Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 5, 2023

VIBAKA WADAIWA KUIBA VIFAA VYA UTANGAZAJI MSIKITINI, WAPEWA SIKU 4 KUVIREJESHA KABLA YA DUA LA KUMUOMBA MUNGU KUSOMWA.

                       Shehe Ally Omar.

 Mchawi Mwambeta akihojiwa jana na Mtandao huu.


     Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Watu wasiofahamika wanaodhaniwa kuwa ‘Vibaka’ wanadaiwa kuingia Msikiti Mkuu wa Morogoro’uliopo barabara ya Boma’ Maarufu ‘Msikiti wa Boma Road’na kuiba vipaza sauti vinavyotumiwa na Mashehe kupiga hadhana Muda wa swala unapofika.

Tukio hilo la kustaajabisha lililofanywa na watu hao wasio na hofu ya Mungu limetokea Mwanzoni mwa wiki hii.

Mara baada ya kutokea kwa wizi huo  taarifa zilisambaa kwa kasi  maeneo mbali mbali ya Mji wa Morogoro zikidai Vibaka hao wameiba Mixer Machine, Speaker na Mic.

Kufuatia ubwa wa habari hiyo Mwandishi wa habari hizi kaingia Mzigo na kuzungumza na watu mbali mbali wakiwemo Mashehe.

Wa kwanza kupatikana alikuwa Mhadhini Mkuu wa Msikiti huyo uliopo barabara ya boma inayoelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro’lkulu ndogo’ Shehe Ally Omari ambapo alipohojiwa alisema.

”Ni kweli Shekidele juzi watu wameingia hapa Msikitini wameiba vipaza sauti’Mic’ lengo lao lilikuwa kuiba vifaa vyote vya utangazaji wameshindwa kuiba Speaker kwa sababu ilikuwa juu sana na Mixer Machine tuliitengenezea Sanduku la Chuma”alisema Shehe huyo.

Alipoulizwa wamechukua hatua gani kuhusiana na tukio hilo amesema.

”Tumetoa tangazo la siku 4 kwa watu waliochukua vifaa hivyo  wavirejeshe na siku hizo 4 zinafika tamati kesho Alhamisi[leo] kama hawakufanya hivyo ljumaa tutasoma dua ya kumshitakia Mwenyezi Mungu”alisema shehe Omar.

Baada ya kutoka Msikitini hapo Mwandishi wa Mtandao huu alitinga maeneo ya Mji Mpya na kukutana na Mmoja wa Mashehe wa Msikiti wa Mwembesongo Shehe Mussa Makalla alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa dua ya kumshitakia Mungu alisema.

”Maombi ya dua kupitia watu waliopigana vita vya Badri [Ahlul Badri]. Maombi mengine ni dua ya Kunut”alisema Shehe Makalla na kuongeza.” Unaposoma Ahlul Badri unawataja wale watu wapatao 3 waliopambana na watu zaidi ya 100 wakiipigiania Uislam walipata dhawabu kubwa kwa mwenyezi Mungu na walipofariki majina yao yamebandwakwa Maka, hivyo dua hiyo inaposwana yanatajwa majina ya mashujaa hao wa dini ya kiislama na mwenyezimu Mungu anapokea dua hiyo”alisema Shehe Makalla.

Taarifa zinadai hii si mara ya kwanza  vibaka kuiba vifaa vya utangazaji kwenye Msikiti huu imeelezwa mwaka 1979 vibaka waliingia kwenye msikiti huo na kuiba Mixer Mashine, Speaker na Mic.

Kufuatia taarifa hizo Mwandishi wa habari hizi aliwatafuta wazee wazaliwa wa mkoa wa Morogoro kuelezea tukio hilo.

Mtandao huu ulitinga tawi la Simba lililopo Ofisi Kuu ya CCM Kata ya Mji Mpya ambapo wazee wengi wazaliwa wa mkoa wa Morogoro Mashabiki wa Simba hupenda kuketi katika tawi hilo wakinywa kahawa na kucheza bao.  

         HUYU HAPA MZEE MWAMBETA.

Mwandishi- Heshima yako Mzee wangu, naomba kukufahamu kwa majina yako.

Mzee. Naitwa Mchawi Mwambeta.

Mwandishi. Kicheko,Kwa nini uitwe Mchawi?

Mwambeta. Hayo ndiyo majina yangu kamili ndio maarufu hapa Morogoro na Dar es salaam.

Mwandishi. Ok ujio wangu hapa juzi vibaka wanadaiwa kuingia msikiti Mkuu wa Boma Road na kuiba vifaa vya utangazaji, nasikia hii sio mara ya kwanza miaka ya nyuma waliiba tena vifaa hivyo,je kama mzee wa Morogoro unakumbuka ni mwaka gani wizi huo ulifanyike na nini kilitokea  baada ya wizi huo?

Mwambeta. Nakumbuka ilikuwa mwaka 1979 baada ya kumtwanga Nduli ldd Amin watu waliingia Msikiti wa Boma Road wakaiba Vifaa vya utangazaji na kwenda kumulizi Mwanamuziki Maarufu sana hapa Morogoro.Tanzania na Afrika kwa ujumla[anamtaja jina]mashehe wakatoa tangazo kwamba mtu aliyeiba au kununua arudishe kwa hiyari yake ndani ya siku 7 muda huo ukifika vifaa havijarudishwa wanasoma dua la kumshitakia mwenyezi Mungu.

Mwandishi. Je vitu hivyo vilirudi ndani ya muda huo au la?

Mwambeta. Havikuludia na mashehe wamesoma dua kilichotokea baada ya dua hilo kusomwa watu moja baada ya mwingine kuanzia walioiba, madalili na aliyenunulia kwa maana ya huyo Mwanamuziki anamtaja tena jina] wote wamekufa huyo[mwanamuziki anamtaja jina alipata ajari Nairobi Kenya kafa hapo hapo wenzi aliokuwa nao kwenye hilo gari wote wamepona.

 Hawao walioiba nawaone huruma kama kuna mtu anawajua au wanasoma Mtandao wako warudishe mali hiyo ya Mungu kabla siku hiyo ya ljumaa.

Mwandishi. Asanye Mzee wangu kwa ushirikiano ngoja nikutandike Picha moja kusindikiza maneno yako.

Mwambeta. Ok Piga tu hiyo Picha.

Mtandao huu umeshindwa kutaja jina la Mwanamuziki huyo ambaye hadi leo hii nyimbo zake zinapendwa na wengi kwa sababu hakuna taasisi ya serikali au ndugu wa Mwanamuziki huyo aliyethibisha madai  hayo.

Kwenye tukio hilo la juzi Mwandishi wa Mtandao huu atalifuatilia kujua Mwisho wake hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu siku zote.

Mwaka jana Vibaka wanadai kuvunja kanisa  Katoliki Parokia ya Modeko Mkoa hapa na kuiba vikombe na vibakuri vya dhahabu vinavyotumika kuhifadhia Mwili na damu ya Yesu’Sakramanti  Takatifu’baada ya tukio takribani mwenzi mmoja waumini wa kanisa hilo waliabudu nje ya kanisa.

Hii natokana na Imani ya dhebubu lao kwamba kanisa limenajisiwa kwa kukosekana kwa vifaa hivyo.

                    

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...