Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 11, 2023

LIGI DARAJA LA KWANZA, FOUTAIN GATE YAINYUKA RUVU SHOOTING.

                                        Kikosi cha Ruvu Shooting
                            Kikosi cha Foutain Gate
Waamuni wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili

Baada ya ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuanza TFF Taifa kupitia Mdhamini Mkuu wa ligi hizo 'Wazee wa Twiga Mwekundu' walitoa Bips kwa Waandishi wa habari za Michezo nchini, miongoni mwa Waandishi waliokabidhi kitendea kazi hicho ni pamoja na Mwandishi wa Mtandao huu Dustan Shekidele ambaye kwa mara ya kwanza jana alitinga Bips hiyo kwenye gemu ya Foutain Gate na Ruvu Shooting.

 




Cheki Winga hatari wa Ruvu Shooting Joseph Ludovic[kulia jezi nyekundu]akiasama mdomo kwa ‘Style’ ya kumtoka beki wa Foutain Gate Haruna Mgecha.



Beki wa Ruvu Shooting Haji lbrahim akiruka juu na kufunga bao la kwanza akiunganisha mpira wa kona huku kipa wa Fountain Gate Mussa Majuto naye akipaa hewani kuufuata mpira huuo bila mafanikio na kujikuta akifugwa  bao hilo.



Cheki refa akichungulia bao la pili la Foutain lililofungwa na Raymond Chamungu  anayeungana na wenzake kwenda kwenye kibendera kushangalia, wakati hao wakishangilia bao Nahodha wa Ruvu Haji lbrahimu alipiga magoti na kupiga ngumi chini kwa uchungu baada ya kipa wake Joel Mwamasika  kupitwa kirahisi na mpira uliozaa bao la pili.







Aisee cheki mshambuliaji wa Foutain Gate Raymond Chamungu alivyokosa bao la wazi akiwa yeye na kipa wa Ruvu Joel Mwamasika.

Baada ya kukosa bao hilo Chamungu alijitupa chini kwa uchungu na kulala hapo zaidi ya dakika moja jambo lililopelekea wachezaji wa Ruvu kumchongea kwa refa ambaye alimlima kadi ya njano kwa kosa  la kupoteza muda.

baada ya kupoteza nafasi hiyo ya wazi kahamia upande wa pili wa kupoteza muda, hawa ndio wachezaji wetu wa kibongo bongo.






Huyu naye yeye na kipa mpira umempira kakosa bao la wazi


 


Na Dustan Shekidele, Morogoro.

TIMU ya Fountain Gate ya Mkoani Morogoro,  imenza vyema Michuano ya Ligi daraja la kwanza’Champion Ship’ baada ya kuinyuka timu ya Ruvu Shooting ya Mkoani lringa kwa bao 2-1.

Gemu hiyo ya mzunguko wa kwanza imepigwa jana uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, huku Ruvu wakiwa wa kwanza kupata bao dakika ya 24 baada ya beki wa kati wa timu hiyo Haji lbrahim kufunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona iliyochingwa na Mocka Msafiri.

Baada ya kufungwa bao hilo Vijana wa Fountain Gate walitulia na kuliandama lango la wapinzani wako na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 42 kupitia kwa Seleman Simba aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa wa Ruvu Joel Mwamasika.

Wana wa Pakaya’Watoto wa nyumbani’ Fountain Gete waliongeza juhudi za kusaka ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani na juhudi hizo zilizaa matunda dakika 59 baada ya Raymond Chamungu kupachika bao 2 lililoipa alama 3 muhimu timu yake.

Katika hali ya kushangaza dakika ya 84 Chamungu tena akiwa yeye na kipa wa Ruvu alikosa bao baada ya kuti lake kali kutoka nje ya gori.

Baada ya kukosa bao hilo mchezaji huyo akijitupa chini na kukulala kwa zaidi ya dakika moja  jambo lililopelekea wachezaji wa Ruvu wakiongozwa na kipa wao kumvamia refa na kumuamulu ampe kadi mchezaji huyo kwako la kupoteza Muda.

Kweli baada ya mchezaji huyo kunyanyuka alilimwa kadi ya njano na kuamuliwa kutoka nje ya uwanja kisha kuomba tena kurejea uwanjani. Timu hizo mbili zinahistoria zimazofanana.

Mosi timu zote mbili zinatoka mikoa tofauti na kuhamia mkoa wa Morogoro, Foutain wanatokea Dodoma na Ruvu walioutumia uwanja wa Jamhuri Morogoro kwenye michezo yake ya Ligi kuu msimu uliopita wao wanatokea Mkoa wa Pwani.

Pili Msimu huu timu hizo zilipigwa bei, Ruvu imeuzwa mkoani lringa ambapo kwa sasa wako kwenye mchakato wa kubadili jina na kuitwa Lipuli Fc.

Huku Foutain Gate nayo ikiuzwa mkoani Morogoro nao wakiwa kwenye mchakati wa kubadili jina ikiitwa FGA Talent.

 Kama kawaida mtandao huu umekusanya matukio kadhaa kwenye mchezo huo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

Kwa sasa angalia picha mbali mbali za matukui ya gemu hiyo hapo chini ya stori hii.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...