Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, October 3, 2023

UDAKU SPESHO. HOUSE GIRL AFARIKI DUNIA WAZAZI WASHINDWA KUSAFIRISHA MWILI.


 


                  Na Dustan Shekidele.Morogoro.

INASIGITISHA SANA. 

Mfanyakazi wa kike wa kazi za ndani Yaya au kwa kimombo’House Girl’ amefariki dunia ghafla eneo lake la kazi Kata ya Mazimbu Mkoani hapa, huku wazazi wake wanaoishi Sumbawanga wakitoa ruhusa  binti yao kuzikwa Morogoro baada ya kukosa uwezo wa kusafiri mwili wa mpendwa mtoto wao.

Taarifa zilizopatikana eneo la msiba zinadai ‘Yaya’ huyo amefariki dunia ghafla juzi.

Baada ya kupokea taarifa za tukio hilo la kuhudhunisha Mdakuzi wa Mtandao huu aliingia kazi ambapo mashuhuda wa tukio hilo walidai bint huyo wa kazi aliyekuwa akiishi vizuri na bosi wake amezimika kama mshumaa.

” Inasigitisha sana bint huyo aliyekuwa akifanya kazi  za ndani kwa rafiki yangu amefariki dunia ghafla juzi na tunazika leo Jumanne saa 7 Mchana, baada ya wazazi wake kutoa ruhusa ya kuzikwa hapa kufuatia  kukosa uwezo kwa kusafirisha maiti kutoka Morogoro mpaka kwao Sumbawanga”alisema shuhuda huyo na kuendelea 

kufunguka. Kiukweli inauma sana binti huyo alifanya kazi kwa huyu rafiki yangu zaidi ya miaka 8 na walikuwa wakiishi kwa Upendo Mkubwa kama mtu na mdogo wake.

 Miaka minne iliyopita huyo dada wa kazi kapata ujauzito  alipata wasisi wakumuambia bosi wake akihofia anaweza kutimuliwa kazi na mimba yake, baada ya kuona tumbo linaanza kuchomoza kaamua kumwambia bosi wake.

Alipopewa taarifa hizo nzito rafiki yangu alimtia moyo mfanyakazi wake akimwambia asiwe na wasi wasi aendele na kazi na muda wa kijifungua ukifika atamsaidi mahitaji yote.

Baada ya kujifungua bosi wake alimtia nguvu akimwambia asihofu mtoto tutamlea hapa nyumbani na Mungu atamsimamia atakua na atacheza na hawa wenzie.

Mtoto alipotimiza miaka 2 bosi wake kampa ushauri kwamba ampeleke watoto  Sumbawanga wazazi wake wakamuone mjukuu wao.

Bint huyo kafurahia ushauri huo mwisho wa mwezi alipopokea mshahara wake,bosi wake na kamfungashia na zawadi za kuwapelekea wazazi wake. Amekaa huko kama wiki mbili kareja Morogoro na mtoto wake huyo wa kiume anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka  4.

Tunashangaa bint huyo juzi amefariki ghafla hakuumwa wala nini, bosi wake kawapigia simu wazazi wake wamedai hawana uwezo wa kusafiri maiti hivyo wametoa ruhusa azikwe hapa hapa Moro, hivi tunavyoongea  mama mdogo wa marehemu yuko njiani anakuja kuzika na baada ya mazishi ataondoka na mtoto wa marehemu.”alimalizia kusema shuhuda huyo. 

 Mtandao huu unatoa pole za dhati kwa wafiwa, wazazi wa marehemu na bosi wa marehemu aliyeishi vizuri na mfanyakazi wake ni wachache sana wenye moyo kama huo. 

 Kwa tukio hilo la bint huyo kupata Mimba eneo la kazi baadhi ya mabosi wangemfukuza kazi lakini kwa bosi huyo baada ya kupokea taarifa hizo alimtia moyo mtumishi wake, na kuishia naye akiwa na mtoto wake hadi kifo kinamkuta, 

Kipekee Mdakuzi wa Mtandao huu anaipongeza sana familia hiyo kwa moyo wao wa Upendo na Mungu na MwenyezI Mungu mwingi wa Rehema atawalipa mara dugu.                       

Kwa vile Mdakuzi hakufanikiwa kuzungumza na wahusika hivyo ameandika habari hii kidakuzi bila kutaja jina la mtu hadi hapo atakapofanikiwa kuzungumza na wahusika.

Muda huu Mwandishi wa Mtandao huu baada ya kuguswa na kifo hicho anajiandaa kwenda kushiriki mazishi hayo.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana  lihimidiwe.

”Mwendo umeumalizi House Girl nenda salama tutaonana baadae”

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...