Kikosi cha Obama Fc
Emmanuel Pius akiruka juu akipiga Free Eda'Mpira wa Kichwa
Cheki Mohamed lssa alivyokosa bao la wazi akiwa uso kwa uso na kipa wa Obama
....Mali hiyooo inatoka senti meta chake langoni mwa Obama,huku Mohamed lssa akishangaa asiamini kilichotokea
Beki kisiki wa Obama Nassoro Chollo akiruka hewani kama njiwa kuokoa hatari lakoni mwake
Cheki beki wa Obama Collo aliyelala chini akimuangusha kwenye kiduara cha pelanati mshambuliaji hatari wa Black People Emmanuel Piusi aliyelala chini akinyoosha mkono kumuomba refa pelnat, hata hivyo refa aliyekuwa jirani kabisa na eneo la tukio kama anavyoonekana pichani alitwanga na kupeta akigomea ombi la mchezahi huyo.
Kiuongo 'Fundi'wa Black People' Mjeshi' Zuberi Dabi mwenye kipara akimpa pole kipa wa Obama. ifahamike Mwanajeshi huyo ni mchezaji tegemo wa timu ya Mashujaa ya Kigoma inayomilikiwa na jeshi la wananchi wa Tanzania'JWTZ' na juzikati alicheza kwenye mchezo dhidi ya ndugu zao wa JKT Tanzania uliopigwa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.na mashujaa kupokea kichapo cha bao 1-0.
Mara baada ya gemu hiyo Mwandishi wa Mtandao alimfuata Dabi na kumuliza kuliko yuko kwenye ndondo Cup." Shekidele baada ya gemu yetu ya shinyanga tutacheza tena octobar 29. hivyo uongozi umetupa likizo fupi kuja kuona familia"alisema mjeshi huyo ambaye ni Mkazi wa Kichangani Manispaa ya Morogoro. lfahamike kaka yake anyeitwa Nassoro Dabi naye ni mchezaji wa zamani wa Polisi Morogoro ambaye kwa sasa ni Askari Polisi mkaoni Morogoro.
Wamuzi mastaa wa ligi kuu Tanzania Bara wakifuatilia fainali hiyo ya ndondo jana baada kuona kamera za Mtandao huu walitabasamu.
Kutoka kushoto ni Raphael lkambi ambaye juzikati alichezesha mchezo wa ligi kuu kati ya Tabora United na Prinson uliopigwa dimba la Ally Hassan Mwinyi Tabora. mwenye koti ni refa wa daraja la kwanza Kassim Saleh Boko na mwenye nguo ya njano pia ni refa wa daraja la kwanza Juma Ramadhan, wengine ni marafiki wa marefa hao,
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
FAINALI ya Michuano ya The Gunners Super Sixstin’Ndondo Cup 2023’kati ya Obama Fc ‘Chuma cha Mjerumani’kutoka Kata ya Kiwanja cha Ndege na Black People’Taifa la Watu Weusi’ Kutoka ‘Jijinga Kaloleni’ Kata ya Mji Mpya, imevunjika dakika ya 84 baada ya kundi la Mashabiki wa Black People kuvamia uwanja wakiwalalamikia wamuzi waliolikataa bao .
Gemu hiyo ya fainali imepigwa jana Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro huku Obama wakijipatia bao hilo pekee dakika 8 kupitia kwa mshambuliaji hatari Mrisho Said’Ziko wa Kilosa’ ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga Hayati Said Mrisho’Ziko wa Kilosa.
Mara baada ya kufungwa bao hilo Vijana wa Black People wakiongozwa na mchezaji nyota wa ligi Kuu Zuberi Dabi anayekipiga Mashujaa ya Kigoma inayoshiriki ligi kuu walilishambulia lango la Obama kwa muda mrefu huku wakikosa mabao ya wazi.
Dakika 28 refa akilalamikiwa kwa kuwanyima Pelnati ya wazi Black baada ya Emmanuel Pius kuangushwa ndani ya boksi na beki wa Obama Nassoro Chollo.
Licha ya mapungufu hayo ya Mwamuzi Jeshi hilo la taifa la watu weusi kutokea kipande cha Mji Mpya waliendelea kulishambulia lango la Obana kama nyuki.
Juhuzi hizo zilizaa Matunda yaliyotafunwa na marefa dakika ya 84 baada ya winga Mohamed lssa kuchonga krosi iliyookolewa kwa kichwa hafifu na beki mmoja Obama, mpira huo ulitua kichwani mwa mshambuliaji wa Black People Emmanuel Pius aliyetumbukiza mpira wavumi.
Chaajabu Mshika kipendera namba moja ‘ Line One’aliinua kipendera akidai mfungaji alikuwa eneo la kuotea ’Off Side’.
Hali hiyo iliwapandisha hasira mashabiki wa Black People walioamua kuvamia uwanja kwa lengo la kuwauliza waamuzi hao sababu za kulikataa bao hilo muda huo wa Magharibi jua likizama.
Waamuzi hao baada ya kulioka kundi hilo la Taifa la watu weuzi likivamia uwanja wametimu mbio kama swala anayefukuzwa na simba wakatoka nje ya uwanja kabisa ya uwanja kufuatia mageti kuwa wazi muda huo saa 12 na robo na mchezo huo ukaishia hapo.
Maaskali wawili waliokuwepo uwanjani hapo kulinda usalama walijitahidi sana kuwaokoa waamuzi hao na kama sio uwepo wa maafande hao wa ‘Foda fasta’ huenda hali ingekuwa mbaya zaidi kwa waamuzi hao.
Kwa sasa wadau wa soka wanasubiri maamuzi ya kamati ya mashindano hayo itaamuani nini juu ya hatima ya mchezo.
Mtandao huu pia unafuatilia maamuzi wa kamati hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kujua kilichoamuliwa na kamti.
Cheki picha zaidi za matukio ya gemu hiyo hapo chini ya stori hii, ikiwemo sababu alizotoa mchezaji huyo wa Mashujaa kukipiga kwenye ndondo Cup.
No comments:
Post a Comment