoa majibu haya.

” Vita hii sio yako peke yako Mume wangu ni yetu sote  hakuna mtu yoyote anayependa kuishi na mshirikini, hivyo kama mganga na mjomba wote wamekueleza uniondoe hapa niko tayari hata sasa hivi  kuondoka hapa na kuambatana nawe, natii na kuheshimu maelekezo yako  Mume wangu ambaye ni kichwa cha familia, 

kumbe anayetutesa mimi na mwanangu ni bibi yangu nayamini hayo maneno kwa kiwangu kikubwa kwani hapa nyumbani kuna chumba kimoja toka nifike hapa bibi hajakifungua huenda ndio kahifadhi mambo yake hayo”alisema mke huyo.

Baada ya majibu hayo ya mkewe fundi huyo naye kamueleza hivi.

” Asante mkewe wangu kwa kuungana nami kwenye vita hii awari nilihisi kwa muda mrefu uliokaa hapa bila sisi kujua kama bibi ni mshirikini  huenda dawa zimeshakukolea utanikana na kuungana na bibi yako.

Kama unavyojua mimi na wewe bado ni vijana wadogo wewe unaumri wa miaka 22 na mimi nina  miaka 28 tumekutana na mambo haya makubwa, awari niliwaeleza wazazi wangu kila kitu ikiwemo majibu ya Mganga na yale maelezo aliyonipa Mjomba.

Wakaniambia nikueleze wewe tujue utasimama  upande gani wa kwangu au wa bibi yako kwa hiyo baada ya majibu yako nimewapigia simu sasa hivi wameniambia kesho nipande gari niende fasta nyumbani Mtwara huku  ukiendelea kukaa hapa mpaka nitakaporudi baada ya siku 4”:alisema Fundi huyo.

Baada ya kikao kizito cha familia  huko Mtwara walimuita kijana wao kwa lengo la kujibu mapigo nini nimeamuliwa huko majibu ya kikao hicho yataruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

 

Friday, November 24, 2023

UDAKUZI SPESHO. SEHEMU YA TATU MKE WA FUNDI UMEME ADAIWA KUTEKWA KIAINA NA BIBI YAKE.




 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

STORI iliishia sehemu ambapo Fundi Umeme ametinga kwa Mganga na kupewa majibu ya tatizo lake na hatua za kuchukua kumnusuru mkewe pamoja na Mwanaye.

               TUENDELEE SEHEMU YA 3.

 Fundi huyo alifunga safari kutoka Morogoro Mpaka Manyara kufuata huduma ya Mganga huyo wa kienyeji alipofika alimsimulia matatizo yanayoikabiri familia yake.

 Baada ya kumsikia mteja wake  Mganga huyo alimuacha ofisini  na kuzama kwenye chumba c Maalumu chenye vifaa vya Tiba asili kilichounganishwa Enternet ya kishirikina inayobaini mambo ya kichawi’ ‘Wich Dokta’ alirejea Ofisini akiwa na Majibu ya Fundi huyo na moja kwa moja alimsomea majibu hayo na hatua za kuchukua.

”Kijana unamatatizo Makubwa sana yanayosababishwa na familia ya mkeo, Majibu yangu yananionyesha mkeo ulisoma mambo ya dini, na mmoja wa bibi zake ni mshirikia hivyo kati ya wajukuu zake  umemchagua huyu aliyesoma dini amlisishe mikoba hiyo ya uchawi ili amuasi Mungu.

Kama tunavyojua washirikina hawapendi mtu Mchamungu, kitendo cha mkeo kusoma dini kilimchukiza bibi huyo, kamua kumvuta kishirikina aishi naye pale nyumbani ili baadae amfundishe mambo hayo ya kishirikina”alisema Mganga  huyo na kuongeza kudadavua.

 

“Mke na Mwanao wanamajeraha ambayo hayawezi kupona mpaka waondoke kwenye nyumba ya bibi huyo wakitoka tu ndani ya muda mfupi majeraha yao yatapona hivyo tatizo lako halihitaji nikupe dawa yoyote daya ninayokupa ni hiyo ya kuhakikisha unamtoa haraka mkeo na mwao pale kwa bibi yao.

Nakuomba usitumia nguvu wala hasira ya kugombana na huyo bibi utazidisha tatizo tumia hekima na busara za kuongea na mkeo aondoke pale, mpaka sasa mkeo hajui kama bibi yake huyo na mshirikina sasa naye utumie hekima kubwa kuongea naye juu ya jambo hilo”alimalizia kusema Mganga huyo.  

Baada ya kureja Morogoro  Fundi huyo alikuta hali nyingine tofauti kwa mwanaye ambaye licha ya jeraha lake la suna kuchelewa kupona, kiumbe huyo asiye na hatia amepata tatizo lingi la sikio  kutoa usaha na harufu mbaya.

 “Kama hiyo haitoshi Usiku licha ya baridi kali mwanangu pekee hatakia kulala na nguo wala kujifunika shuka, anataka kulala mtupu, na hataki kulala kwenye kitandani anataka kulala chini ya sakafu akiwa uchi wa mnyama mkimvisha nguo na kumlaza kitandani hamlali atalia usiku kucha”alisema Fundi huyo kwa sauti ya upole.

Siku iliyofuata Fundi huyo aliamua kumsimulia mkewe majibu  ya Mganga je Mkewe  ameayapokeaje majibu hayo, atakuwa upande wa Mume wake kuondoka hapo kwa bibi yake au atakuwa upande wa bibi yake aendelee kusalia hapo.?

Sehemu ya nne ya stori hii inamajibu ya maswali hayo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...