Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 30, 2023

MWAKA MPYA MAMBO MAPYA. MWONEKANO MPYA KILAKALA SECONDARY


 


  Na Dustan Shekidele,Morogoro.

WAKATI Imebaki takribani miezi miwili  kuuga Mwaka 2023 na kuingia Mwaka Mpya wa 2024,Jumuiya ya Wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasichana [Kilakala Girls Secondary School] ‘KILASEPA’ chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa Jumyiya hiyo  Dr. Kelvin Njunwa wamefanya Ukarabati wa uzio na  Gate kuu la kuingia shuleni hapo na lile Geti la pande wa  Nyuma.

Wazazi hao wameamua kufanya ukarabati huo kwa lengo la kuipa hadhi shule hiyo kongwe na Maarufu nchini Tanzania ambapo baadhi ya viongozi wengi maarufu nchini wamesoma  shule hiyo iliyopo chini ya Milima ya Uluguru Kata ta Kilakala Manispaa ya Morogoro.

 lfahamike pia Upendo Shekidele ambaye ni Mdogo wake Mwandishi wa habari hizi. alihitimu kidato cha sita katika shule hiyo.

Uongozi wa KILASEPA Umesapoti  Juhudi za Rais Dr. Samia Suluu Hassan chini ya Uongozi wake  Umejenga Mabweni Mapya 3 na Madarasa Mapya 8 yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 450.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mageti hayo kwa uongzo wa shule hiyo,Mwenyekiti wa Jumiya hiyo Dr Njunwa aliushukuru  Uongozi wa Shule ya Kilakala kwa kusimamia  Vizuri

ukarabati huu.

“Kwa niaba ya Jumuiya wa Wazazi wa shule hii tunaushukuru Uongozi wa shule kwa kusimamia kwa kwa weledi kazi hii,Kipekee tumshukuru Mkuu wa Shule Madam  Mary Lugina  na Makamu wake Mr. Mkangwa” alisema Dr Njunwa Msomi anayemiliki PHD ya Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine’SUA’ 

Wakati akitunukiwa PHD hiyo huku akisindikizwa na Matarumbeta takrinani miaka 3 iliyopita Mpiga Picha Maarufu wa Mtandao huu anayemiliki Kamera za Kisasa ambaye pia ni ’Photo Journalist’ ndiye aliyepewa tenda na familia ya Profesa Njunwa kupiga Picha matukio yote ya hafra hiyo iliyofanyika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro’MSJ’uliopo Mkundi Manispaa ya Morogoro.

Saturday, October 28, 2023

MIDOMO YA MALAYA.


 



Mithali 5.1-3

“Mwanangu  sikiliza hekima yangu Tega sikio lako Mzisikie akili zangu.

Upate kulinda busara  na Midomo yako iyahifadhi maarifa.

Maana midomo ya malaya hudondoza asali,na kinywa chake ni laini kuliko mafuta” Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili ya October 29.

                         CAPTION


Mama yangu Mzazi Bi, Tumain Samwel Juma. Mrs Shekidele.

Mama yetu Kipenzi mimi na ndugu zangu tunaendelea kuishi vizuri tukiongozwa na hekima zako ulizotupatia toka tukiwa wadogo.

Kwa sasa Mama  unaumwa tunaendelea kumuomba MUNGU akuponye.

Pichani  Bi Mkubwa nilikubeba kwenye Pikipiki nikakupeleka hospital kupata matibabu, niyo ni Moja ya busara ulizonifundisha niishi nayo siku zote za Maisha yangu.

 Kwa Msaada wa Mungu nitaendelea kufanya hivyo kwa watu wote mpaka naingia kaburini.

Wednesday, October 25, 2023

MREJESHO STORI VIBAKA KUDAIWA KUKWAPUA VIPAZA SAUTI MSIKITINI.

                                      Shehe Ally Omari

                Msikiti Mkuu wa Morogoro


          Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Takribani wiki mbili zilizopita watu wasiojulikana walidaiwa kuingia Msikiti Mkuu wa Morogoro na kuiba Vipaza Sauti ’Mic’, baada ya kutokea kwa wizi huo Viongozi wa Msikiti huo walitoa muda wa siku 5 kwa aliyechukuwa vifaa hivyo kuvirejesha kwa hiyari yake kabla hawajasoma dua la kumshitakia Mwenyezi Mungu.

 Baada ya kutokea kwa wizi huo Mtandao Pendwa wa Shekidele uriripoti habari hiyo kwa kina  na kuahidi kufuatia kujua kama wahusika watarudisha Vifaa hivyo baada ya tangazo hilo au la.

Na kama hawajaludisha dua hiyo imesomwa?na imewapata wahusika? Wadau wengi wa Mtandao huu walifuatilia habari hiyo na wengi walimpigia simu Mwandishi na wengine kumfuata ‘ln boksi’ wakiulizia mjesho wa stori hiyo iliyoumiza mioyo ya watu wengi wenye mapenzi Mema na Mwenyezi Mungu.

Kubwa zaidi mdau mmoja alionana uso kwa uso na Mwandishi wa habari hizi na kumueleza.

”Shekidele taarifa ile uliotueleza ya vibaka kuiba vifaa msikitini nilimsimulia rafiki yangu Dulla baada ya siku 2 Dulla kaniambia mtaani kwao kuna kijana alikuwa akifanya biashara ya kubani nyimbo ghafla amechanganyikiwa kawa  chizi sijui malaria yamempanda kichwani au anahusika na wizi huo wa Msikitini”alisema Mdau huyo aliyefahamika kwa jina moja la TOT.

Juzi Mtumishi wawatu Mwandishi wa Mtandao huu alitinga kwenye msikiti huo uliopo barabara ya Boma Kata ya Mji Mkuu kwa lengo la kuzungumza na Mhadhini Mkuu wa Msikiti huo Shehe Ally Omari ambaye kwenye stori ya awari ndiye aliyezungumza na Mtandao huu juu ya wizi huo.

Hivyo Mtandao huu ulimtafuta shehe huyo kwa lengo la kutupa mrejesho, kwa bahati mbaya muda huo hakuwepo Msikitini hapo hivyo Mwandishi wa habari hizi aliamua kumtwangia simu ambapo alipopokea na kuulizwa maswali hayo alijibu kama ifuatavyo.

” Shekidele ni kweli siku tulizotoa simepita na vifaa vyetu havijaludishwa, kuhusu swali lako kwamba tumesoma dua la kumshitakia mwenyezi Mungu, jibu ni kwamba hatukusoma tumekaa na kutafakari tumeona vifaa hivyo ni vidogo  na tunahisi waliochukua ni vijana wa maeneo  ya hapa jirani”alisema Shehe huyo na kuendelea kufunguka.

”Badala yake tumesamehe na kumuachia Mungu atajua adhabu atakayo wapa, Wizi kama huo lilitokea hapa Msikitini mwaka 1978 licha ya tangazo kutolewa wahusika hawakurejesha vifaa hivyo,dua likasomwa tukampoteza mtu Maarufu hapa Morogoro na Tanzania kwa ujumla alikuwa Mwanamuziki, aliyeuziwa vifaa hivyo”alimalizia kusema Shehe huyo Maarufu mkoani Morogoro.

Mwandishi wa habari hizi anawapongeza mashehe hao kwa uamuzi wao huo wa busara  huku ukiendelea kuwakemea wahusika waliokwapua vifaa hivyo vilivyokuwa vikitumika kupaza sauti Kuhadhini na kumtukuza  Mwenyezi Mungu.                         

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...