Timu ya Foutain Gate Fc
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
PAZI la Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara Maarufu ‘Champion Ship’limefunguliwa Jumamosi iliyopita, huku Mashabiki wa Morogoro wakishindwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao ya Foutain Gate licha ya kupewa ofa ya kuingia bure uwanjani.
Timu hiyo ya Foutain Gate iliyonunuliwa na Mfanyabiashara Mmoja mkoani Morogoro ikitokea jijini Dodomam ilianza ligi hiyo Jumapili kwa kupambana na Ruvu Shooting Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katika kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mchezo huo Uongozi wa timu hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Soka Mkoa Morogoro’MRFA’ kwa pamoja walimua mashabiki kuingia bure.
Licha ya Mageti kuwa wazi toka saa 8 mchana mpaka saa 12 jioni bado mashabiki wengi wameshindwa kujitokeza kuisapoti timu hiyo, hata hivyo mashabiki hao wachache wenye moyo safi waliishangilia timu yao kwa muda wote wa dakika 90 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa Mtandao huu aliingia kazini na kufanya uchunguzi wa kina wakwa lengo la kubaini sababu za mashabiki wengi kukacha kuingia uwanjani kuisapoti timu yao mkoani mwao ya Foutain Gate licha ya kupewa ofa ya kuingia bure.
Baadhi ya mashabiki walioojiwa na Mtandao huu kwa nyakati tofauti kwenye mitaa mbali mbali ya Mji wa Morogoro walionekana kuelekeza lawama zao kwa Viongozi wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’ na Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ wakidai Viongozi wa vyama hivyo wanashindwa kuzisimamia timu.
WASIKIE WADAU HAO.
“Morogoro tunapenda Mpira na miaka mingi tumejitoa sana kuzisapoti timu zetu za Mkoa, tatizo la sasa ni viongozi wa Wilaya na Mkoa kushindwa kuzisimamia timu na kusababisha timu kuuzwa na nyingine kushuka madaraja.
Tunamifano iliyohai Wadau wa Soka Kata ya Mwembesongo eneo la Mafisa walianzisha timu ya Burkinafaso wamepambana mpaka imefika daraja la kwanza imecheza kwenye daraja hilo kwa miaka 8 mfurulizo bila kupanda ligi kuu wala kushuka daraja, baada ya kukosa sapoti timu hiyo imeshuka madaraja hadi daraja la tatu.
Vile vile wadau wa soka Wilaya Kilombero eneo la Mkamba walianzisha timu ya Mkamba Ranger nayo ilicheza ligi daraja la kwanza kabla ya kushuka madaraja baada ya kukumbwa na ukata na kukosa sapoti ya kutatua tatizo hilo.
Kama hiyo haitoshi Wafanyabiashara wa Soko la Matunda la Mawezi walijikusanya na kuanzisha timu ya Mawenzi Market iliyoshiriki ligi daraja la kwanza kwa misimu takribani 3 baada ya kukubwa na ukata hali iliyopelekea viongozi na wanachama kuamua kuipiga bei timu hiyo isije ikawafia mikononi kama wenzao wa Mkamba na Burkina”.alisema Mdau wa Soka aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Msimbe ambaye aliongeza kutoa maoni yake akisema
Nao wafanyabiashara wa Soko la Saba saba walianzisha timu ya Saba Saba united iliyoshiriki ligi daraja la Pili kabla nao kukumbwa na ukata na kushuka hadi daraja la tatu.
Kingine kilichotumiza sisi wadau wa Soka tulipambana kuisapoti Polisi Morogoro ilivyopanda ligi kuu imehamishiwa Moshi na kubadilishwa jina ikiitwa Polisi Tanzania.
Na hii Foutain Gate ya Dodoma awari waliutumia uwanja wa CCM Gairo hapa Morogoro baada ya kuona misimu miwli hawapandi ligi kuu msumu huu wamesogea hapa Mjini wakiomba sapoti yetu nao wakipanda ligi kuu wanahamia kwao Dodoma mpaka tupate uhakika kweli hii timu ni yetu hapa Morogoro ndio tutoe nguvu zetu kuisapoti ”alimalizia kusema Msimbe.
Akizungumzia madai hayo Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Emmanuel Kimbawala aliwatoa hofu wadau hao kuhusiana na timu hiyo ya Foutain Gate.
”Hii timu ni yetu sisi wana Morogoro imenunuliwa na Mdau wa Soka hapa Morogoro Bw Jerry anayeongoza shule ya Educare sasa Foutain Gate School ya Mkoani Morogoro, na timu hii iko kwenye mchakato wa kubadili jina itaitwa FGA Talent Fc ya Morogoro”alisema Katibu huyo.
Mtandao huu unaendelea kuwasihii wana Morogoro kusahau ya nyumba tuendelee kuosapoti timu yetu ya Foutain Gate, hata vitabu vya dini vinasema ukigeuka kuangalia ya nyuma unageuka jiwe la Chumvi, pia kuna kauli mbiu ya timu moja kubwa hapa nchini inasema “Daima Mbele nyuma Mwiko”
No comments:
Post a Comment