Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, September 24, 2023

UDAKU SPESHO.BODA BODA ADAIWA KUMUUA MWENZAKE CHANZO DEMU.

 Boda boda ya Mwandishi wa Mtandao huu 'Ez Come Ez Go'


Na Mdakuzi, Dustan Shekidele,Morogoro. 

Vijana wawili wanaofanya biashara ya kupakia abiria kwenye Pikipiki’Maarufu Boda boda’wanadaiwa kucharazana mapanga na kuchomana bisibisi hali iliyopelekea mmoja  kufariki dunia na mwingine kulazwa hospital huku akiwa na ’bangili’ Pingu mkononi akituhumiwa na Mauaji.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku Maeneo ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.huku chanzo kikidai kwamba boda boda hao walikuwa wakimgombea mwanamke.

Mdakuzi wa Mtandao huu ambaye pia ni Mkazi wa Mji Mpya, anawafahamu vizuri wahusika wote watatu kwa maana ya boda boda hao na demu huyo anayedaiwa kuwachanganya wafukuza upepo hao’Boda boda.’

Kwa sababu habari hii haijakamilika kwa maana ya kuzungumza na mamlaka husika Mwenyekiti wa Mtaa, Polisi, Madaktari na ndugu wa pande zote tatu hivyo japo nawafahamu wahusika hao sitotaja majina yao hadi hapo nitakapokamilisha mahojiano na wahusika niliowataja hapo juu.

Kwa sasa habari hii inaandikwa kwa mfumo huu wa Udakuzi kwa kutotaja jina la mtu yoyote hadi hapo itakapo ‘Balance Story’.

Wakizungumza na Mdakuzi wa Mtandao huu Mashuhuda wa tukio hilo walifunguka yafuatayo.

“ Huyo Mwanamke’wanamtaja jina anafanya biashara hapa soko la Mji Mpya na boda boda hao pia wanapaki hapa jirani na soko eneo la wauza samaki wa kukaanga Pale njia panda.

Boda mmoja [anamtaja jina] majira ya saa 3 usiku boda boda wa pili [anamtaja jina] alimuliza mwenzake kwa nini anatembea na demu wake  zogo likaanzia hapo wakaanza kuzichapa kavu kavu.

Baadae kila mmoja kakimbilia silaha mmoja kafanikiwa kupata Panga na mwingine bisi bisi”.walisema mashuhuda hao na kuendelea kudadavua.

Aliyeshika panga kweli kampelekea mwenzie  mkononi jamaa kuona hivyo naye kamtumnbukiza bisi bisi tumboni jamaa kaanguka chini katingisha miguu badae kafariki dunia  .

Tunashangaa wote wawili hawana haki na Mwanamke huyo kwa maana hakuna aliyetoa posa ya kuoa, hivyo kumuonea wivu kiasi cha kuchapata mapanga na kutoana roho  sio sawa. 

Wengine wamenyang’anywa wake wa ndoa wameepisha Ugomvi wamemshitakia Mungu, mbona wanawake wako wengi.

Pia tutoe rai kwa baadhi ya wanawake kuacha tabia ya kuchanganya wanaume ‘kugema’ pesa huku na kule wakiita ‘ATM’ Madhara yake ndio haya” walimalizia kusema mashuhuda hao.

 Kesho Jumatatu panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mwandishi wa habari hizi ataendelea kufuatilia habari hii kwa ukamilifu hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...