Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, October 8, 2023

KILICHOMPONZA KUKU KWA MGANGA NI ILE RANGI YAKE

                              Dunstan Shekidele 'Mkude Simba;

 

Kilichomponza kuku kufika kwa Mganga wa Kienyeji ni rangi yake.

 Kilichomponza Manchester City leo kupokea kichapo kitakatifu cha bao 1-0 kutoka kwa washika mtumbu wa jiji la Maraha la Londoni Arsenal’Chama la Wana’ ni Jina lao.

lkumbukwe Arsenal inapokutana na Manchester United ‘Mashetani Wekundu’ kama Mbwa aliyemuona Chatu anajipeleka mwenyewe kwenye Mdomo wa Chatu anamezwa kama tonge la Ugari.

Juzi tu Arsenal kamchapa Manchester United bao 3-1, leo wadogo zao Manchester City wamepokea kichapo cha bao 1-0 huku wakipigiwa mpira mwingi uliomfunika Staa wao Haaland kawa kama lile joka la kibisa lililokosa sumu mbele ya mabeki ya Arsenal ambayo hadi sasa kwenye Ligi ya England haijapoteza mchezo yoyote.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...