Msikiti Mkuu wa Morogoro
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Takribani wiki mbili zilizopita watu wasiojulikana walidaiwa kuingia Msikiti Mkuu wa Morogoro na kuiba Vipaza Sauti ’Mic’, baada ya kutokea kwa wizi huo Viongozi wa Msikiti huo walitoa muda wa siku 5 kwa aliyechukuwa vifaa hivyo kuvirejesha kwa hiyari yake kabla hawajasoma dua la kumshitakia Mwenyezi Mungu.
Baada ya kutokea kwa wizi huo Mtandao Pendwa wa Shekidele uriripoti habari hiyo kwa kina na kuahidi kufuatia kujua kama wahusika watarudisha Vifaa hivyo baada ya tangazo hilo au la.
Na kama hawajaludisha dua hiyo imesomwa?na imewapata wahusika? Wadau wengi wa Mtandao huu walifuatilia habari hiyo na wengi walimpigia simu Mwandishi na wengine kumfuata ‘ln boksi’ wakiulizia mjesho wa stori hiyo iliyoumiza mioyo ya watu wengi wenye mapenzi Mema na Mwenyezi Mungu.
Kubwa zaidi mdau mmoja alionana uso kwa uso na Mwandishi wa habari hizi na kumueleza.
”Shekidele taarifa ile uliotueleza ya vibaka kuiba vifaa msikitini nilimsimulia rafiki yangu Dulla baada ya siku 2 Dulla kaniambia mtaani kwao kuna kijana alikuwa akifanya biashara ya kubani nyimbo ghafla amechanganyikiwa kawa chizi sijui malaria yamempanda kichwani au anahusika na wizi huo wa Msikitini”alisema Mdau huyo aliyefahamika kwa jina moja la TOT.
Juzi Mtumishi wawatu Mwandishi wa Mtandao huu alitinga kwenye msikiti huo uliopo barabara ya Boma Kata ya Mji Mkuu kwa lengo la kuzungumza na Mhadhini Mkuu wa Msikiti huo Shehe Ally Omari ambaye kwenye stori ya awari ndiye aliyezungumza na Mtandao huu juu ya wizi huo.
Hivyo Mtandao huu ulimtafuta shehe huyo kwa lengo la kutupa mrejesho, kwa bahati mbaya muda huo hakuwepo Msikitini hapo hivyo Mwandishi wa habari hizi aliamua kumtwangia simu ambapo alipopokea na kuulizwa maswali hayo alijibu kama ifuatavyo.
” Shekidele ni kweli siku tulizotoa simepita na vifaa vyetu havijaludishwa, kuhusu swali lako kwamba tumesoma dua la kumshitakia mwenyezi Mungu, jibu ni kwamba hatukusoma tumekaa na kutafakari tumeona vifaa hivyo ni vidogo na tunahisi waliochukua ni vijana wa maeneo ya hapa jirani”alisema Shehe huyo na kuendelea kufunguka.
”Badala yake tumesamehe na kumuachia Mungu atajua adhabu atakayo wapa, Wizi kama huo lilitokea hapa Msikitini mwaka 1978 licha ya tangazo kutolewa wahusika hawakurejesha vifaa hivyo,dua likasomwa tukampoteza mtu Maarufu hapa Morogoro na Tanzania kwa ujumla alikuwa Mwanamuziki, aliyeuziwa vifaa hivyo”alimalizia kusema Shehe huyo Maarufu mkoani Morogoro.
Mwandishi wa habari hizi anawapongeza mashehe hao kwa uamuzi wao huo wa busara huku ukiendelea kuwakemea wahusika waliokwapua vifaa hivyo vilivyokuwa vikitumika kupaza sauti Kuhadhini na kumtukuza Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment